Kumbe Khalfan Bwire na wenzake ndio walikuwa Walinzi wa Tundu Lissu wakati anaingia Tanzania Julai 28, 2020?

Aisee kumbe usione vyaelea vimeundwa. Hii inatupa picha gani nyie wataalam

Mgombea wa Chama kikuu cha Upinzani Mh Tundu Lissu alikuwa akilindwa na hawa ma x commandos yaani Khalfani Bwire, Adamu Kusekwa, Mohamed Ligwenya na wenzake.

Baada ya matishio makubwa ya usalama dhidi ya viongozi hawa wa upinzani Kamati kuu ya chama ikiongozwa na Kurugenzi ya intelijensia na Usalama ndani ya chama waliamua kutafuta ulinzi mkali na usio na doa kuhakikisha usalama wa Viongozi wao.

Hayo yamebainika wakati wa mahojiano mahakamani kutoka kwa Msomi Wakili Peter Kibatala Jana ktk kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Imeelezwa kuwa baada ya walinzi hawa kukamatwa na kutiwa ndani hali ya usalama wa Tundu Lissu ilikuwa hati hati na ndio sababu ya Tundu Lissu kukimbilia Ulaya tena kuokoa uhai wake.

Wenzangu nyie mnaelewa sasa kinachoendelea huko?

Walitaka kumuua Lissu
 
Tufikirie tu kidogo nje ya siasa, hivi mamlaka zikikutaka ndani ya ardhi ya Tanzania kweli zinaweza kukushindwa hata kama unalindwa na Commandoz?

Kumbuka hizo mamlaka ndio zinamiliki maelfu ya makomando na silaha zote..

Si kweli eti TL aliamua kukimbia baada ya hao makomando kuacha
Tufikirie tu kidogo nje ya siasa, hivi mamlaka zikikutaka ndani ya ardhi ya Tanzania kweli zinaweza kukushindwa hata kama unalindwa na Commandoz?

Kumbuka hizo mamlaka ndio zinamiliki maelfu ya makomando na silaha zote..

Si kweli eti TL aliamua kukimbia baada ya hao makomando kuacha kumlinda.

Mbona hakukimbia kabla ya uchaguzi?
Baada ya kumaliza uchaguzi hakua na kazi ya kufanya tanzania hivyo akaona aondoke tu.
Magufuli alikuwa muuaji na wala hilo halina ubishi sasa kama wangeendelea kukaa hapa na kucheza kamari huenda leo hii wangekuwanae huko wakimzaba vibao kwa kuwaua.

Wewe rais wa nchi mpaka anaunda genge la wauaji hadi anawapachika jina la wasiojulikana unafikiri huyo ni mtu wa kubeza. Alimwambia Ndugai wewe utawashughulikia huko bungeni na mimi nitadili nao huku nje, huyo kweli ni mtu si shetani 😈 kabisa.
 
Tundu Lissu alirejea tarehe 27 July 2020. Hao Makomandoo wamekamatwa mwezi wa nane.
Ni sahihi walikuwepo kumpokea Tindu Lissu AirPort tarehe 27 July.

Hakuna ubaya wowote kutukua ex soldiers kwa shughuli za ulinzi. In fact wanatumika hivyo sehemu mbalimbali.
Unajua kuwa Urio alikutana tarehe kati tarehe 10 mpaka 15 july ndio akamwambia issue ya kumtafutia hao makomandoo,? Unajua mpaka tarehe 24july bado makomandoo walikuwa hawajaenda kuonana na na mbowe, rudi kwenye massage za akina Mbowe na urio utaona, ni lini walitumiwa nauli.
 
Walikamatwa mwezi August. Lissu alirudi Tanzania tarehe 27 July.
Sasa km alirudi tarehe 27 july, mpaka tarehe 24july hawa makomandoo walikuwa bado hawajafika kwa Mbowe, rudi kwenye massage za Mbowe na urio utaona lini Urio aliwatafuta na walipotumiwa nauli,
 
Kwa hiyo utafutiwe watu siku mbili tuu hata ujawajua vizuri uwape kazi ya kukulinda Kelli. Kwann mnadanganya watu hivi?? Au unaona watu woote wanaakili za kitoto, hawa makomandoo mpaka kufika July, 24 2020 walikuwa hawajaenda kwa Mbowe, lissu alikuja July 17, 2020. Yaan ndio walinzi wanakuaga recruited. Acha kutudanganya
Je kwenye hiyo video ya kumpokea Lisu wanaonekana?
 
Tundu Lissu alirejea tarehe 27 July 2020. Hao Makomandoo wamekamatwa mwezi wa nane.
Ni sahihi walikuwepo kumpokea Tindu Lissu AirPort tarehe 27 July.

Hakuna ubaya wowote kutukua ex soldiers kwa shughuli za ulinzi. In fact wanatumika hivyo sehemu mbalimbali.
Mweleze vizuri amekalia ubishi tu.
 
... ni kipi kina-make sense zaidi;

(1) kuwapa watu kazi ya KUKULINDA, watu ambao umefahamiana nao kwa siku mbili (kama unavyodai wewe) ila ulitafutiwa na uliyeamini kwamba ni rafiki yako mliyefahamiana kwa muda mrefu?
AU
(2) kuwapa watu kazi ya kufanya UGAIDI, watu ambao umefahamiana nao kwa siku mbili (kama unavyodai wewe) ila ulitafutiwa na uliyeamini kwamba ni rafiki yako mliyefahamiana kwa muda mrefu?

Kwako kati ya hayo mawili lipi ni sensible zaidi?
You are comment is supper.
 
Ndio maana namchukia sana Magufuli, huyu jamaa ntamuombea dua mbaya maisha yangu yote, alikuwa na roho mbaya sana uyu mshenzi.

Mitoto inazaliwa kisha inanukishwa ugolo halafu gafla tu linaukwaa uraisi, wananchi wake hawawez kuwa salama katu.

JPM moto wa milele umuangazie na kumchoma rest of his life uko alipo
Ingekuwa mtu ukifanya matendo ya hovyo kama jiwe na ukifa adhabu hata wanao na mkeo watapewa sehemu ya adhabu ingesaidia watu kuogopa kutenda matendo ya hovyo maana watatithisha taabu uzao wao.
Lakini sivyo, ona kule Chato wanakula Bata tu kwa kodi zetu!
 
Tufikirie tu kidogo nje ya siasa, hivi mamlaka zikikutaka ndani ya ardhi ya Tanzania kweli zinaweza kukushindwa hata kama unalindwa na Commandoz?

Kumbuka hizo mamlaka ndio zinamiliki maelfu ya makomando na silaha zote..

Si kweli eti TL aliamua kukimbia baada ya hao makomando kuacha kumlinda.
Mkuu mamlaka ya Tanzania ikimtaka yoyote yule.. Inampata hata kama ni balozi wa nje.. Inampata.. Mamlaka ingemtaka Lissu ingempata tuu hata kama angelindwa na UN.
Shida ya Tanzania wakati ule wa awamu ya giza (5) mamlaka ilikuwa ikikutaka kwa njia mbili.. Ambazo ni wito / au hata taarifa unaenda na nyingine ni kufanyiwa arrest...
Lakini awamu hiyo hiyo mamlaka ilikuwa na njia za giza zingine ambazo unapotea tuu.. Au unatandikwa risasi tu bila kujua aliyefanya hivyo ni nani... Sasa ukiweka ulinzi mkali hasa matendo ya gizani yatoweke ndio shida ikawatokea hawa makomandoo
 
Aisee kumbe usione vyaelea vimeundwa. Hii inatupa picha gani nyie wataalam

Mgombea wa Chama kikuu cha Upinzani Mh Tundu Lissu alikuwa akilindwa na hawa ma x commandos yaani Khalfani Bwire, Adamu Kusekwa, Mohamed Ligwenya na wenzake.

Baada ya matishio makubwa ya usalama dhidi ya viongozi hawa wa upinzani Kamati kuu ya chama ikiongozwa na Kurugenzi ya intelijensia na Usalama ndani ya chama waliamua kutafuta ulinzi mkali na usio na doa kuhakikisha usalama wa Viongozi wao.

Hayo yamebainika wakati wa mahojiano mahakamani kutoka kwa Msomi Wakili Peter Kibatala Jana katika kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Imeelezwa kuwa baada ya walinzi hawa kukamatwa na kutiwa ndani hali ya usalama wa Tundu Lissu ilikuwa hati hati na ndio sababu ya Tundu Lissu kukimbilia Ulaya tena kuokoa uhai wake.

Wenzangu nyie mnaelewa sasa kinachoendelea huko?

Nilijiuliza sana aisee.kuwarudisha mtaani makomando wanne waliofundishwa wakaiva.Naona kama ni hatari kubwa ikiwa wataamua kujiingiza kwenye uharifu.halafu kwenye maelezo inaonekana mwingine aliamua kwenda kuanza kuponda kokoto baada ya kutimuliwa jeshini.
 
Kwa mujibu wa mashataka ya mchongo. Lakini ukweli ni huo
Sawa sasa wewe mbona unasema mambo ya uongo, unajua kabisa tarehe 20july Mbowe alimuuliza umefanikiwa wangapi akajibu wawil, akamwambia hao wawil kwa kuanzia sio mbaya, sasa hizo ni msg na, july 20 alitumiwa nauli 500,000/= , 24july walikutana moro akawafanyia vetting alafu ndio wakaenda kwa Mbowe,
 
Tufikirie tu kidogo nje ya siasa, hivi mamlaka zikikutaka ndani ya ardhi ya Tanzania kweli zinaweza kukushindwa hata kama unalindwa na Commandoz?

Kumbuka hizo mamlaka ndio zinamiliki maelfu ya makomando na silaha zote..

Si kweli eti TL aliamua kukimbia baada ya hao makomando kuacha kumlinda.
Mamlaka inatenda kwa mujibu wa sheria, hapo kwenye kutenda maovu ni watu individual ndani ya mamlaka.
Matendo ya Magufuli sio official kama amemnyonga Ben, ni yeye binafsi kwa kutumia raslimali za umma. Hivyo lazima afanye kwa siri
 
M
Tufikirie tu kidogo nje ya siasa, hivi mamlaka zikikutaka ndani ya ardhi ya Tanzania kweli zinaweza kukushindwa hata kama unalindwa na Commandoz?

Kumbuka hizo mamlaka ndio zinamiliki maelfu ya makomando na silaha zote..

Si kweli eti TL aliamua kukimbia baada ya hao makomando kuacha kumlinda.

Mbona zilishindwa kwa Hamza.
 
Mkuu mamlaka ya Tanzania ikimtaka yoyote yule.. Inampata hata kama ni balozi wa nje.. Inampata.. Mamlaka ingemtaka Lissu ingempata tuu hata kama angelindwa na UN.
Shida ya Tanzania wakati ule wa awamu ya giza (5) mamlaka ilikuwa ikikutaka kwa njia mbili.. Ambazo ni wito / au hata taarifa unaenda na nyingine ni kufanyiwa arrest...
Lakini awamu hiyo hiyo mamlaka ilikuwa na njia za giza zingine ambazo unapotea tuu.. Au unatandikwa risasi tu bila kujua aliyefanya hivyo ni nani... Sasa ukiweka ulinzi mkali hasa matendo ya gizani yatoweke ndio shida ikawatokea hawa makomandoo
hii ni dunia ya mwaka gani? Chukua nafasi kujielimisha mkuu achana na story za season na series
 
Tufikirie tu kidogo nje ya siasa, hivi mamlaka zikikutaka ndani ya ardhi ya Tanzania kweli zinaweza kukushindwa hata kama unalindwa na Commandoz?

Kumbuka hizo mamlaka ndio zinamiliki maelfu ya makomando na silaha zote..

Si kweli eti TL aliamua kukimbia baada ya hao makomando kuacha kumlinda.
Ni kweli serekali ikikutaka haitakukosa. Lkn pia hawatakuondoa kama mbuzi achinjwavyo machinjioni, hata zile pure dictatorship regimes wanawekaga tusababu sababu ku mu excute mtu.
Binafsi mpaka dakika hii naamini awamu ya Magu alishiriki kikamilifu kumhujumu Lisu.
 
Sasa mpaka tarehe 24july walikuwa hawajafika kwa Mbowe na kumbuka walikamatwa kabla hata hawajaanza kazi. Wewe vip boss
Kwa uhakika gani? Mbowe alituma laki tano ya nauli tarehe 20 July. Baada ya hapo wakaenda Moshi kumfuata Mbowe,
Most likely Mbowe akaja nao Dar kumpokea Lissu tarehe 27 July.

Hivi wengine mnasoma case ipi?
 
Back
Top Bottom