Kumbe bwawa la Nyerere yalikuwa maono, Kenya yafunga mkataba wa miaka 25 kununua umeme wa bwawani kutoka Ethiopia

Kumbe bwawa la Nyerere yalikuwa maono, Kenya yafunga mkataba wa miaka 25 kununua umeme wa bwawani kutoka Ethiopia

Shida kwenye mradi wetu unategemea maji ya mvua na mito midogo!hivi vyanzo vinaweza kukauka,kama inavyotokea sasa hv,maji yemepungua chanzo Cha ruvu,umeme umekuwa shida,Ethiopia wanategemea maji ya mto Nile,kutoka ziwa Victoria!hiki chanzo hakitakauka,mpaka milele!
Shuleni ulienda kusomea ujinga? Tangu lini maji ya ziwa Victoria yanatiririka kwenda Ethiopia? White Nile ndiyo mto unaotiririsha maji kutoka ziwa Victoria kwenda Misri kupitia Uganda na Sudani Kusini. Blue Nile ni mto unaoanzia ziwa Tana nchini Ethiopia na kwenda kuungana na White Nile Khartoum nchini Sudani. Hivyo basi bwawa la Ethiopia limejengwa kwenye Blue Nile unaotiririsha maji kutoka ziwa Tana na si Victoria kama unavyofai.
 
Tofauti iliyopo kati yetu na bwawa la Ethiopia ni vyanzo, wakati sisi tunategemea maji ya mvua yakajaze mito hasa Ruvu ndio maji ya kutosha yapatikane bwawani, Ethiopia chanzo chao ni mto Nile unaoanzia Ziwa Victoria, hawa waliona mbali zaidi.
Acha kupotosha, Ethiopia chanzo chao ni Blue Nile kinaanzia ziwa Tana nchini Ethiopoa na si Victoria. Chanzo cha White Nile ndicho kinachoanzia ziwa Victoria.Hivi shuleni ulienda kusomea ujinga?
 
Hakuja na hilo wazo, lilikuwepo tangu enzi za Nyerere.
Lilikuwepo ila lilikuwa wazo mfu, alihitajika mtu wa kuja kulifufua maana ilionekanika ni suala lisilo wezekanika
 
Hizo ni nadharia leta takwimu hilo bwawa limeajiri watu wangapi, Ethiopia impata wawekezaji wangapi kupitia hilo bwawa?

Jiulize kwanini Kenya inaonunua umeme kutoka Uganda na Ethiapia kwanini mpaka leo imebaki kuwa industrial hub ya Africa mashariki kuliko nchi zenye umeme wawakika
Watu kuajiriwa sio nadhari, wanaonekana na wanafanya kazi. Uwekezaji ni mchakato endelevu na ngumu kuunadi ukiwa huna nishati ya uhakika.

Kenya imekuwa ilipo kwa sababu za kihistoria na Ethiopia na wengineo wanajaribu kuibadili. Umeme uliozidi Ethiopia obvious utatafutiwa matumizi ikiwemo viwanda.

Kuongeza tu, Ethiopia inaenda kufanya kilimo kikubwa sana cha umwagiliaji kupitia bwawa lake hilo.
 
Tofauti iliyopo kati yetu na bwawa la Ethiopia ni vyanzo, wakati sisi tunategemea maji ya mvua yakajaze mito hasa Ruvu ndio maji ya kutosha yapatikane bwawani, Ethiopia chanzo chao ni mto Nile unaoanzia Ziwa Victoria, hawa waliona mbali zaidi.

1668939948098.png

Read more : https://www.sis.gov.eg/section/52/9426?lang=en-us
 
Kwani baada ya miaka 50 ndiyo mwisho wa maisha sawa tuanzie kwenye hiyo 50 kwenda 200 hiyo ni faida au hasara?
 
Tofauti iliyopo kati yetu na bwawa la Ethiopia ni vyanzo, wakati sisi tunategemea maji ya mvua yakajaze mito hasa Ruvu ndio maji ya kutosha yapatikane bwawani, Ethiopia chanzo chao ni mto Nile unaoanzia Ziwa Victoria, hawa waliona mbali zaidi.
Chanzo cha maji cha bwawa la Ethiopia siyo Ziwa Victoria (White Nile) bali ni Blue Nile inayoanzia milima ya huko huko Ethiopia!
 
Tofauti iliyopo kati yetu na bwawa la Ethiopia ni vyanzo, wakati sisi tunategemea maji ya mvua yakajaze mito hasa Ruvu ndio maji ya kutosha yapatikane bwawani, Ethiopia chanzo chao ni mto Nile unaoanzia Ziwa Victoria, hawa waliona mbali zaidi.

We ni kitojo Ruvu na Bwawa la Nyerere wapi na wapi? Hujui tofauti ya Ruvu na Rufiji halafu unaandika upopoma
 
Acha kupotosha, Ethiopia chanzo chao ni Blue Nile kinaanzia ziwa Tana nchini Ethiopoa na si Victoria. Chanzo cha White Nile ndicho kinachoanzia ziwa Victoria.Hivi shuleni ulienda kusomea ujinga?
Kusomea ujinga maana yake nini? ningesomea ujinga hata hilo ziwa Victoria nisingelijua wala mto Nile, na usipende ku copy maneno ya wengine, huko ndio kujifunza ujinga, tafuta yako!
 
Acha akil za ajabu muwe mnasoma kwanza ! Chanzo cha kutoka ziwa Victoria sicho kilichopo Ethiopia, kule kuna chanzo kingine. Hujui kama kuna blue Nile na White Nile na vyote vinakutana Sudan. Pia chanzo chenye maji mengi ni kile kinachotoka Ethiopia ndo maana Wamisri walipiga kelele sanaa
Muhimu chanzo cha maji ya hilo bwawa ni kutoka ziwani, ambapo wana chanzo cha uhakika cha kuzalisha umeme, hilo la blue Nile sikuwa na wazo nalo.
 
Bwawa la Ethiopia lime cost wafadhiri $6bn I.e $6000m + environment costs and risks kwa miaka 50 litawarudishia $500m minus operational cost, ni kama $300m, hiyo biashara haifae bora ununue umeme kuliko kutengeneza bwawa.
Kama Kenya tu watalipa USD milioni mia kwa mwaka kwq miaka hansini watakuwa wamelipa USD milioni elfu tano i.e USD bilioni tano; kama walijenga kwa USD Milioni elfu sita huoni kuwa almost watakuwa wamerudisha hela waliyoinvest? Kumbuka kenya hawanunui umeme wote ni megawati 2 000 tu kati ya 5,000.. Hizo zingine zitauzwa ndani ya nchi na pia kuchochea uzalishaji katika sekta nyingi tu. umeme wa ethiopia utawalipa sana
 
Unatagemea hela irudi ndani ya mwaka mmoja au mimi ndo sijakuelewa.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Kama Kenya tu watalipa USD milioni mia kwa mwaka kwq miaka hansini watakuwa wamelipa USD milioni elfu tano i.e USD bilioni tano; kama walijenga kwa USD Milioni elfu sita huoni kuwa almost watakuwa wamerudisha hela waliyoinvest? Kumbuka kenya hawanunui umeme wote ni megawati 2 000 tu kati ya 5,000.. Hizo zingine zitauzwa ndani ya nchi na pia kuchochea uzalishaji katika sekta nyingi tu. umeme wa ethiopia utawalipa sana
Mkuu hiyo sio biashara mantainanxe ya bwawa iko juu sanaa, miaka 50 cabinet yote ya mawaziri watakua wamesha kufa na umasikini utabaki pale pale, bora hiyo pesa $6bn Uwekeze kwenye viwanda zaidi ya 1000 ununue umeme kwa nchi isio kua na viwanda, utaweza kutowa ajira za moja kwa moja sio chini 1m kwa raia wakawaida purchasing power zita ongezeka na domestic market itapanuka zaidi, viongozi wetu wamejaa mihemko bila kua na real strategic planning.
 
Sasa unashangaa nchi kama yetu kutegeneza umeme mwingi wenye gharama kubwa ni nini, wakati hata viwanda hatuna, 90% ya bidhaa tunao tumia ukiondowa nafaka inatoka nje,
nchi imeshindwa hata kusambaza maji safi na salama katika mji wake mkuu eti inakimbilia mega project ya hydro electricity power ambayo sio reliable na hi global worming tutalia mapema raisi jpm hakua real planning man anakurupuka mno.
 
Mkuu hiyo sio biashara mantainanxe ya bwawa iko juu sanaa, miaka 50 cabinet yote ya mawaziri watakua wamesha kufa na umasikini utabaki pale pale, bora hiyo pesa $6bn Uwekeze kwenye viwanda zaidi ya 1000 ununue umeme kwa nchi isio kua na viwanda, utaweza kutowa ajira za moja kwa moja sio chini 1m kwa raia wakawaida purchasing power zita ongezeka na domestic market itapanuka zaidi, viongozi wetu wamejaa mihemko bila kua na real strategic planning.
Mkuu hiyo sio biashara mantainanxe ya bwawa iko juu sanaa, miaka 50 cabinet yote ya mawaziri watakua wamesha kufa na umasikini utabaki pale pale, bora hiyo pesa $6bn Uwekeze kwenye viwanda zaidi ya 1000 ununue umeme kwa nchi isio kua na viwanda, utaweza kutowa ajira za moja kwa moja sio chini 1m kwa raia wakawaida purchasing power zita ongezeka na domestic market itapanuka zaidi, viongozi wetu wamejaa mihemko bila kua na real strategic planning.
Mkuu hauko sahihi.

Bwawa la Kidatu Morogoro lilijengwa na kukamilika miaka ya katikati ya 1970 nadhani ilikuwa 1976 hadi leo ni miaka 46 na bado linafanya kazi. Kuhusu gharama za maintenance ya dam, kwanza elewa hakuna production unit yeyote isiyo na gharama za maintenance hata hivyo viwanda unavyovisema navyo vina maintenance costs. Ukokotoaji wa gharama za mradi huzingatia gharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji ikiwemo maintenance, urudishaji gharama na faida. Elewa kuwa kabla mradi wowote haujajengwa huwa inafanyika kitu inaitwa economic analysiss ambapo kuna vigezo rasmi vya kuchambua kama mradi utakuwa na faida au la vinaitwa B/C ratio (benefit cost), IRR (Internal rate of return) na NPV (Net present value; hivi vyote ndivyo hutumika kutoa majibu kama mradi ujengwe au la. Pili ule mradi wa Ethiopia umejengwa kwa pesa ya diaspora mbalimbali waliochangia kidogo kidogo haukujengwa kifisadi .

Hivyo viwanda unavyodhani ni bora kwanza elewa viwanda sio majengo tu kuna mambo mengi lazima uyazingatie kabla hujajenga kiwanda: Je unajenga kiwanda cha nini, je unayo teknolojia yako au unategemea ukodi teknooijia? Unao wafanyakazi ambao ni skilled katika uzalishaji unaotaka kufanya? Malighafi inatoka wapi?Unatarget soko gani la nje au la ndani? Je bidhaa yako inao uwezo wa kushindana na bidhaa toka nje huko sokoni kwa ubora na bei? Kuna mambo mengi ndio maana wengine wana viwanda wengine hawana. Hao wananchi unaosema watapata ajira wanazo sifa za kuajirika? Miaka ya sitini na sabini tulijenga hivyo viwanda unavyosema lakini vilikuwa aina ile inaitwa import substitution industries ambavyo vilitegemea sana malighafi za nje hivyo kutengeneza tatizo la fedha za kigeni, ilifika wakati vilioperate chini ya asilimia 30 na vingine vilifungwa kabisa ndipo likaja wimbi la ubinafsishaji ambapo vikauzwa kwa bei za kutupwa miaka ya 80 na tisini.

Aidha hata kama viwanda vinaweza toa ajira bado watu wenye miaka kuanzia 50 na kuendelea hawawezi kuajiriwa katika hivyo viwanda na bado hilo kundi linahitaji kipato.

Katika suala zima la nchi kupiga hatua za maendeleo kiuzalishaji (GDP) upatikanaji wa umeme wa uhakika ndio kigezo namba moja kinachoangaliwa (ingawa kuna vigezzo vingine kadhaa).

Bwawa la Ethiopia litawasaidia sana kuongeza uzalishaji wa viwandani na shughuli zingine za kiuchumi ikiwemo kuuza umeme wa ziada na walifanya uamuzi sahihi kujenga hilo bwawa.
 
Back
Top Bottom