Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Ni vizuri kivuta kitu ya Arusha iliyokaushwa,mbichi ina madhara sana.Ata tukihoji kwanini bei za vyakula zipo juu na tunalima wenyewe,majibu ni kuwa na huko Duniani hali ni hiyohiyo!
 
Import bill kuongezeka kutokana na Sababu mbalimbali ikiwemo mfumuko wa vitu huko ughaibuni..

Ndio maana Ili kujinasua Nchi nyingi saiizi zimeanza kuikacha dollar
Ujue pesa ya kigeni hupatikana kwa exports
Hata hizo pesa zingine zikitumika itafika wakati demand and supply itafanya kazi yake
 
Nchi masikini za Afrika zinajenga uchumi wa china na kumnufaisha china bila kujua , unaagiza bidhaa nyingi kuliko unachouza nje ,mwisho wa siku wewe ni looser Maana hutakiwa na pesa za kigeñi na thamani yako ya pesa itashuka
Dunia nzima inaitegemea china kama kiwanda.

Leo Tanzania imewakabidhi Wachina wajenge maduka 2060 ambayo yatahitaji bidhaa kutoka China.
Maana yake Wachina watahitaji kununua kwao zaidi na waje kutuuzia kwetu
 
Huna option labda Serikali izuie msululu wa bidhaa za kutoka China kiasi ikifanya hivyo na wao wanajibu Kwa kuweka vikwazo vya uhafifu wa bidhaa zenu..

Njia pekee ni kuzalisha import substites na kuongeza investments zako tuu.
Swala ni rahisi sana tuwekeze kwenye kilimo bora ili tuuze mazao nje.

Hao wachina waje wajenge viwanda na kuuza nje na sio kuwa wauza maduka
 
Hili swala litasumbua sana na wataofaidika ni kina Azam, MO maana wao wanauza nje sana hivyo wanapata dollar.
Itafika wakati magari yatauzwa bei kubwa sana hadi tushangae
 
BOT imeipeg kwa 2330 wakati wauzaji wako 2401
 
Leo kununua Dola imefika 2, 405 Haijawahi kufikia bei hiyo hata siku moja
 
Kupitia tozo za miamala tungechangia vizuri tu miradi yote ikakamilika kwa wakati. Ingekuwa inaumiza ila kwa maendeleo ya kasi watu wangelalamika ila at last wangeelewa.
Hizo tozo hazifiki bilioni 300 kwa mwaka

Miradi inahitaji zaidi ya tril 5 kwa mwaka
 
Wenzako wanapandisha thamani ya pesa yap kuzuia mfumuko wa bei
 
Mfano nilisoma sehemu Standard Chartered Bank ndo hutumika kwenye 60% ya pesa za kigeni.
Hivyo faida yao ya Bilioni 85 ilitokana na hilo la kuhusika katika kutuma pesa
 
Ni vizuri kivuta kitu ya Arusha iliyokaushwa,mbichi ina madhara sana.Ata tukihoji kwanini bei za vyakula zipo juu na tunalima wenyewe,majibu ni kuwa na huko Duniani hali ni hiyohiyo!
Uelewa wako kwenye mambo kama haya Upo chini sana… pole
 
Swala ni rahisi sana tuwekeze kwenye kilimo bora ili tuuze mazao nje.

Hao wachina waje wajenge viwanda na kuuza nje na sio kuwa wauza maduka
Ndio hivyo ila Hilo sio swala la overnight so hakiwezi kuleta suluhu ya upungufu wa dollar in short term maana it needs time,pesa za investments na Wataalamu wa irrigation na mambo ya processing na masoko..

Kwa hiyo ndicho Serikali inafanya Kwa Sasa ,wameanza mwaka Jana so itsweza kuleta matokea labda kuanzia 2025 huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…