Kumbe Diamond Karanga Diamond ni balozi! Mali ni ya Joseph Kusaga

Kumbe Diamond Karanga Diamond ni balozi! Mali ni ya Joseph Kusaga

Binafsi sipendi kuongelea watu na mambo ya wasanii lakini hili limenigusa sana sana.

Kama mnakumbuka namna mr Nice alivyokuwa akiishi maisha ya kuigiza,steven kanumba hivyo ivyo pamoja na wasanii wengine sikuua kama msanii mahiri kama Diamond akiingizwa katika ujinga huo huo na wasaka pesa.

Kutokana na ugomvi wa chini chini baina ya kundi la WCB na Clouds media hasa chanzo kikiwa ni mradi wa redio na tv..sasa akina kusaga wameweka wazi kuwa zile Karanga za Diamond Karanga ni mali ya kampuni ya Clouds na Diamond ni balozi tu.

Nimeumia sana,maana nimekuwa nikimuona diamond kama kijana anayesaka fursa licha ya kutokuwa na elimu ya kutosha.

Namuomba diamond afanye yake atatoboa badala ya maisha ya show.

--------------------\

Mbona hizo karanga zilikuwepo hapo nyuma,
Zikiwa chini ya smart industry
Na baadae wakaingia mkataba wa kutumia jina la Diamond na zikaanza kuitwa Diamond karanga,

Kutoka hapo karanga zinauzwa kwa hali ya juu.

Na wala sijawahi kuona siku Diamond amesema ana kiwanda cha karanga.

Analipwa kwa kuvaa uhusika wa owner wa Diamond karanga na hiyo ni fursa aliyoiona.

Sasa wewe usiumie na mambo ya maisha yako umia na mtu anaingiza pesa zake.
 
Diamond huwa anasema : amekuwa Muuza karanga, na atatoa zawadi ya ushindi ya gari au TV, kumbe karanga zenyewe sio zake, Tutakutanaje shell anipe zawadi yangu? Halafu kuna watu husema Tz kuna Tume ya kuzuia michezo ya bahati nasibu, Hivi ni kweli kama mambo yenyewe ni usanii usanii namna hii, nasikia na hii michezo ya Biko, Tatu mzuka ni usanii mtupu, Hao tume wako wapi, Biko ni hao hao clouds
 
Back
Top Bottom