Kumbe BongoFleva inalipa!! Diamond Platnumz anaingiza Milioni 200 kwa mwezi kwa matangazo tu

Kumbe BongoFleva inalipa!! Diamond Platnumz anaingiza Milioni 200 kwa mwezi kwa matangazo tu

Watu walioko nyuma ya billgate wanamuangalia kama boss wakati diamond hao watu ye ndio maboss zake. Hiyo inamaanisha kwamba swala la mgao linategemeana na mode ya boss siku hiyo boss kaamkaje

Hili tumeliona kwa wengi wadananda hasa hawa wabongo fleva wazee wa kufake, eti ooh sijui "msanii hautakiwi kuonekana sana utapoteza brand"

brand au brandina? Mbona kina mawenge, dizasta tunaishi nao street kiaina

Kunawasaidia nini kufake maisha mseme mnapesa mingi wakati waleti inabisha? Sasa hao mamluki wake almost karibia wote wameshindwa kumudu kodi ya nyumba...ni aibu
nimegundua wewe ni mtu wa aina gani, wivu tu na majungu.
 
Juzi kasema ukipata view one million YouTube bas unapata around 900K up to 1000K , video ya waah ina view 37Mil , IT wao karopoka imeingiza 90 Mil mpak sasa , jamaa wamekaa kiongo ongo sana
jambo ambalo hujui zile clip video zote za dance zikicount views hela inaenda kwa mond
 
nimegundua wewe ni mtu wa aina gani, wivu tu na majungu.
Kipandacho hushuka ulishawaza?, si miujiza ni asili inawashangaza

Wasahaulifu walimwengu ilitangazwa, Watajatwa mashujaa na jina lake halita tajwa

wanafki walafi na mabishoo zake, wangapi watakuwepo kiu ikidaka koo lake?

Muda wa kuwasoma wote waliopo kando yake, maana hata pesa haitatibu jeraha la roho yake
 
Huyu mr nice acha tu [emoji23][emoji23][emoji23]
Umenikumbusha mbali sana!
Naskia yuko kenya huko sasa

Ova
Mr Nice alikuwaga anamwaga sana makreti ya bia plus wapambe kibao , kuzungusha round bar hadi kero sijui ana hali gani sasa hivi

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mr Nice alikuwaga anamwaga sana makreti ya bia plus wapambe kibao , kuzungusha round bar hadi kero sijui ana hali gani sasa hivi

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
Badaye akawa anakunywa kulipa utata
Bar kibao vimeo...kudaiwa mpk kudhalilishwa
Hela alipata ila hamfiki huyu wa sasa lkn
Angeweza ku manage fedha zake vzr angeishi
Maisha bila wasi ...

Ova
 
Mr nice kumfananisha na Diamond ni kukosa ufahamu hakuna msanii aliyewai fikia Peak ya juu kabisa kama ya Diamond sio kwa Tz hiyo ni EA.
Ni kweli,ila huyo nice kwa wakati naye hela aliyopata si haba angetulia asingeshuka hivi
Kifedha...diamond kusema ukweli anaweza kuwa msanii wa tz aliyetengeneza pesa sana mpka ku manage pesa zake yaani anakaza

Ova
 
Hivi ubora wa kitu unatokana na anayetangaza kitu au material iliyotengeneza kitu!
 
We mjinga sana ni Kwakuwa unakaa Tanzania tu! Hakuna mtu kafika peak kama Chameleon
Mr nice kumfananisha na Diamond ni kukosa ufahamu hakuna msanii aliyewai fikia Peak ya juu kabisa kama ya Diamond sio kwa Tz hiyo ni EA.
 
No, amejenga kwenye kiwanja cha mama'ake Madale. Mama yuko na Ben10, yeye na Zari, dada zake na vijamaa vyao humo humo, akaona isiwe tabu, akaenda kupanga....eti kanunua hoteli lakini anapanga, eti anaingiza 500m kwa mwezi, upuuzi tu

Alijenga pagala akafanyiwa finishing na zari Madale, nyumba anazo uswahilini za uwezo wake millioni 30 Mpaka 50 amenunua kule kunduchi kwenye mashimo ya kuchimba kokoto na yeye Anajiona ni wa hadhi ya kukaa kwenye mansion ndio maana anapanga
 
Nyumba anayoishi pale Mbezi si ya kwake, nalifahamu hili kutokana na asili ya kazi yangu nina access ya kujua wamiliki wa nyumba mbalimbali upande wa Mkoa wa Kinondoni. Tofauti na ile ya Madale ambayo ni maarufu kwa watu Ila ananyumba yake aliyonunua Kunduchi jiwe gumu walishawahi kuishi Harmonize na Jackline Wolper kwa nyakati tofauti. Pia ana nyumba pale Salasala machimbo ya mawe.
Yes kunduchi kule uswazi wanapouza kokoto ni kibanda, jamaa chai sana
 
Diamond yuko juu sana ya nice
Diamond amewekeza mpk sasa anazidi kukaza
Nice alikuwa hana nidhamu ya hela kwa wakati wake ule

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app


Mr. Nice alikuja kufanya fujo show ya watu Jolly Club, Upanga enzi hizo. Jamaa wanafanya show live yeye akawaletea mazereu, ikabidi majibizano yaanze, Mr. Nice akatangaza, kama wewe ni demu na umevaa pedo, kula bia. Malaya wote wa Jolly Club wakalipuka Fagilia waa waa. Alizungukwa na machangu kama 30 hivi. Mimi niwaambie ndugu zangu, ile sio discipline ya pesa, lazima ulosti. Kama unataka pesa zako zikusaidie baadae, usizivuruge.
 
Yeah....moja ya mbwembwe zao
Ulimsikia ggy mny anakuambia napanga
Nyumba ya $2000 kwa mwezi[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
Kesho akalia insta kwamba baba watoto kamzalisha tu hahudumii mtoto hana kodi.
Huyo kibakuli ukimuona sijui hata km anapata laki 5 kazini kwake.
 
Msanii wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema kila mwezi huingiza Sh200 milioni kutokana na kuingia mikataba na kampuni mbalimbali kuwa balozi wa bidhaa zao.

Akizungumza katika kipindi cha TheSwitch kinachorushwa na redio ya Wasafi leo Alhamisi Januari 28, 2021, Diamond amesema fedha hizo ni mbali na zile anazoingiza kupitia muziki.

Amebainisha kuwa anaingia mikataba na kampuni na amekuwa akifanya hivyo kwa kila kampuni inayohitaji huduma yake.

“Endosment zangu mimi mshahara wangu kwa mwezi si chini ya milioni 200, na tunasaini mikataba kila siku. Ninaingiza kwa wiki Sh55 milioni kwa siku Sh7 milioni kwa saa moja Sh300,000 na kwa sekunde Sh6,000.”

Amesema mwaka 2021 fedha anazozipata katika eneo hilo huenda zikaongezeka kwa kuwa anatarajia kuwa balozi wa vitu vingi zaidi kwa kuwa ameamua kufanya muziki kuwa kazi na biashara.

View attachment 1689019
=====

Ina maana hii ni kwa endorsement za matangazo tu
Akishaingiza hizo mil 200 anazitumiaje? Hilo ndio swali la kujiuliza.
 
Back
Top Bottom