Naaam, eti hata rais wa nchi anavunja sheria live! Kwanini sheria hii walishindwa kubadili kwa hati ya dharula?
Hii inatokana na mtawala kutokuwa na weledi sababu ya kuamini kutawala kwa kupiga ramli na matunguli!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naaam, eti hata rais wa nchi anavunja sheria live! Kwanini sheria hii walishindwa kubadili kwa hati ya dharula?
Ni kesi ya dharura,over?Kesi itapangiwa muda wa kusikilizwa tarehe 26
ndio raha ya kua na viongozi watetezi na majasiri..
LAKINI
tatizo liko palepale
kesi ya ngedere kumpelekea nyani !!
jakaya amefeli miaka 10 anataka umaarufu kwa siku 10.
Hivi mnataka yatokee MAUAJI ya kina nani ili CCM Wapelekwe ICC??Je, na watoto wa kina Freeman Mbowe,Philemon Ndessapessa,Reginard Mengi,Edward Lowassa,Rostam Aziz na James Mbatia Watakuwepo?????!!Duniani hakuna HAKI DUNIANI.Unauawa na wanapelekwa ICC Wanashinda KESI unawaacha kina MBOWE Wanakula BATA huku wazazi wako wakiteseka.Uhuru Kenyata yupo HURU.Umenena sawia kabisa.Ila ningeshauri swala hili pia lifikishwe ICC.Vita ya kuisaka ikulu ni kali kwa hiyo ni lazima kusimama ikulu.
Tayari wakili jembe na nguli Peter Kibatala akiambatana na wanasheria nguli wa Ukawa Prof Safari, Mallya na Tundu Lissu asubuhi ya leo amefungua kesi mahakama kuu kuishitaki NEC kwa ukiukwaji wa sheria juu ya wananchi kukaa mita mia mbili na kulinda kura.
Kesi imefunguliwa under certificate of urgency nadhani kama sijakosea kwa kiswahili ni 'hati ya dharura' ili isikilizwe na tafsiri itoke kabla ya uchaguzi.Tayari jalada lishapelekwa kwa pilato na wanasheria nguli wa Ukawa wamejipanga kwa hoja za nguvu na ushahidi wa kutosha.
Pia jopo la wanasheria nguli wa UKAWA wameiomba mahakama kuu ya Tanzania kutoa tafsiri ya kisheria juu ya matamshi ya rais wa nchi kuwa alitumia mamlaka gani kuvaa kazi za tume.
Je kama mahali hapo ni puplic road inakuwaje. .
Usichokijua ni kuwa sheria ya Uchaguzi inasema siku ya kupiga kura hakutakuwa na mikusanyiko ya kisiasa.Mikusanyiko yote ya kisiasa mwisho wake ni siku ya mwisho wa kampeni ambayo ni tarehe 24 octoba 2015.Ukikusanya watu wako siku hiyo ya uchaguzi wawe wana UKAWA au CCM wakajikusanya mahali ni kosa kisheria.
Pili kwa mujibu wa sheria zinazohusu mikusanyiko ni lazima kutoa taarifa polisi kuwa kutakuwa na mkusanyiko mahali fulani na kwa lengo gani. Hivyo kama kurtakuwa na watu wenye lengo la kukusanyika popote inabidi wawasilishe maombi yao polisi wakijieleza wao ni akina nani ili wapewe ulinzi wa polisi
Tatu kuna sheria ya ardhi.Unaposema utakusanyika hapo kwenye mita 200 hilo eneo ni mali ya baba yako au mama yako? Huyo mwenye miliki ya hiyo ardhi karidhia? Hivyo kama kuna watu watakaotaka kukusanyika ni lazima wapeleke kibali cha mwenye eneo kuwa karidhia eneo lake litumike kwa mikusanyiko.Na kwamba mikusanyiko hiyo haitakuwa kero wala bugudha kwa wakazi wa eneo husika,majirani n.k Maana kama watu watajiamulia kukusanyika hiyo mita mia 200 bila mwenye eneo lake kuridhia ina maana ni uvamizi wa ardhi ya mtu bila ridhaa yake.Na huo ni uvunjifu wa amani kwenye eneo la watu.Hivyo Mahakama lazima iangalie maslahi ya wenye maeneo maeneo yao yasije vamiwa SIKU YA KUPIGA KURA NA KUKALIWA KWA MABAVU na hao wanaojiita walinda kura.
Polisi kwa kuliona hilo kuwa kutakuwa na uvunjaji sheria kwa watu kuvamia maeneo ya watu na kujikusanya wakasema kila mtu aende kwake asubirie kwake.Sababu vituo vya kupigia kura haviko mbali na makazi ya watu.Kwa nini watu wakae kwenye viwanja vya watu? Mahakama iliangalie hilo
Kwangu sikubali mtu akusanyike WALA KUWEKA MAKALIO YAKE KWENYE ENEO LANGU NITAITA DEFENDER NA GARTI LA WASHA WASHA HARAKA WAJE NA MABOMU NA VIRUNGU WAONDOE WAVAMIZI KWENYE ENEO LANGU.
Hawa akina KIBATALA wanataka kuleta vurugu na ugomvi kati ya wenye maeneo na hao watu anaotaka wakusanyike hizo mita mia mbili sababu sio kwao ni kwa watu.
Eti bila haya lowasa na mbowe wanatoa amri mkimaliza kura kaeni mita 200.Hilo eneo wanaloamrisha watu wakae ni la baba yake au mama yake lowasa au mbowe.Sheria ya ardhi iheshimiwe majaji msimamie hilo kwa maslahi ya wenye maeneo yao.Mkiwakubalia mnawaweka wenye maeneo matatizoni.
Sheria haitenguliwi kwa amri.
Waliotunga sheria hawakujua kuwa hizi mita ziko ardhini?