Kumbe kuna watu wana PhD halafu wanalipwa laki 5?

Kumbe kuna watu wana PhD halafu wanalipwa laki 5?

500,000/2,318=USD216. Yaani akifunga kula mwaka mzima, atasevu USD261x12 = 2,592! Uongo huo. Amenunuaje hiyo suit? Utakuta kajenga jumba sehemu hapa Dar. Vinginevyo atakuwa mwizi.
Hahaha
 
Kwa usanii hao jamaa hutawaweza.

Hio yote ni kukwambia shukuru kwa ulicho nacho huku nyie mlioko serikalini mkipewa ujumbe wa mnalalamika nini na vi diploma/degree zenu wkt huku Chamani kuna watu wana PH.d na wanalipwa laki 5 tu.
Ni Usalama huyo.
 
Huyo jamaa amesha mbrand ktk promotion za ajira ...
Angetaja na posho anazopokea .. Usanii tu huo wa jukwaani
 
inawezekana, nitoe mfano mdogo, kuna faza yangu mdogo ana degree ila kaomba nafasi ya Afisa mtendaji kupitia cheti cha astashahada(certificate) kapata. sasa atalipwa mshahara wa kiwango gani? its obvious atalipwa 3k kwa sababu ya kuajiliwa kwa certificate ila ana degree. Ndio hali aliyokua nayo hiyo jombaa. OVER
 
Sio tatizo kabs ila wasiwasi wangu na amesoma china kabs alafu unakuja kula mshahara wa 500,000 wakat wabongo kwa boom la serikali la chuo wamejiajiri huyo atakuwa amewekwa pale kwa malengo na mzee wake
 
Kuna ambao wana PhD na wamekaa nyumbani tu wanadeki na kuosha vyombo. Taifa linapoteza sana na ingekuwa vizuri kama rais akawaita akawapatia kazi.
Hujui unaloongea wewe. Unajua kunawatu mpo kiushabiki tu. Hv mtu kasoma akawa na degree akakosa kazi bado akasoma Masters akakosa kazi hv unafikiri ni rahisi kwenda kusomea phd kweli. Wengi waosomea phd lazma awe anakazi ndio aende kusomea phd.
 
Lakini simpingi magu kwa hilo moja kwa moja,maana mimi binafsi nimewahi kufanya kazi kwenye kampuni moja ya mjasiriamali wa kihindi na utaratibu wa malipo(mshahara) ulikuwa kama ifuatavyo,Basic salary-250,000/ attendance allowance-450,000/technical allowance-300,000/loyalty-250,000/transport allowance-150,000/ fixed overtime-185,000!! Sasa hapo ukilala kazi siku moja kwa sababu yoyote ile attendance allowance inaondoka yote,jumlisha na day pay ya hiyo basic salary,na sehemu ya tech allowance,na mbaya zaidi makato ya nssf yanakatwa kutoka kwenye basic ambayo ni 10% ya hiyo 250,000 so ni 25,000 per month! Na hadi leo bado wanalipa kwa mfumo huo,sasa ikitokea tajiri akaamua kukuachisha kazi anakulipa mshahara wa miezi mitatu kama notice ambayo pia ni kwa basic salary basis,hivyo ningelipwa 750,000 tu,nchi ina uhuni hii.
 
Ha ha we jamaa utakuwa ni Engineer bila shaka
Umeona ee, wazee wa kujaza questionnaire wanaokota PhD kwenye mitandao halafu wanakuja kutusumbua na title za dr. Hivi yule jamaa msemakweli alipotelea wapi, maana aliwaumbua sana kwenye kile kitabu chake..
 
Back
Top Bottom