Kumbe Abushiri wa Tanga aliyepigana na wajerumani na kunyongwa hakuwa na maana yoyote

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Shuleni tulifundishwa habari ya Abushiri wa Tanga kupigana na wakoloni wa kijerumani. Alitajwa kama shujaa mpigania uhuru kumbe hamna lolote. Kumbe jamaa alikuwa anamiliki mashamba makubwa na watumwa. Kifupi alikuwa anapigania nafasi ya kuendelea kukandamiza wengine. Hakuwa na maana kabisa.

1685787369466.png
 
Kimsingi historia tunayosoma kwa 90%ni watawala au watu waliokuwa na umaarufu mkubwa sana na Wala sio watu wema
Miaka 200 ijayo historia itawataja Nyerere,Mwinyi ,Mkapa ,Kikwete ,Magufuli na Samia Hawa wengine tena hata mawaziri hawatatajwa je watu hao ni wema kwa watu wote!?historia itaangaliwa kwa namna yake wakati huo.
Watawala wa kiafrika hawakuwa wema sana ila hawakuwa na ukatili kama ule wa wageni maana wageni wao walikuwa wamejifunza hadi mbinu za ukatili kama kunyonga kupiga mijeledi na mateso mengine ambazo mbinu hizo waliambukiza kwa waafrika
 
Kila mmoja alipigania kulinda nafasi yake!Viongozi wengi walihofia kupoteza nafasi zao.Na ndivyo ilivyotokea baada ya kushindwa.Hakuna Uzalendo wote wote.Wengi wamehusika Sana kuuza ndugu zao(slave trade)
 
Achana na huyo mpigania Uhuru, soma historia ya Chief Mangungo aliyeonekana ameingia Mkataba wa Kitapeli na Carl Peters kutokana na Kukosa Elimu na Exposure.

Siku hizi Watawala wetu wamesoma hadi Elimu za Masters au PhD lakini Mikataba wanayosainishana ni zaidi ya ile ya Chifu Mangungo 🙌
 
Bushiri, Mkwawa, Mirambo wote walikuwa watemi na walikuwa wakifanya biashara na waarabu ya kuuza watumwa na pembe za ndovu, dhahabu n.k

Hata watawala maarufu wa Afrika Magharibi kama akina Mansa Musa walikuwa wakiuza watumwa kwa Waarabu na wazungu

Ila haya yanafichwa
 
Kimsingi historia tunayosoma kwa 90%ni watawala au watu waliokuwa na umaarufu mkubwa sana na Wala sio watu wema
Miaka 200 ijayo historia itawataja Nyerere,Mwinyi ,Mkapa ,Kikwete ,Magufuli na Samia Hawa wengine tena hata mawaziri hawatatajwa je watu hao ni wema kwa watu wote!?historia itaangaliwa kwa namna yake wakati huo.
Watawala wa kiafrika hawakuwa wema sana ila hawakuwa na ukatili kama ule wa wageni maana wageni wao walikuwa wamejifunza hadi mbinu za ukatili kama kunyonga kupiga mijeledi na mateso mengine ambazo mbinu hizo waliambukiza kwa waafrika
Watawala wa kiafrika walikuwa makatili kama tu wale wa kizungu.
 
Achana na huyo mpigania Uhuru, soma historia ya Chief Mangungo aliyeonekana ameingia Mkataba wa Kitapeli na Carl Peters kutokana na Kukosa Elimu na Exposure.

Siku hizi Watawala wetu wamesoma hadi Elimu za Masters au PhD lakini Mikataba wanayosainishana ni zaidi ya ile ya Chifu Mangungo 🙌
Kwanza ukute Mangungo alikuwa na nia njema kabisa na nchi yake. Pengine aliona nafasi ya kuilinda dhidi ya wahehe, maana wahehe wakati huo walikuwa wanazingua sana.
 
Hakika Mkuu, naamini Chifu Mangungo angekuwa amepiga shule angekuwa Mtawala mzuri kuliko tulionao miaka ya hivi karibuni

Umewahi kukisoma Kitabu kinaitwa Black Shadow?

Kilifutwa baada ya Watawala kuto kukipenda vile kimewazungumzia
 
Bushiri, Mkwawa, Mirambo wote walikuwa watemi na walikuwa wakifanya biashara na waarabu ya kuuza watumwa na pembe za ndovu, dhahabu n.k

Hata watawala maarufu wa Afrika Magharibi kama akina Mansa Musa walikuwa wakiuza watumwa kwa Waarabu na wazungu

Ila haya yanafichwa
Ni kweli. Japo kwa Mirambo ilikuwa tofauti kidogo, alikuwa anapigana na waarabu waliotawala Tabora. Alifunga njia ya Ujiji. Alikuwa tu anapigania nafasi ya kutawala na kupiga ushuru kwa waenda Ujiji. Lakini alikuwa na afadhali kidogo.
 
Bushiri, Mkwawa, Mirambo wote walikuwa watemi na walikuwa wakifanya biashara na waarabu ya kuuza watumwa na pembe za ndovu, dhahabu n.k

Hata watawala maarufu wa Afrika Magharibi kama akina Mansa Musa walikuwa wakiuza watumwa kwa Waarabu na wazungu

Ila haya yanafichwa
Wakati huo wa Barter Trade au fedha ilikuwa imeshagundulika?
 
Achana na huyo mpigania Uhuru, soma historia ya Chief Mangungo aliyeonekana ameingia Mkataba wa Kitapeli na Carl Peters kutokana na Kukosa Elimu na Exposure.

Siku hizi Watawala wetu wamesoma hadi Elimu za Masters au PhD lakini Mikataba wanayosainishana ni zaidi ya ile ya Chifu Mangungo [emoji119]
Mikataba inasainiwa ikulu haraka haraka haipiti bungeni kufanyiwa analysis ,unategemea nini
 
Wakati huo nguo ndiyo zilitumika hasa kama pesa. Vingine vilivyotumika sana kama pesa vilikuwa shanga, bunduki na unga wa risasi.
Okay, kumbe ilikuwa ni biashara ya kubadirishana vitu kwa vitu 🙌

Ila still walipiga Utajiri Mkubwa hadi kufanya kutengeneza kwa Koo maarufu miaka ile.
 
Back
Top Bottom