Kulingana na ushahidi wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa uliotolewa, Je unadhani maelezo ya Adamoo aliyoandikisha polisi yatapokelewa kama ushahidi..?

Tuna options zipi zaidi ya kusubiria huruma za jaji?
Options ziwe zinatambulika kisheria, kama kukata rufaa ni mojawapo, nje ya hapo hiyo experience kwa nchi yetu sijawahi kuiona.
 
Tuko sote mkuu.

My rhetoric question was only meant to show, all we have is to wait, hope and see. Certainly we can't influence it anyhow.

Indeed it has been good enough to shame them and accordingly. We now know more than we had ever known before.
 
1.Mshitakiw no 1 alionesha majeraha na makovu hata hivo bado anachechemea hii inamaana kwamba aliteswa.

2.Mshitakiwa no 2 alieleza Mahakama kuwa nae mshitakiwa namba moja aliteswa

Ikiwa Jaji atasimamia Haki bila shinikizo la waleta kesi basi utetezi wao utachkuliwa .
 
Uko sahihi
Mkuu rejea case ya uhaini miaka ya 80s mashahidi wa serikali wakiwa kina Mabere Marando na kina Dr. Mahiga. Washitakiwa kina Hatty MacGhee, na kina Hans Poppe.

Kulikuwa na mawakili wa utetezi wazuri tu (first class) kama kina Murtaza Lakha na kina Muccaddam.

Ushahidi ulikuwa umepatikana kwa mateso kama hivi hivi. Ushahidi ulipokelewa na kutumika mahakamani dhidi ya watuhumiwa pamoja na mapingamizi kama hivi hivi.

Karibu Tanzania ambako bila katiba mpya mihimili mingine inawajibika kwa ule mmoja uliojichimbia zaidi.

Bila katiba mpya hatupaswi kuwa na matumaini, kushangilia au hata kusikitika kwa uamuzi wowote utakaotolewa.

Hata hapa pamoja na facts zote usishangae historia ikijirudia.
 
Mimi ni mbumbu wa sheria hivyo naomba nieleweshwe hili kama kuna mtu anajua sheria. Mshtakiwa anapopelekwa mahakamani na kukataa kuwa maelezo aliyotoa hakutoa kwa hiari bali aliteswa, kwa nini mahakama isikubali moja kwa moja? I mean kama mwenye maelezo anayakana mwenyewe kwa nini anatiliwa shaka? Kwa nini zisitumike njia nyingine tu za kumtia hatiani? Najua ndivyo sheria ilivyo lakini kwangu mimi naona kuna ukakasi na kunatoa loophole kwa polisi kutumia njia ya mateso ili kupata maelezo kutoka kwa mshtakiwa. All in all, watuhumiwa wa kesi kama hii naweza kusema kwa uhakika kabisa ni IMPOSSIBLE kwa polisi wa Tanzania kuwakamata na kuwafikisha mahakamani bila kuwatesa.
Mwaka2004 nikiwa kijana mdogo na ndio mara yangu kwanza kuingia mahamani, Mzee mmoja alinifanyia kosa la kijinai na nikampeleka polisi akakiri kosa kwa kuandika maelezo yale ktk lile liboku la polisi bila kushutishwa na siku Ile alilala selo na baadae akapata dhamana baadae polisi walituita kama kufanya suluhu yaani anilipe fidia nikakubali lakn kwa sababu hakuwa na hela aliahidi baada miezi mitatu atanilipa, sijui alishauriwa na watu baada ya muda alinikana na polisi wakaniita kuwa kesi Ile wanaipeleka mahakamani nikweli baadae ikapagwa siku ya kuisikiliza, kwa sababu ilikuwa jinai Mimi nilikuwa shahidi namba moja, nilipojaribu kuomba maelezo aliyoyatoa polisi yazingatiwe aliyakana na mahakama ikayatupilia mbali, labda kwa sababu ni mahakama ya mwanzo, lakini tangu hapo siaminigi maelezo yanatolewa polisi kwamba yanaweza kusaidia, zaidi tuiache mahakama itende haki
 
Huo moto wa katiba unasubiri hadi kesi iishe? Isipoisha karibuni basi moto wa katiba nao haupo?? Upinzani wa TZ ni majanga matupu, ni ubatili na kujilisha upepo. Kesi itaisha na hakutakuwa na moto wa katiba wala bibi ya moto wa katiba, hakuna mpinzani mwenye guts za kuanzisha moto wowote hapa TZ, tuna wapinzani wa kuropoka na kupiga makelele nyuma ya keyboard!! Kama kulikuwa kuna jambo la wapinzani kuwasha huo moto unaosema basi ilibidi wauwashe mwenyekiti wao aachiwe, nini kimetokea?? Kwa sasa wanaogopa hata kuvaa Tshirt zao nyekundu mahakamani...
Mkuu ishu ya katiba mpya sio ishu ya upinzani hii ni ishu ya kitaifa.Mwakani katiba mpya itaanza Kaa ikijua Hilo,utake usitake mambo yko .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona objection ya upande wa utetezi ina nafasi kubwa ya kutoboa kwasababu;

1. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili yote yamethibitisha walikamatwa bila kufuata sheria ( PGO) hawakukamatwa bali walitekwa, na zaidi ilithibitika hata polisi wetu hawavijui vizuri vifungu vya kwenye PGO.

2. Polisi walishindwa kujitambulisha kwa watuhumiwa wao ni akina nani (hawakutoa vitambulisho), na watuhumiwa wana makosa gani.

3. Njia iliyotumika kuwakamata, waliwavizia, mmoja kutoka nyuma akamkaba mtuhumiwa na mwingine mbele, ikiwemo kuwafunika usoni na vitambaa (jacket na shuka) huu haukuwa ukamataji bali ni utekaji.

4. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza, alipokamatwa alipigwa na vishikizo vya mkanda kwenye suruali yake vikakatika na bahati nzuri hiyo suruali ndiyo aliivaa siku ya kutoa ushahidi akiwa ameishikiza kwa kamba.

5. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili kufanana kwamba polisi baada ya kumkamata mshtakiwa wa kwanza, walimuwekea madawa ya kulevya, na pistol, mshtakiwa wa pili akaona atoe vitu vyake mfukoni mapema ili kuepusha nae asijekuwekewa vitu kama mwenzake.

6. Haki za watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi zilikiukwa, kwanza polisi waliwabadilishia majina yao ya asili na kuwapa ya bandia, hili lilifanyika ili ndugu wa watuhumiwa wasijue ndugu zao wako kituo gani cha polisi, pili, kunyimwa chakula kwa siku kumi, na tatu, vipigo walivyopata wakiwa mikononi mwa polisi.

Hapa tunaona mshtakiwa wa kwanza alishindwa kutembea kutokana na kipigo akawa anaburuzwa na polisi, na mshtakiwa wa pili, yeye aliamua kuruka ruka ili apunguze maumivu ya kipigo kwa kuamini kwamba, kama angeendelea kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi ndio maumivu ya kipigo cha polisi yangezidi kwake.

- Vipigo, kauli za vitisho zilizotolewa na polisi kwa watuhumiwa, na kunyimwa chakula kwa siku kumi, vinatosha kuonesha kwamba watuhumiwa walitoa maelezo polisi wakiwa na hofu kwa ukatili waliofanyiwa na polisi/ wakiwa hawana afya njema ya akili kutokana na njaa, hivyo waliona bora watoe maelezo au wasaini maelezo waliyokuta yameshaandikwa tayari, ili kuokoa maisha yao.
Obviously based on prefessional integrity, adherence to ethics and moral values.
 
Wengi tunahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu .

Wengine tunafuatilia mitandaoni hatua kwa hatua mwenendo wa kesi nzima....

Kwa ambao hawajui au hawakumbuki au kusahau ni kuwa, kinachoendelea sasa ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within a trial)...

Kinachobishaniwa ni aidha maelezo ya mshitakiwa wa 1 Adamoo na wenzake waliyoyatoa polisi yapokelewe au yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka...

UPANDE WA MASHITAKA, unadai yapokelewe kwa sababu yalichukuliwa kwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa sheria na PGO na watuhumiwa kusaini wenyewe kwa hiari yao...

UPANDE WA UTETEZI NA WASHITAKIWA WENYEWE, unapinga yasipokelewe kwa sababu unadai maelezo hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria (chini ya shinikizo la mateso makubwa kwa watuhumiwa) kama njia ya kuwalazimisha kukubali na kusaini maelezo ambayo hawajui yameandikwa na nani...!!

Hii ndiyo sababu upande wa mashitaka waliwekewa "OBJECTION" na washitakiwa (utetezi) katika hili na kuzaa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na ndiyo inayosikilizwa sasa...

Ni katika hatua hii ya kesi hii ishu ya PGO imezuka kwa namna ya kipekee sana na watu kujua kumbe polisi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kipolisi wa kila siku ikiwemo kukamata na kuhoji watuhumiwa, kuwasafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine nk nk kwa mujibu wa PGO...!!

Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, maamuzi yoyote ya kesi hii ndogo ndiyo yàtakayotoa uelekeo wa kesi kubwa ambayo huko mbele tutamkuta kinara anayelengwa kuangamizwa au kufungwa (mshtakiwa namba 4, yaani Mh. Freeman A. Mbowe)...

MASWALI YA KUTUONGOZA KATIKA MJADALA HUU NI HAYA;

1. Je, mpaka hatua hii kwa wote mnaofuatilia kesi hii, na kwa mtazamo wa kila mmoja based on the evidence uliokwisha kutolewa, unadhani objection ya upande wa utetezi itatoboa....?

2. Kwa maelezo ya mshtakiwa namba 1 na 2 ambao pia ndiyo mashahidi wenyewe wa kesi hii ndogo, unadhani wameweza kuishawishi mahakama kuwa ni kweli waliteswa kama njia ya kuwalazimisha kukubali maelezo waliyoyatoa polisi chini ya kiapo cha "onyo?"...

3. Ili kuthibitisha kuwa mtu fulani aliteswa, ukiachilia mbali maelezo ya mdomo kuwa nilipigwa sana na kufanyiwa hivi au vile, ushahidi mkubwa huwa ni alama za makovu ya vidonda katika mwili...

Je, mashahidi walionesha alama zozote zinazoashiria tendo la kupigwa na kuteswa lilitendeka kweli....?

Alamsiki. Karibuni kwa mjadala...
Nashukuru kwa ufafanuzi naendelea kukifunza maana wote ni wahanga watatajiwa
 
Mwaka2004 nikiwa kijana mdogo na ndio mara yangu kwanza kuingia mahamani, Mzee mmoja alinifanyia kosa la kijinai na nikampeleka polisi akakiri kosa kwa kuandika maelezo yale ktk lile liboku la polisi bila kushutishwa na siku Ile alilala selo na baadae akapata dhamana baadae polisi walituita kama kufanya suluhu yaani anilipe fidia nikakubali lakn kwa sababu hakuwa na hela aliahidi baada miezi mitatu atanilipa, sijui alishauriwa na watu baada ya muda alinikana na polisi wakaniita kuwa kesi Ile wanaipeleka mahakamani nikweli baadae ikapagwa siku ya kuisikiliza, kwa sababu ilikuwa jinai Mimi nilikuwa shahidi namba moja, nilipojaribu kuomba maelezo aliyoyatoa polisi yazingatiwe aliyakana na mahakama ikayatupilia mbali, labda kwa sababu ni mahakama ya mwanzo, lakini tangu hapo siaminigi maelezo yanatolewa polisi kwamba yanaweza kusaidia, zaidi tuiache mahakama itende haki
Kumbe mahakama ya mwanzo? Ndiyo maana...

Duuuh, kwa hiyo ukawa umeshindwa kiaina namna hiyo...!

Pole...
 
Tukuulize wewe unaehudhuria mahakamani kama ulivyokwisha jinasibu.

Au kama wewe ni jaji basi toa hukumu tu usisumbue watu vichwa.

Ila kama kweli unahudhuria mahakamani rejea pale shahidi alipoonyesha makovu miguuni,mikononi na kichwani huku wakiomba asioneshe yaliyofichwa maungoni.

Asubuhi njema
Unataka kujaribu ku - achieve nini kwa comment yako hii...?

By the way hapa hakuna anayehukumu mtu...

Tunajaribu kutolea maoni ya kinachoendelea mahakamani...

Wewe kama kichwa kimelala, hulazimishwi kushiriki ktk mjadala huu...

Hata hivyo kwa kuwa umeandika, basi asante sana kwa mchango wako...
 
Wengi tunahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu .

Wengine tunafuatilia mitandaoni hatua kwa hatua mwenendo wa kesi nzima....

Kwa ambao hawajui au hawakumbuki au kusahau ni kuwa, kinachoendelea sasa ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within a trial)...

Kinachobishaniwa ni aidha maelezo ya mshitakiwa wa 1 Adamoo na wenzake waliyoyatoa polisi yapokelewe au yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka...

UPANDE WA MASHITAKA, unadai yapokelewe kwa sababu yalichukuliwa kwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa sheria na PGO na watuhumiwa kusaini wenyewe kwa hiari yao...

UPANDE WA UTETEZI NA WASHITAKIWA WENYEWE, unapinga yasipokelewe kwa sababu unadai maelezo hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria (chini ya shinikizo la mateso makubwa kwa watuhumiwa) kama njia ya kuwalazimisha kukubali na kusaini maelezo ambayo hawajui yameandikwa na nani...!!

Hii ndiyo sababu upande wa mashitaka waliwekewa "OBJECTION" na washitakiwa (utetezi) katika hili na kuzaa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na ndiyo inayosikilizwa sasa...

Ni katika hatua hii ya kesi hii ishu ya PGO imezuka kwa namna ya kipekee sana na watu kujua kumbe polisi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kipolisi wa kila siku ikiwemo kukamata na kuhoji watuhumiwa, kuwasafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine nk nk kwa mujibu wa PGO...!!

Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, maamuzi yoyote ya kesi hii ndogo ndiyo yàtakayotoa uelekeo wa kesi kubwa ambayo huko mbele tutamkuta kinara anayelengwa kuangamizwa au kufungwa (mshtakiwa namba 4, yaani Mh. Freeman A. Mbowe)...

MASWALI YA KUTUONGOZA KATIKA MJADALA HUU NI HAYA;

1. Je, mpaka hatua hii kwa wote mnaofuatilia kesi hii, na kwa mtazamo wa kila mmoja based on the evidence uliokwisha kutolewa, unadhani objection ya upande wa utetezi itatoboa....?

2. Kwa maelezo ya mshtakiwa namba 1 na 2 ambao pia ndiyo mashahidi wenyewe wa kesi hii ndogo, unadhani wameweza kuishawishi mahakama kuwa ni kweli waliteswa kama njia ya kuwalazimisha kukubali maelezo waliyoyatoa polisi chini ya kiapo cha "onyo?"...

3. Ili kuthibitisha kuwa mtu fulani aliteswa, ukiachilia mbali maelezo ya mdomo kuwa nilipigwa sana na kufanyiwa hivi au vile, ushahidi mkubwa huwa ni alama za makovu ya vidonda katika mwili...

Je, mashahidi walionesha alama zozote zinazoashiria tendo la kupigwa na kuteswa lilitendeka kweli....?

Alamsiki. Karibuni kwa mjadala...
Ni wazi kabisa kwamba mateso yalipelekea washitakiwa kusaini uongo wa Kingai , maelezo ya Adamoo kule kwa Kingi na Mahita yatatupiliwa mbali , kwa vile namna yalivyopatikana haikuwa halali
 
Wewe unadhan hapa JF wote ni vilaza hakuwa wanasheria, majaj na mahakim na ata wa ufaham wa sheria ambao kwa mujibu wa mtoa mada hawawez kuchangia chochote mpaka mahakam? Au wee ni Mahita nn? Au kingai?
Haha, mimi Kingai Mkuu..
1632963522961.jpeg
 
Kama kwei weee ndo kingai kweli wee Mungu alikuumba mida ya jion saa za uchovu.... Maana sura yako ngum jaman daaah. Sasa hiyo sura hiko hivyo je inakuwa vip ukinywa K.VANT???

Ata Kama binadam tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, mmmm wengine hawafanan nae
Mwanaume hasifiwi sura hahaha
 
Naona objection ya upande wa utetezi ina nafasi kubwa ya kutoboa kwasababu;

1. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili yote yamethibitisha walikamatwa bila kufuata sheria ( PGO) hawakukamatwa bali walitekwa, na zaidi ilithibitika hata polisi wetu hawavijui vizuri vifungu vya kwenye PGO.

2. Polisi walishindwa kujitambulisha kwa watuhumiwa wao ni akina nani (hawakutoa vitambulisho), na watuhumiwa wana makosa gani.

3. Njia iliyotumika kuwakamata, waliwavizia, mmoja kutoka nyuma akamkaba mtuhumiwa na mwingine mbele, ikiwemo kuwafunika usoni na vitambaa (jacket na shuka) huu haukuwa ukamataji bali ni utekaji.

4. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza, alipokamatwa alipigwa na vishikizo vya mkanda kwenye suruali yake vikakatika na bahati nzuri hiyo suruali ndiyo aliivaa siku ya kutoa ushahidi akiwa ameishikiza kwa kamba.

5. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili kufanana kwamba polisi baada ya kumkamata mshtakiwa wa kwanza, walimuwekea madawa ya kulevya, na pistol, mshtakiwa wa pili akaona atoe vitu vyake mfukoni mapema ili kuepusha nae asijekuwekewa vitu kama mwenzake.

6. Haki za watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi zilikiukwa, kwanza polisi waliwabadilishia majina yao ya asili na kuwapa ya bandia, hili lilifanyika ili ndugu wa watuhumiwa wasijue ndugu zao wako kituo gani cha polisi, pili, kunyimwa chakula kwa siku kumi, na tatu, vipigo walivyopata wakiwa mikononi mwa polisi.

Hapa tunaona mshtakiwa wa kwanza alishindwa kutembea kutokana na kipigo akawa anaburuzwa na polisi, na mshtakiwa wa pili, yeye aliamua kuruka ruka ili apunguze maumivu ya kipigo kwa kuamini kwamba, kama angeendelea kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi ndio maumivu ya kipigo cha polisi yangezidi kwake.

- Vipigo, kauli za vitisho zilizotolewa na polisi kwa watuhumiwa, na kunyimwa chakula kwa siku kumi, vinatosha kuonesha kwamba watuhumiwa walitoa maelezo polisi wakiwa na hofu kwa ukatili waliofanyiwa na polisi/ wakiwa hawana afya njema ya akili kutokana na njaa, hivyo waliona bora watoe maelezo au wasaini maelezo waliyokuta yameshaandikwa tayari, ili kuokoa maisha yao.
Ni uchambuzi mzuri, lakini je mahakama zetu zipo huru kuyaona haya? Mh rais alishasema Mbowe ni gaidi je mahakama zipo huru kutofautiana nae? Na haswa Ikichukuliwa cheo cha ujaji ni fadhila za rais? Huko nyuma mahakama zetu ziliwafunga kwa kuwaonea akina Mbowe, Sugu, Lema nk.
Muda utaamua tusiwe wapiga ramli.
 
Nitashangaa sana mahakama ikijivua nguo mbele ya umma wa watanzania na serikali ikijivua nguo mbele ya uso wa dunia (mabalozi wa nje wanaohudhuria kesi).

Hii dunia ya leo sio ile ya 1980's.

Ukiangalia mlolongo wa matukio kwenye hii kesi uliotolewa na watuhumiwa pamoja na mke wa mtuhumiwa Lin'gwenya leo, utaona wazi kuna unyama mwingi zaidi waliotendewa watuhumiwa zaidi hata ya kile kilichofikiriwa mwanzo.

Haki za washtakiwa, na haki za binadamu kwa ujumla wake vyote vilikiukwa wakati wa kuwakamata mpaka baada ya kuwakamata, polisi kukiepuka kikombe hiki hata kwa katiba hii tuliyonayo litakuwa ni ajabu la dunia.

Mkuu denooJ unayaona mambo ya kesi ya ngedere kala mahindi hakimu akiwa nyani.

Hukumu huwa, mlalamikaji (yaani binadamu) apewe mbolea zaidi ili azalishe mahindi kwa wingi kwa ajili ya kuwatosheleza kwa chakula nyani, ngedere na yeye pia "in that order not the other way round."

Bila mihimili huru hakuna kutoboa.
 
Back
Top Bottom