Kwanza ufahamu mkuu Utumwa ulikua ni Mfumo kama mifumo mingine Ubepari, Jamaa Feudal etc.
Utumwa ulifanywa na watu wote Na kulikua na njia maalum za kuwapata.
Zamani Hakukua na Jela prisoners of wars waliuzwa kama watumwa, wenye madeni sugu waliuzwa etc, na ulikua pia unaweza nunua Uhuru wako, Pia watumwa hawakuwa treated vibaya kama historia inavyopotoshwa, watumwa wengi hasa toka Africa walitumika kama war Mercenaries na walipata vyeo vikubwa tu.
So ulikua ni Mfumo wa maisha kama mifumo mingine kulikua na watu weusi wanamiliki watumwa wa kiarabu, warabu wenye watumwa wazungu etc.
Historia ya Utumwa ilikuja Kubadilika baada ya Kugunduliwa America na kuwa target watu weusi hapo ndio ilikua kamata Kamata na watu kuonewa.
Kwa akili zetu fupi unatumia time line ya sasa kuwa Judge ila kwa wakati wao walikua ni Mashujaa na waliwatendea haki wanaowaongoza kwa kupigana hadi kufa,
Watawala wa Ki Zamani walikua makatili kwa Makabila ya Nje ila makabila yao walikua mstari wa Mbele kuyapigania.
Unafikiria Mkwawa, Bushiri, Kinjikitile na wengine walishindwa kuchukua 10% toka kwa Wakoloni na kuuza Makabila yao? Waliweza kufanya hivyo ila wakaamua bora kufa kuliko kusaliti watu wao. Kitu hichi hukipati popote sasa hivi nchi hii.