Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Utumwa ulikuwa ukatiliKitabu gani mkuu? Na Hio website wala haisemi wamekua treated vizuri tu, bali inaelezea vitu ambavyo vina Make sense.
Mfano kwenye Mashamba walipewa eneo la kujikimu, siku kadhaa analima shamba la master na siku kadhaa analima shamba lake na anaweza akauza mazao yake kupata hela ya matumizi yake. Still ni mfumo wa kinyonyaji ila Binadamu anaweza vumilia.
Tofauti na chumvi ambazo zinaongeawa as if hao Watumwa walikua ni ma robot.
Umeshawah kujiuliza Kwa nn hao wazalendo wako hawakupigana na mwarabu Bali walipigana na mjeruman ,.... ?? Hao jamaa walihusika kwenye biashara ya utumwa Kwa kumuuzia mateka mwarabu , walikuwa wanavamia himaya zingine Kwa nguvu , pindi wanaposhinda waliwachukua mateka na kuwauza Kwa waarabu ... Tatizo lilikuja mjeruman hakutaka hzo mambo , yeye alitaka resources wao wakaona wanapoteza umiliki wakaamua kuingia front , walichofanywa wanajua wenyewe ......Wadiz,
Ukifika Mkwawa Museum Kalenga utakuta historia ya urafiki kati ya Abushiri na Mtwa Mkwawa.
Utakuta bunduki ambayo Abushiri alimpa Mkwawa na ndiyo bunduki iliyomsaidia Mkwawa kuanza kutengeneza bunduki nyingine yeye mwenyewe.
Hii ndiyo bunduki Mkwawa aliitumia katika vita vya Wahehe na Wajerumani.
Mkwawa na Abushiri walifanya biashara pamoja.
Abushiri ndiye aliyemsilimisha Mtwa Mkwawa akawa Muislam na Mkwawa akachagua jina la Abdallah.
Abushiri hakuishia hapo alimfundisha Mkwawa kusoma na kuandikwa kwa hati za Kiarabu hadi akajua.
Barua za Mkwawa zipo hapo Mkwawa Museum.
Baada ya kusilimu Mkwawa akawa hampi mtu uongozi katika himaya yake hadi kwanza amekuwa Muislam.
Inategemea unaitazamaje historia ya Abushiri na umeisoma kutoka vyanzo gani?
Je ni kweli Abushiri alikuwa anafanya biashara ya utumwa?
Je kuna ushahidi wowote kuwa Abushiri alifanya biashara hii na Mkwawa?
Ngome ya Mkwawa ilishambuliwa kwa kupigwa mizinga kutoka upande wa Tosamaganga na leo hapo limejengwa kanisa kubwa na maarufu.
Hakuna uwezekano kuwa hii ni kumbukumbu kwa kuanguka kwa Mtwa Abdallah Mkwawa?
Kuwa wanahistoria wanaotafsiri hili kama moja ya kusafisha njia ya kuingiza ukoloni kwani wamishionari walifuatiwa nyuma na wakoloni.
Lakini kuna wanahistoria wanatazama athari ya kusilimu kwa Mkwawa na matokeoa yake.
Je Uislam ulienea baada ya kifo cha Mkwawa au ulishindwa kukua?
Manispaa ya Iringa ina misikiti 25 yote inasaliwa Sala ya Ijumaa na mkoa mzima una misikiti 80.
Baadhi ya wanahistoria wanajiuliza nini ilikuwa athar ya kusilimu kwa Chief Mkwawa?
Ingekuwaje kama Mkwawa angekufa mpagani?
Laiti Abushiri angekuwa ''dubwana la hovyo'' (ovyo) asingeweza kuwa na usuhuba na Mtwa Mkwawa kiasi cha kumtia katika Uislam na kumfunza kusoma na kuandika.
Wazalendo hawa wawili wote wameacha historia kubwa ya vita vyao na Wajerumani.
Kabla ya Kuja Mjerumani alikuja Mreno, Mreno alinunua Watumwa ila pia walipigana na makabila ya Tanzania kwa nini?Umeshawah kujiuliza Kwa nn hao wazalendo wako hawakupigana na mwarabu Bali walipigana na mjeruman ,.... ?? Hao jamaa walihusika kwenye biashara ya utumwa Kwa kumuuzia mateka mwarabu , walikuwa wanavamia himaya zingine Kwa nguvu , pindi wanaposhinda waliwachukua mateka na kuwauza Kwa waarabu ... Tatizo lilikuja mjeruman hakutaka hzo mambo , yeye alitaka resources wao wakaona wanapoteza umiliki wakaamua kuingia front , walichofanywa wanajua wenyewe ......
NGOJA WAJE....Shuleni tulifundishwa habari ya Abushiri wa Tanga kupigana na wakoloni wa kijerumani. Alitajwa kama shujaa mpigania uhuru kumbe hamna lolote. Kumbe jamaa alikuwa anamiliki mashamba makubwa na watumwa. Kifupi alikuwa anapigania nafasi ya kuendelea kukandamiza wengine. Hakuwa na maana kabisa.
View attachment 2644629
Historia ya Tanzania/Tanganyika/Zanzibar ila kabla ya mwaka 1900Baba...
Nifahamishe ''issues'' unazotaka kuzijua.
Ikiwa najua vitabu nitakuelekeza na pia naweza hata mimi nikakueleza baadhi ya mambo katika hizo ''issues.''
Halikadhalika kuna elimu kubwa sana mitandaoni unaweza kufanya ''search.''
Zous,
Huyu uliyemtaja jina lake ni Abdulraufu Songea Mbano lakini wanahistoria wamefuta jina la ''Abdulraufu'' wanamwita Songea Mbano.
Kaburi lake lipo peke yake Mahenge Songea kwenye makumbusho ya Vita Vya Maji Maji pembeni ya kaburi la halaiki ambalo majemadari wenzake wa vita hivyo wamezikwa.
Kuna historia ya kusikitisha sana ya kunyongwa kwao.
Majemadari hawa walikuwa Waislam na hukumu ya kuuliwa kwao ilipopitishwa na Wajerumani alikuja mmeshionari kutoka Peramiho akawaambia kuwa ikiwa watakubali kubatizwa hawatanyongwa.
Hii ilikuwa ghilba waliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo kisha wakawanyonga.
Orodha ya majina yao ipo hapo Mahenge kwenye mnara wa kumbukumbu.
Katika hawa majemadari kuna mwanamke pekee aliyenyongwa huyu wanamwita kwa jina moja ''Mkomanile'' lakini jina lake la Khadija Mkomanile.
Wanahistoria wamefuta jina lake la Khadija.
View attachment 2645371
Majemadari walionyongwa wa kwanza kulia waliosimama n Abdulraufu Songea Mbano
View attachment 2645373
Nduna Abdulraufu Songea Mbano
Baba...Historia ya Tanzania/Tanganyika/Zanzibar ila kabla ya mwaka 1900
Zous,Shukran mkuu kwa kuniongezea jambo.kuna maneno yaliandikwa kwenye Hilo kaburi la majemedari.nimeyasahau ila yalikua yanahamasisha xnaa uzalendo
Sasa utajuaje kwa nini walikuwa wanapigania uhuru?Hizi historia zingefutwa tu hazina maana yeyote katika maisha. Tuanzie enzi za Nyerere na Uhuru mpaka udikteta wa kina Magufuli
Mpaka sasa hivi hili linaendelea. Hamuoni watu wanavyoporwa ardhi na kupewa wageni? Hii ndiyo ilifanya Afrika iwe rahisi kuchukuwa watumwa.Watawala wa kiafrika walikuwa makatili kama tu wale wa kizungu.
Mkuu hiki kitabu naweza PATA nakala durufu(photocopy) yake kama unacho?Hakika Mkuu, naamini Chifu Mangungo angekuwa amepiga shule angekuwa Mtawala mzuri kuliko tulionao miaka ya hivi karibuni
Umewahi kukisoma Kitabu kinaitwa Black Shadow?
Kilifutwa baada ya Watawala kuto kukipenda vile kimewazungumzia
Hiki kitabu kilizuiwa kutumika na Serikali, bahati nzuri ninacho kwenye library yangu ya Kijijini huko.Mkuu hiki kitabu naweza PATA nakala durufu(photocopy) yake kama unacho?