Wadiz,
Ukifika Mkwawa Museum Kalenga utakuta historia ya urafiki kati ya Abushiri na Mtwa Mkwawa.
Utakuta bunduki ambayo Abushiri alimpa Mkwawa na ndiyo bunduki iliyomsaidia Mkwawa kuanza kutengeneza bunduki nyingine yeye mwenyewe.
Hii ndiyo bunduki Mkwawa aliitumia katika vita vya Wahehe na Wajerumani.
Mkwawa na Abushiri walifanya biashara pamoja.
Abushiri ndiye aliyemsilimisha Mtwa Mkwawa akawa Muislam na Mkwawa akachagua jina la Abdallah.
Abushiri hakuishia hapo alimfundisha Mkwawa kusoma na kuandikwa kwa hati za Kiarabu hadi akajua.
Barua za Mkwawa zipo hapo Mkwawa Museum.
Baada ya kusilimu Mkwawa akawa hampi mtu uongozi katika himaya yake hadi kwanza amekuwa Muislam.
Inategemea unaitazamaje historia ya Abushiri na umeisoma kutoka vyanzo gani?
Je ni kweli Abushiri alikuwa anafanya biashara ya utumwa?
Je kuna ushahidi wowote kuwa Abushiri alifanya biashara hii na Mkwawa?
Ngome ya Mkwawa ilishambuliwa kwa kupigwa mizinga kutoka upande wa Tosamaganga na leo hapo limejengwa kanisa kubwa na maarufu.
Hakuna uwezekano kuwa hii ni kumbukumbu kwa kuanguka kwa Mtwa Abdallah Mkwawa?
Kuwa wanahistoria wanaotafsiri hili kama moja ya kusafisha njia ya kuingiza ukoloni kwani wamishionari walifuatiwa nyuma na wakoloni.
Lakini kuna wanahistoria wanatazama athari ya kusilimu kwa Mkwawa na matokeoa yake.
Je Uislam ulienea baada ya kifo cha Mkwawa au ulishindwa kukua?
Manispaa ya Iringa ina misikiti 25 yote inasaliwa Sala ya Ijumaa na mkoa mzima una misikiti 80.
Baadhi ya wanahistoria wanajiuliza nini ilikuwa athar ya kusilimu kwa Chief Mkwawa?
Ingekuwaje kama Mkwawa angekufa mpagani?
Laiti Abushiri angekuwa ''dubwana la hovyo'' (ovyo) asingeweza kuwa na usuhuba na Mtwa Mkwawa kiasi cha kumtia katika Uislam na kumfunza kusoma na kuandika.
Wazalendo hawa wawili wote wameacha historia kubwa ya vita vyao na Wajerumani.