Elections 2015 Kulinda kura: Wakili Peter Kibatala afungua kesi Mahakama Kuu

Elections 2015 Kulinda kura: Wakili Peter Kibatala afungua kesi Mahakama Kuu

Ninapoishi (nyumbani) ni mita chini ya mia moja kutoka kituo cha kupiga kura. Sijui itanibidi nihame na familia baada ya kupiga kura au itakuwa vipi? Wanajukwaa ninaomba ushauri.
Asanteni sana.
..,
Kaa nyumbani kwako lakini sio kulinda kura.usitumie vibaya uhuru wako kwa kuhamishia UKAWA yote humo
 
Polisi wanakuambia, mkusanyiko wowote ule unatakiwa kuwa na kibali.

Hivyo, kabla hamjabaki kwenye hayo maeneo mtakayobaki, hakikisheni mmepata vibali vya polisi ili kwa mujibu wa sharia., ila watu wakibaki bila kibali cha polisi, huo ni uvunjifu wa amani.

SIdhani kama ni hekima kuwaambia watu wabaki vituoni. Fikiria
1. Ukawa mmewaambia watu wenu wabaki
2. CCM watuambie watu tubaki
3. ACT wawaambie watu wao wabaki
4-8 na vyama vingine wawaambie watu wao wabaki

Je, nini kitatokea kwenye hayo makundi yatakayobaki kama sio uvunjifu wa amani? hivi mnafikiri amani ikivunjika na wewe utakatiwa ticket ya ndege kwenda nje au ni hao viongozi wanaowahamasisha tu ambao tayari wengi wao wanavisa za kwenda nje ya nchi tayari? akili za kuambiwa, changanyeni na za kwenu.

A QUOTE FROM JAMII FORUMS MEMBER CALLED UTAMADUNI
vitisho hivyo wapelekeeni mazezeta wenzenu wa fisiem, kila siku mitaani watu wanakusanyika kwenye misiba na harusi bila vibali iweje mkusanyiko wa kusubiria matokeo ya hatma ya maisha yao kwa miaka mitano ijayo ndio ihitahi hicho kibali?
 
Kwani ni nini majukumu ya tume siku ya kupiga kura? na hata kama itaonekana sawa bado kuna sheria ya mikusanyiko nayo inazuia mikusanyiko bila kibari ...hawa wenzetu Ukawa wana shida sana na yawezekana wakahonga hata majaji lakini wataisoma tu
 
Yehodaya acha mhemuko wa kushindwa kubali mabadiliko tartiiiibu. Sisi tutalinda kura zetu kwa gharama yetu,hatujasahau ya Mnyika,Mdee,Wenje na goli la nkono la blandes kule karagwe. Peope.........s
 
Kibali cha kusubiria mrejesho wa kura yako kaombe wewe,sisi tutasubiria mpaka kieleweke.
 
Madudu ni mengi tu ndani ya ccm!kuna mikakati ya makusudi rushwa pia ikitumika ili kujihakikishia ushindi lakini cha kushangaza watanzania wameshaamua. Hiyo ni barua iliyonaswa.
 

Attachments

  • 1444992713053.jpg
    1444992713053.jpg
    54.1 KB · Views: 508
Kwani nimara ya kwanza kupiga kura mbona tumekaa mita 200 na kura zikahesabika zikatangazwa. Yahodaya unastahili viboko tena vyanguvu. Tupige kura turudi nyumbani wahesabu wamalize wawatangazie akinanani na watu hawapo. Yahodaya hacha kunywa viroba. Kupiga kura nihaki ya raia kulinda haki yake ni lazima kwa mujibu Wa sheria.
 
Mkuu wala liberal approach haihitajiki kwani kifungu kipo wazi kabisa kuwa kukaa mita mia mbili toka sehemu ya kupigia kura sio kosa. Ila haisemi mkiwa hapo muwe kwa ajili ya kulinda kura. Kwa hiyo watu wakae mita hizo mia mbili ila polisi wakija wasiseme tupo hapa tunalinda kura hata kama mioyoni mwao lengo ni kulinda kura.

Hapo umenena.....
 
Mkuu wala liberal approach haihitajiki kwani kifungu kipo wazi kabisa kuwa kukaa mita mia mbili toka sehemu ya kupigia kura sio kosa. Ila haisemi mkiwa hapo muwe kwa ajili ya kulinda kura. Kwa hiyo watu wakae mita hizo mia mbili ila polisi wakija wasiseme tupo hapa tunalinda kura hata kama mioyoni mwao lengo ni kulinda kura.

Labda waseme tupo hapa kusubilia matokeo nani alieshinda au itakuwa kosa vitatembea virungu
 
Mtu mmoja anavunja sheria za nchi eti kwa sababu ni mkuu wa nchi. So stupid.
 
Hii italeta matatizo zaidi.At any moment,ikiwa mahakama itasema mkusanyiko hauruhusiwi,polisi watakuwa na justification.
 
Kingunge '' nguvu ya kuzuia ma​badiliko ni kubwa,ila nguvu ya kutaka mabadiliko ni kubwa zaidi''
 
Ndugu yangu hiyo ni hofu ya wengi kwani nao majudges ni wateule wao kwa maana ya ajira ingawa wakishawateua hawana uwezo wa kuwatimua. Tuombe mungu awe upande wetu.
Jaji yoyote yule hapa anatoa hukumu sahihi bila wasiwasi huku akipiga mluzi na akicheza cheza na htc yake coz JK at this point hana madhara kwake!
 
Back
Top Bottom