Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Jamani tuwe tunasoma soma kidogo! Tatizo la uhaba wa USD currency sio la Tanzania peke yake, hili ni tatizo la dunia yote. Please soma link hizi hapa chini kwa taarifa zaidi



Ni vizuri kivuta kitu ya Arusha iliyokaushwa,mbichi ina madhara sana.Ata tukihoji kwanini bei za vyakula zipo juu na tunalima wenyewe,majibu ni kuwa na huko Duniani hali ni hiyohiyo!
 
Import bill kuongezeka kutokana na Sababu mbalimbali ikiwemo mfumuko wa vitu huko ughaibuni..

Ndio maana Ili kujinasua Nchi nyingi saiizi zimeanza kuikacha dollar
Ujue pesa ya kigeni hupatikana kwa exports
Hata hizo pesa zingine zikitumika itafika wakati demand and supply itafanya kazi yake
 
Nchi masikini za Afrika zinajenga uchumi wa china na kumnufaisha china bila kujua , unaagiza bidhaa nyingi kuliko unachouza nje ,mwisho wa siku wewe ni looser Maana hutakiwa na pesa za kigeñi na thamani yako ya pesa itashuka
Dunia nzima inaitegemea china kama kiwanda.

Leo Tanzania imewakabidhi Wachina wajenge maduka 2060 ambayo yatahitaji bidhaa kutoka China.
Maana yake Wachina watahitaji kununua kwao zaidi na waje kutuuzia kwetu
 
Huna option labda Serikali izuie msululu wa bidhaa za kutoka China kiasi ikifanya hivyo na wao wanajibu Kwa kuweka vikwazo vya uhafifu wa bidhaa zenu..

Njia pekee ni kuzalisha import substites na kuongeza investments zako tuu.
Swala ni rahisi sana tuwekeze kwenye kilimo bora ili tuuze mazao nje.

Hao wachina waje wajenge viwanda na kuuza nje na sio kuwa wauza maduka
 
Kila siku tunanunua mavitu kwa pesa za nje miradi yote tunalipa kwa Dollars
Meanwhile hakuna tunachofanya kupata hizo dollars hatuuzi vitu nje
Walitegemea izo pesa hazina hazitaisha?
Miezi zaidi ya 5 dollar haipo banks wanasema hawawezi kukupa peke ako dollar 8000 waache wengine
Kama una kihela chako hauna mpango nacho usiweke fixed acc kanunue dollar sindika ndani mpaka mama atoke unaenda unachange
Hili swala litasumbua sana na wataofaidika ni kina Azam, MO maana wao wanauza nje sana hivyo wanapata dollar.
Itafika wakati magari yatauzwa bei kubwa sana hadi tushangae
 
Hata hizo nchi ulizozitaja zina reserve za kutosha za USD, achilia mbali uwekezaji waliofanya ama serikali zao ama matycoon wao wote upo katika usd.

Leo hata hao suppliers wa china sijui india wanakomaa walipwe kwa dollar. Hawataki kusikia kbs habar za currency za nchi zao.

Ila kinachoshangaza bongo ni exchange rate. Naona mamlaka imeamua kuifix/peg.

Athari zake ni kubwa sana, ikiwamo black markets, wananchi kuitilia shaka financial system na watu ku hold hard cash in usd bila kuziweka kwenye mifumo rasmi.
BOT imeipeg kwa 2330 wakati wauzaji wako 2401
 
Huko Twitter Carol Ndosi aliuliza "Kuna Uhaba wa Dola"? Majibu yalikuja ata kwa kwa watumishi wengine wa bank wakisema ndiyo!

Sasa hizi mbwembwe za World Bank Uchumi wenu huko imara unatokana na nini kama Reserve yetu ya USD iko chini?

Wachumi tuambiane! Mbona exchange ya USD bado iko palepale ikiwa kuna uhaba wa dola kiasi hiki?
View attachment 2607741
View attachment 2607742
Leo kununua Dola imefika 2, 405 Haijawahi kufikia bei hiyo hata siku moja
 
Dollar inakwenda kupoteza thamani yake kama reserve currency ya Dunia. Kibano cha sasa kimewabana wamarekani kuchapisha Dollar na kuzimwaga hovyo Duniani, imewapasa kuzungusha ile iliyoko kwenye mzunguko na kuongeza interest rate.
Dollar inakwenda kuadimika na kupoteza thamani, hata ukiipata na kuificha haitakuwa na thamani ile yuliyoizoea.
BOT amkeni.... Anzeni kuhifadhi dhahabu ya kutosha, siku zijazo kutakuwa na dhoruba kali kwenye soko la fedha.
Wenzako wanapandisha thamani ya pesa yap kuzuia mfumuko wa bei
 
Mifumo ya kulipa inafanywa kupitia overseas Nostro accounts kupitia mabenki ya US kama Citibank , Bank of America etc hii inamaanisha lazima tuwe na credit account balances ktk hayo mabenki.
Kuna kampuni kubwa inaitwa Travelex ina deal na kkt import na export ya forex hard cash ambazo zikifika huko zinacredit account zetu za USD ktk overseas Banks kwa ajili ya kufanya malipo ktk USD.
Mfano nilisoma sehemu Standard Chartered Bank ndo hutumika kwenye 60% ya pesa za kigeni.
Hivyo faida yao ya Bilioni 85 ilitokana na hilo la kuhusika katika kutuma pesa
 
Ni vizuri kivuta kitu ya Arusha iliyokaushwa,mbichi ina madhara sana.Ata tukihoji kwanini bei za vyakula zipo juu na tunalima wenyewe,majibu ni kuwa na huko Duniani hali ni hiyohiyo!
Uelewa wako kwenye mambo kama haya Upo chini sana… pole
 
Swala ni rahisi sana tuwekeze kwenye kilimo bora ili tuuze mazao nje.

Hao wachina waje wajenge viwanda na kuuza nje na sio kuwa wauza maduka
Ndio hivyo ila Hilo sio swala la overnight so hakiwezi kuleta suluhu ya upungufu wa dollar in short term maana it needs time,pesa za investments na Wataalamu wa irrigation na mambo ya processing na masoko..

Kwa hiyo ndicho Serikali inafanya Kwa Sasa ,wameanza mwaka Jana so itsweza kuleta matokea labda kuanzia 2025 huko.
 
Back
Top Bottom