Kila jambo hatua.
Tuna options zipi zaidi ya kusubiria huruma za jaji?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila jambo hatua.
Options ziwe zinatambulika kisheria, kama kukata rufaa ni mojawapo, nje ya hapo hiyo experience kwa nchi yetu sijawahi kuiona.Tuna options zipi zaidi ya kusubiria huruma za jaji?
Options ziwe zinatambulika kisheria, kama kukata rufaa ni mojawapo, nje ya hapo hiyo experience kwa nchi yetu sijawahi kuiona.
Mkuu rejea case ya uhaini miaka ya 80s mashahidi wa serikali wakiwa kina Mabere Marando na kina Dr. Mahiga. Washitakiwa kina Hatty MacGhee, na kina Hans Poppe.
Kulikuwa na mawakili wa utetezi wazuri tu (first class) kama kina Murtaza Lakha na kina Muccaddam.
Ushahidi ulikuwa umepatikana kwa mateso kama hivi hivi. Ushahidi ulipokelewa na kutumika mahakamani dhidi ya watuhumiwa pamoja na mapingamizi kama hivi hivi.
Karibu Tanzania ambako bila katiba mpya mihimili mingine inawajibika kwa ule mmoja uliojichimbia zaidi.
Bila katiba mpya hatupaswi kuwa na matumaini, kushangilia au hata kusikitika kwa uamuzi wowote utakaotolewa.
Hata hapa pamoja na facts zote usishangae historia ikijirudia.
Mwaka2004 nikiwa kijana mdogo na ndio mara yangu kwanza kuingia mahamani, Mzee mmoja alinifanyia kosa la kijinai na nikampeleka polisi akakiri kosa kwa kuandika maelezo yale ktk lile liboku la polisi bila kushutishwa na siku Ile alilala selo na baadae akapata dhamana baadae polisi walituita kama kufanya suluhu yaani anilipe fidia nikakubali lakn kwa sababu hakuwa na hela aliahidi baada miezi mitatu atanilipa, sijui alishauriwa na watu baada ya muda alinikana na polisi wakaniita kuwa kesi Ile wanaipeleka mahakamani nikweli baadae ikapagwa siku ya kuisikiliza, kwa sababu ilikuwa jinai Mimi nilikuwa shahidi namba moja, nilipojaribu kuomba maelezo aliyoyatoa polisi yazingatiwe aliyakana na mahakama ikayatupilia mbali, labda kwa sababu ni mahakama ya mwanzo, lakini tangu hapo siaminigi maelezo yanatolewa polisi kwamba yanaweza kusaidia, zaidi tuiache mahakama itende hakiMimi ni mbumbu wa sheria hivyo naomba nieleweshwe hili kama kuna mtu anajua sheria. Mshtakiwa anapopelekwa mahakamani na kukataa kuwa maelezo aliyotoa hakutoa kwa hiari bali aliteswa, kwa nini mahakama isikubali moja kwa moja? I mean kama mwenye maelezo anayakana mwenyewe kwa nini anatiliwa shaka? Kwa nini zisitumike njia nyingine tu za kumtia hatiani? Najua ndivyo sheria ilivyo lakini kwangu mimi naona kuna ukakasi na kunatoa loophole kwa polisi kutumia njia ya mateso ili kupata maelezo kutoka kwa mshtakiwa. All in all, watuhumiwa wa kesi kama hii naweza kusema kwa uhakika kabisa ni IMPOSSIBLE kwa polisi wa Tanzania kuwakamata na kuwafikisha mahakamani bila kuwatesa.
Mkuu ishu ya katiba mpya sio ishu ya upinzani hii ni ishu ya kitaifa.Mwakani katiba mpya itaanza Kaa ikijua Hilo,utake usitake mambo yko .Huo moto wa katiba unasubiri hadi kesi iishe? Isipoisha karibuni basi moto wa katiba nao haupo?? Upinzani wa TZ ni majanga matupu, ni ubatili na kujilisha upepo. Kesi itaisha na hakutakuwa na moto wa katiba wala bibi ya moto wa katiba, hakuna mpinzani mwenye guts za kuanzisha moto wowote hapa TZ, tuna wapinzani wa kuropoka na kupiga makelele nyuma ya keyboard!! Kama kulikuwa kuna jambo la wapinzani kuwasha huo moto unaosema basi ilibidi wauwashe mwenyekiti wao aachiwe, nini kimetokea?? Kwa sasa wanaogopa hata kuvaa Tshirt zao nyekundu mahakamani...
Yatapokelewa yote. Fuatilieni kwa umakini si kiushabiki tuKwa upande wangu baada ya ufuatiliaji wa mwenendo mzima wa shauri hili dogo,Ninaona upande wa utetezi utatoboa.
Obviously based on prefessional integrity, adherence to ethics and moral values.Naona objection ya upande wa utetezi ina nafasi kubwa ya kutoboa kwasababu;
1. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili yote yamethibitisha walikamatwa bila kufuata sheria ( PGO) hawakukamatwa bali walitekwa, na zaidi ilithibitika hata polisi wetu hawavijui vizuri vifungu vya kwenye PGO.
2. Polisi walishindwa kujitambulisha kwa watuhumiwa wao ni akina nani (hawakutoa vitambulisho), na watuhumiwa wana makosa gani.
3. Njia iliyotumika kuwakamata, waliwavizia, mmoja kutoka nyuma akamkaba mtuhumiwa na mwingine mbele, ikiwemo kuwafunika usoni na vitambaa (jacket na shuka) huu haukuwa ukamataji bali ni utekaji.
4. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza, alipokamatwa alipigwa na vishikizo vya mkanda kwenye suruali yake vikakatika na bahati nzuri hiyo suruali ndiyo aliivaa siku ya kutoa ushahidi akiwa ameishikiza kwa kamba.
5. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili kufanana kwamba polisi baada ya kumkamata mshtakiwa wa kwanza, walimuwekea madawa ya kulevya, na pistol, mshtakiwa wa pili akaona atoe vitu vyake mfukoni mapema ili kuepusha nae asijekuwekewa vitu kama mwenzake.
6. Haki za watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi zilikiukwa, kwanza polisi waliwabadilishia majina yao ya asili na kuwapa ya bandia, hili lilifanyika ili ndugu wa watuhumiwa wasijue ndugu zao wako kituo gani cha polisi, pili, kunyimwa chakula kwa siku kumi, na tatu, vipigo walivyopata wakiwa mikononi mwa polisi.
Hapa tunaona mshtakiwa wa kwanza alishindwa kutembea kutokana na kipigo akawa anaburuzwa na polisi, na mshtakiwa wa pili, yeye aliamua kuruka ruka ili apunguze maumivu ya kipigo kwa kuamini kwamba, kama angeendelea kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi ndio maumivu ya kipigo cha polisi yangezidi kwake.
- Vipigo, kauli za vitisho zilizotolewa na polisi kwa watuhumiwa, na kunyimwa chakula kwa siku kumi, vinatosha kuonesha kwamba watuhumiwa walitoa maelezo polisi wakiwa na hofu kwa ukatili waliofanyiwa na polisi/ wakiwa hawana afya njema ya akili kutokana na njaa, hivyo waliona bora watoe maelezo au wasaini maelezo waliyokuta yameshaandikwa tayari, ili kuokoa maisha yao.
Nashukuru kwa ufafanuzi naendelea kukifunza maana wote ni wahanga watatajiwaWengi tunahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu .
Wengine tunafuatilia mitandaoni hatua kwa hatua mwenendo wa kesi nzima....
Kwa ambao hawajui au hawakumbuki au kusahau ni kuwa, kinachoendelea sasa ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within a trial)...
Kinachobishaniwa ni aidha maelezo ya mshitakiwa wa 1 Adamoo na wenzake waliyoyatoa polisi yapokelewe au yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka...
UPANDE WA MASHITAKA, unadai yapokelewe kwa sababu yalichukuliwa kwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa sheria na PGO na watuhumiwa kusaini wenyewe kwa hiari yao...
UPANDE WA UTETEZI NA WASHITAKIWA WENYEWE, unapinga yasipokelewe kwa sababu unadai maelezo hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria (chini ya shinikizo la mateso makubwa kwa watuhumiwa) kama njia ya kuwalazimisha kukubali na kusaini maelezo ambayo hawajui yameandikwa na nani...!!
Hii ndiyo sababu upande wa mashitaka waliwekewa "OBJECTION" na washitakiwa (utetezi) katika hili na kuzaa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na ndiyo inayosikilizwa sasa...
Ni katika hatua hii ya kesi hii ishu ya PGO imezuka kwa namna ya kipekee sana na watu kujua kumbe polisi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kipolisi wa kila siku ikiwemo kukamata na kuhoji watuhumiwa, kuwasafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine nk nk kwa mujibu wa PGO...!!
Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, maamuzi yoyote ya kesi hii ndogo ndiyo yàtakayotoa uelekeo wa kesi kubwa ambayo huko mbele tutamkuta kinara anayelengwa kuangamizwa au kufungwa (mshtakiwa namba 4, yaani Mh. Freeman A. Mbowe)...
MASWALI YA KUTUONGOZA KATIKA MJADALA HUU NI HAYA;
1. Je, mpaka hatua hii kwa wote mnaofuatilia kesi hii, na kwa mtazamo wa kila mmoja based on the evidence uliokwisha kutolewa, unadhani objection ya upande wa utetezi itatoboa....?
2. Kwa maelezo ya mshtakiwa namba 1 na 2 ambao pia ndiyo mashahidi wenyewe wa kesi hii ndogo, unadhani wameweza kuishawishi mahakama kuwa ni kweli waliteswa kama njia ya kuwalazimisha kukubali maelezo waliyoyatoa polisi chini ya kiapo cha "onyo?"...
3. Ili kuthibitisha kuwa mtu fulani aliteswa, ukiachilia mbali maelezo ya mdomo kuwa nilipigwa sana na kufanyiwa hivi au vile, ushahidi mkubwa huwa ni alama za makovu ya vidonda katika mwili...
Je, mashahidi walionesha alama zozote zinazoashiria tendo la kupigwa na kuteswa lilitendeka kweli....?
Alamsiki. Karibuni kwa mjadala...
Kumbe mahakama ya mwanzo? Ndiyo maana...Mwaka2004 nikiwa kijana mdogo na ndio mara yangu kwanza kuingia mahamani, Mzee mmoja alinifanyia kosa la kijinai na nikampeleka polisi akakiri kosa kwa kuandika maelezo yale ktk lile liboku la polisi bila kushutishwa na siku Ile alilala selo na baadae akapata dhamana baadae polisi walituita kama kufanya suluhu yaani anilipe fidia nikakubali lakn kwa sababu hakuwa na hela aliahidi baada miezi mitatu atanilipa, sijui alishauriwa na watu baada ya muda alinikana na polisi wakaniita kuwa kesi Ile wanaipeleka mahakamani nikweli baadae ikapagwa siku ya kuisikiliza, kwa sababu ilikuwa jinai Mimi nilikuwa shahidi namba moja, nilipojaribu kuomba maelezo aliyoyatoa polisi yazingatiwe aliyakana na mahakama ikayatupilia mbali, labda kwa sababu ni mahakama ya mwanzo, lakini tangu hapo siaminigi maelezo yanatolewa polisi kwamba yanaweza kusaidia, zaidi tuiache mahakama itende haki
Unataka kujaribu ku - achieve nini kwa comment yako hii...?Tukuulize wewe unaehudhuria mahakamani kama ulivyokwisha jinasibu.
Au kama wewe ni jaji basi toa hukumu tu usisumbue watu vichwa.
Ila kama kweli unahudhuria mahakamani rejea pale shahidi alipoonyesha makovu miguuni,mikononi na kichwani huku wakiomba asioneshe yaliyofichwa maungoni.
Asubuhi njema
Ni wazi kabisa kwamba mateso yalipelekea washitakiwa kusaini uongo wa Kingai , maelezo ya Adamoo kule kwa Kingi na Mahita yatatupiliwa mbali , kwa vile namna yalivyopatikana haikuwa halaliWengi tunahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu .
Wengine tunafuatilia mitandaoni hatua kwa hatua mwenendo wa kesi nzima....
Kwa ambao hawajui au hawakumbuki au kusahau ni kuwa, kinachoendelea sasa ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within a trial)...
Kinachobishaniwa ni aidha maelezo ya mshitakiwa wa 1 Adamoo na wenzake waliyoyatoa polisi yapokelewe au yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka...
UPANDE WA MASHITAKA, unadai yapokelewe kwa sababu yalichukuliwa kwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa sheria na PGO na watuhumiwa kusaini wenyewe kwa hiari yao...
UPANDE WA UTETEZI NA WASHITAKIWA WENYEWE, unapinga yasipokelewe kwa sababu unadai maelezo hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria (chini ya shinikizo la mateso makubwa kwa watuhumiwa) kama njia ya kuwalazimisha kukubali na kusaini maelezo ambayo hawajui yameandikwa na nani...!!
Hii ndiyo sababu upande wa mashitaka waliwekewa "OBJECTION" na washitakiwa (utetezi) katika hili na kuzaa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na ndiyo inayosikilizwa sasa...
Ni katika hatua hii ya kesi hii ishu ya PGO imezuka kwa namna ya kipekee sana na watu kujua kumbe polisi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kipolisi wa kila siku ikiwemo kukamata na kuhoji watuhumiwa, kuwasafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine nk nk kwa mujibu wa PGO...!!
Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, maamuzi yoyote ya kesi hii ndogo ndiyo yàtakayotoa uelekeo wa kesi kubwa ambayo huko mbele tutamkuta kinara anayelengwa kuangamizwa au kufungwa (mshtakiwa namba 4, yaani Mh. Freeman A. Mbowe)...
MASWALI YA KUTUONGOZA KATIKA MJADALA HUU NI HAYA;
1. Je, mpaka hatua hii kwa wote mnaofuatilia kesi hii, na kwa mtazamo wa kila mmoja based on the evidence uliokwisha kutolewa, unadhani objection ya upande wa utetezi itatoboa....?
2. Kwa maelezo ya mshtakiwa namba 1 na 2 ambao pia ndiyo mashahidi wenyewe wa kesi hii ndogo, unadhani wameweza kuishawishi mahakama kuwa ni kweli waliteswa kama njia ya kuwalazimisha kukubali maelezo waliyoyatoa polisi chini ya kiapo cha "onyo?"...
3. Ili kuthibitisha kuwa mtu fulani aliteswa, ukiachilia mbali maelezo ya mdomo kuwa nilipigwa sana na kufanyiwa hivi au vile, ushahidi mkubwa huwa ni alama za makovu ya vidonda katika mwili...
Je, mashahidi walionesha alama zozote zinazoashiria tendo la kupigwa na kuteswa lilitendeka kweli....?
Alamsiki. Karibuni kwa mjadala...
Haha, mimi Kingai Mkuu..Wewe unadhan hapa JF wote ni vilaza hakuwa wanasheria, majaj na mahakim na ata wa ufaham wa sheria ambao kwa mujibu wa mtoa mada hawawez kuchangia chochote mpaka mahakam? Au wee ni Mahita nn? Au kingai?
Haha, mimi Kingai Mkuu..
View attachment 1957855
Mwanaume hasifiwi sura hahahaKama kwei weee ndo kingai kweli wee Mungu alikuumba mida ya jion saa za uchovu.... Maana sura yako ngum jaman daaah. Sasa hiyo sura hiko hivyo je inakuwa vip ukinywa K.VANT???
Ata Kama binadam tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, mmmm wengine hawafanan nae
Ni uchambuzi mzuri, lakini je mahakama zetu zipo huru kuyaona haya? Mh rais alishasema Mbowe ni gaidi je mahakama zipo huru kutofautiana nae? Na haswa Ikichukuliwa cheo cha ujaji ni fadhila za rais? Huko nyuma mahakama zetu ziliwafunga kwa kuwaonea akina Mbowe, Sugu, Lema nk.Naona objection ya upande wa utetezi ina nafasi kubwa ya kutoboa kwasababu;
1. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili yote yamethibitisha walikamatwa bila kufuata sheria ( PGO) hawakukamatwa bali walitekwa, na zaidi ilithibitika hata polisi wetu hawavijui vizuri vifungu vya kwenye PGO.
2. Polisi walishindwa kujitambulisha kwa watuhumiwa wao ni akina nani (hawakutoa vitambulisho), na watuhumiwa wana makosa gani.
3. Njia iliyotumika kuwakamata, waliwavizia, mmoja kutoka nyuma akamkaba mtuhumiwa na mwingine mbele, ikiwemo kuwafunika usoni na vitambaa (jacket na shuka) huu haukuwa ukamataji bali ni utekaji.
4. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza, alipokamatwa alipigwa na vishikizo vya mkanda kwenye suruali yake vikakatika na bahati nzuri hiyo suruali ndiyo aliivaa siku ya kutoa ushahidi akiwa ameishikiza kwa kamba.
5. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili kufanana kwamba polisi baada ya kumkamata mshtakiwa wa kwanza, walimuwekea madawa ya kulevya, na pistol, mshtakiwa wa pili akaona atoe vitu vyake mfukoni mapema ili kuepusha nae asijekuwekewa vitu kama mwenzake.
6. Haki za watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi zilikiukwa, kwanza polisi waliwabadilishia majina yao ya asili na kuwapa ya bandia, hili lilifanyika ili ndugu wa watuhumiwa wasijue ndugu zao wako kituo gani cha polisi, pili, kunyimwa chakula kwa siku kumi, na tatu, vipigo walivyopata wakiwa mikononi mwa polisi.
Hapa tunaona mshtakiwa wa kwanza alishindwa kutembea kutokana na kipigo akawa anaburuzwa na polisi, na mshtakiwa wa pili, yeye aliamua kuruka ruka ili apunguze maumivu ya kipigo kwa kuamini kwamba, kama angeendelea kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi ndio maumivu ya kipigo cha polisi yangezidi kwake.
- Vipigo, kauli za vitisho zilizotolewa na polisi kwa watuhumiwa, na kunyimwa chakula kwa siku kumi, vinatosha kuonesha kwamba watuhumiwa walitoa maelezo polisi wakiwa na hofu kwa ukatili waliofanyiwa na polisi/ wakiwa hawana afya njema ya akili kutokana na njaa, hivyo waliona bora watoe maelezo au wasaini maelezo waliyokuta yameshaandikwa tayari, ili kuokoa maisha yao.
Nitashangaa sana mahakama ikijivua nguo mbele ya umma wa watanzania na serikali ikijivua nguo mbele ya uso wa dunia (mabalozi wa nje wanaohudhuria kesi).
Hii dunia ya leo sio ile ya 1980's.
Ukiangalia mlolongo wa matukio kwenye hii kesi uliotolewa na watuhumiwa pamoja na mke wa mtuhumiwa Lin'gwenya leo, utaona wazi kuna unyama mwingi zaidi waliotendewa watuhumiwa zaidi hata ya kile kilichofikiriwa mwanzo.
Haki za washtakiwa, na haki za binadamu kwa ujumla wake vyote vilikiukwa wakati wa kuwakamata mpaka baada ya kuwakamata, polisi kukiepuka kikombe hiki hata kwa katiba hii tuliyonayo litakuwa ni ajabu la dunia.