Mfano kuna kijana anatengeneza laptop na simu, ana ofisi nzuri tu inayoaminika. akitengeneza laptop yako inarudi katika hali yake na unaweza kuendelea kuitumia bila tatizo
Huyu kijana ana elimu ya IT ila hajasoma akafaulu mtihani wowote unaohusu IT. Inamaana kumbe inawezekana tukawa na elimu bila kufaulu mitiani kisha utendaji ukaamua nani ni kaelimika ?
Hapo hapo yupo graduate ambaye amefaulu kwa A za kutosha lakini na hana hiyo elimu ya kutengeneza laptops na atahitaji muda tena kuipata elimu.