Kumbe Majini sio viumbe vya kuogopa, yana vibrate at low frequency kuliko sisi

Kumbe Majini sio viumbe vya kuogopa, yana vibrate at low frequency kuliko sisi

Mzee mbona tunaona mpaka watoto wadogo wa miezi 6 wanarogwa na wengine wanarogwa tangu wakiwa mimba , je Hao huwa wanakuwa wamefanya makosa gani ?? Yanayo toa nafasi ya wao kurogwa !?
Wazazi vipi,wako vizuri kiroho?hapa nazungumzia Baba na mama,Babu na bibi.Kwasababu uovu wako unaweza kusababisha kufungua mlango wa watoto au mpk wajukuu wako wakashambuliwa....
 
Katika muktadha wa kiroho, masafa ya chini (low frequency) na masafa ya juu (high frequency) mara nyingi yanahusishwa na hali tofauti za kiroho, nishati, au mtetemo wa mwili na nafsi. Hii inatokana na imani kwamba kila kitu ulimwenguni kina nishati na hutetemeka katika masafa fulani.

Masafa ya Chini (Low Frequency) Kiroho

Sifa: Masafa ya chini mara nyingi yanahusishwa na hisia au hali hasi kama vile:

Woga

Hasira

Chuki

Uchovu wa kiroho


Athari:

Hutengeneza uzito wa kiroho au kutojihisi huru.

Inaweza kuzuia ukuaji wa kiroho au kuleta hali ya kutengwa na chanzo cha nishati chanya (Mungu, ulimwengu, au nafsi yako ya juu).


Mfano:

Mtu anayepitia huzuni kali au anaelemea hali za hofu mara kwa mara mara nyingi huonekana "kuvutia" matukio ya kiroho hasi.



Masafa ya Juu (High Frequency) Kiroho

Sifa: Masafa ya juu yanahusishwa na hali chanya kama:

Upendo

Furaha

Amani

Shukrani


Athari:

Husaidia mtu kuunganishwa na nishati za juu za kiroho (Mungu, malaika, au ulimwengu wa kiroho).

Huongeza ufahamu wa kiroho, uvuvio, na hali ya amani ya ndani.


Mfano:

Sala, tafakari, au matendo ya huruma huongeza masafa ya mtu kiroho, na hivyo kumwezesha kujihisi karibu na nishati ya kimungu.



Mambo Yanayoshawishi Masafa Kiroho

Kuongeza Masafa (Kuhamia High Frequency):

Meditate (kutafakari).

Kufanya sala au maombi.

Kuonyesha shukrani na huruma.

Kuishi maisha ya maadili na kupunguza mzigo wa hasira au chuki.


Kupunguza Masafa (Kuhamia Low Frequency):

Kuzingatia mambo hasi kama wivu, chuki, au tamaa mbaya.

Kutojitunza kimwili na kiakili.

Kuwa mbali na mazoea ya kiroho au chanzo cha imani yako.



Kwa Nini Masafa ni Muhimu Kiroho?

Masafa yanaaminika kuvuta nishati zinazofanana. Masafa ya juu huvuta nishati na hali za juu kama amani na upendo, ilhali masafa ya chini huvuta hali hasi.

Watu wanaoishi katika masafa ya juu wanajulikana kuwa na nuru ya kiroho, kuvutia furaha, na kupitisha nishati nzuri kwa wengine.


Ikiwa unatafuta njia za kuinua masafa yako ya kiroho, tafakari zaidi au fanya mazoea yanayokuletea furaha na amani.
By robot
Umefafanua vyema ila haya mnayo yaongea mnapo husisha na majini ndio naona kidogo kuwa mnachanganya mambo , ...
 
Wazazi vipi,wako vizuri kiroho?hapa nazungumzia Baba na mama,Babu na bibi.Kwasababu uovu wako unaweza kusababisha kufungua mlango wa watoto au mpk wajukuu wako wakashambuliwa....
Okay nieleze kuhusu namna ambavyo generation 1 inavyo weza kuwa Na Yale majini ya ukoo + Mizimu Halafu generation Hiyo Hiyo inapoleta generation nyingine hata iwe kizazi cha nne ambacho hakikuwahi kuiona generation ya Kwanza kina kuwa kina sumbuliwa na hayo majini na Mizimu , Nini kinacho tokea maana Hiyo generation ya 4 inakuwa haina kosa wala haikuwahi kuwaona mababu na mabibi zao why wawe attached na hivyo viumbe ??

Nadhani umeshasikia kesi nyingi Tu huko mitaanj unakuta kijana alikuwa anasoma ghafla anafuatwa na Mizimu ya kwao na inataka awe mganga Yana Mpa uchizi au maradhi yasiyo pona mpaka Huyo mtu Akubali na akikataa Yana Muua mind you unakuta Huyo mtu amesha hangaika Sana mpaka basi Kwa waganga wachungaji mapadrii mashekhe lakini wapi haponi Shida inakuwa nini !? Na afanye nini ili kukwepa hivyo viumbe ,

Maana kuna viumbe vingine Vikimfuata Huyo mtu vinamtaka awe decent kama nyie mnavyosema hapa ili aweze kuwa ktk high frequency wanataka awe ana Sali asiwe mdhambi awe anatoa sadaka asiwe mfanya dhulma aepukw zinaa ,

Yaani mnayo yaelezea hapa ktk lugha ya physics kuwa ktk high frequency Nimesha waelewa ni kuwa smart kiroho kutokuwa mtenda mabaya Hilo nimeshaielewa so nataka kujua Inakuwaje kuwaje mpaka mtu afuatwe na Madudu yaliyopo ndani ya ukoo wao na yaanze kumshurutisha kuwa mtu Wa spiritual!! !? Nini hutokea na atumie mbinu zipi ili aweze kuwakwepa !?

Tirilika mkuu
 
Knowledge is power..kumbe MAJINI, WACHAWI, NA BLACK MAGIC ZOTE, zinafanyika at low vibrational frequency ndio maana ili mtu alogeke lazima washushe frequency yake awe kwenye range zao.

Kwa mfano mtu akiwa ana hofu au hasira ni rahis kumloga coz ana resonate at 7Hz very low frequency.

PEPO MCHAFU anamuingia mtu akiwa at low frequency. Siri iliyopo hapa ni kucheza frequency game isishuke, msibani watu wanalogwa sana coz wana huzuni na frequency zao zinakuwa down, bila shaka umewahi kusikia msiba mmoja umesababisha msiba mwingine then wanasingizia presha..

Labda nikuulize:

1. Marais
2. Wabunge
3. Wafanya biashara…..

Na watu wote wakubwa, huufuata Uganga na mapepo kwa Sababu gani?
 
Sina uhakika saana kama majini yana vibrate katika low frequency kuliko binadamu.

Ila uko sahihi kua binadamu tuna uwezo mkubwa/kama Mungu like father like son.

Ukijua kwanini amri kuu ni upendo pia ukibaini kwanini uliambiwa usamee saba mara sabini, ni ili kua positive na kuvunja negative energy zote. Hakika utakua salama.

Kumbe ukiwa na hekima utakundua kitabu cha biblia ni moja ya vitabu adimu, ni hazina (kwani kina code muhimu kama ukizijua unakua hauna haja ya kuhangaika kusoma maelfu ya vitabu).

Mfano ukisoma vitabu vya injili. Unakua ume-master masuala yote ya spiritual awakening, consciousnesss enlightenment, higher dimension, manifestation etc. Terminology kibao ila kitu ni kile kile.
Kikubwa ni Kuwa positive na kujiAMINI

Kua positive ni sawa sawa na kua mtakatifu (kuto kutendaa dhambi).

Mja ya watu waliokua katika viwango vya juu vya kiroho ni YESU alikua na mind yenye positivity ya hali ya juu kiasi kwamba ukimkosea haumii kabisa badala yake anakusikitikia wewe naamu yaani anakuonea huruma maana anakuona unavibrate katika frequency ya chini mno. Mtu mwenye dhambi au mwenye negativity nyingi katika mind yake... Anakua ana vibrate katika low frequency tukisema tu sketch graph itasoma negative.

Note.
View attachment 3165805
Sasa Alishindwa nini kutumia Hiyo high frequency yake ili asiuwawe !? Mmesema ktk huu ulimwengu frequency huwa inatabia ya kulipa kile unacho kifanya ukiwa na frequency positive ktk performance utapata Matokeo hayo hayo the same ktk low frequency, kuna mtu akatolea mfano if ukiua mtu lazima na wewe utauwawa tu , je Yesu Ambaye mmemtaja kuwa Ndiye master of high frequency mbona aliuwawa je nayeye aliwahi kuuwa mtu !? Vipi kuhusu Baba yake gorge bush mbona alishawahi kuua watu wengi kupitia vita alipokuwa madarakani lakini yeye kafa Kifo cha kawaida Tu cha uzeeni , Which is which!?
 
Sasa Alishindwa nini kutumia Hiyo high frequency yake ili asiuwawe !? Mmesema ktk huu ulimwengu frequency huwa inatabia ya kulipa kile unacho kifanya ukiwa na frequency positive ktk performance utapata Matokeo hayo hayo the same ktk low frequency, kuna mtu akatolea mfano if ukiua mtu lazima na wewe utauwawa tu , je Yesu Ambaye mmemtaja kuwa Ndiye master of high frequency mbona aliuwawa je nayeye aliwahi kuuwa mtu !? Vipi kuhusu Baba yake gorge bush mbona alishawahi kuua watu wengi kupitia vita alipokuwa madarakani lakini yeye kafa Kifo cha kawaida Tu cha uzeeni , Which is which!?
Yashua Amashiach aliwasamehe kumbuka katika physical na spiritual Realm kitu ukisamehe kinakua clean,
Pia kumbuka Spiritual Realm ilimfufua kutoka wafu hivyo hakuna kisasi Ulimwengu wa Roho uliwalipa waliomuua sababu ya forgiveness!
 
Habari mkuu pm yako umefunga,

Naomba na Mimi unisaidie hzo materials
Natanguliza shukrani
Hawezi kukupa mtu pekee ambaye sio mchoyo wa material ni kiranga peke yake ila hao wengine ni ujuaji umewajaa,
Sana sana atakwambia hizi mambo sio za kumpa kila mtu mara hivi vitu ni vya siri sana, nonsense
 
Sasa Alishindwa nini kutumia Hiyo high frequency yake ili asiuwawe !? Mmesema ktk huu ulimwengu frequency huwa inatabia ya kulipa kile unacho kifanya ukiwa na frequency positive ktk performance utapata Matokeo hayo hayo the same ktk low frequency, kuna mtu akatolea mfano if ukiua mtu lazima na wewe utauwawa tu , je Yesu Ambaye mmemtaja kuwa Ndiye master of high frequency mbona aliuwawa je nayeye aliwahi kuuwa mtu !? Vipi kuhusu Baba yake gorge bush mbona alishawahi kuua watu wengi kupitia vita alipokuwa madarakani lakini yeye kafa Kifo cha kawaida Tu cha uzeeni , Which is which!?
Masuala ya kiroho mara nyingi huwa yanaenda kinyume na mantiki, jambo linakosa logic kabisa mpaka linakuja kutimia ndio unapata maana na picha kamili... Muda mwingine hata likitimia kama unaufahamu mdogo bado huwezi kuelewa mpaka watokee walimu/watu wenye hekima na hayo mambo au manabii, wayatolee ufafanuzi.

Kuhusu hili la Yesu;
Hiyo ilikua ni sehemu ya mchakato... Ili kufikia kusudi, sometimes shetani au watu wabaya anahusisha bila wao kujijua ili husudi/unabii udhililike na kufikia malengo.

Ukisoma Habari mbalimbali katika Biblia utagundua Mungu alikua anajidhihilisha katika mazingira ya ajabu na kwa watu wadhaifu/wenye kasoro au low status katika jamii.

Mfano. Kina Musa, YUSUFU, Daudi,
 
Sasa Alishindwa nini kutumia Hiyo high frequency yake ili asiuwawe !? Mmesema ktk huu ulimwengu frequency huwa inatabia ya kulipa kile unacho kifanya ukiwa na frequency positive ktk performance utapata Matokeo hayo hayo the same ktk low frequency, kuna mtu akatolea mfano if ukiua mtu lazima na wewe utauwawa tu , je Yesu Ambaye mmemtaja kuwa Ndiye master of high frequency mbona aliuwawa je nayeye aliwahi kuuwa mtu !? Vipi kuhusu Baba yake gorge bush mbona alishawahi kuua watu wengi kupitia vita alipokuwa madarakani lakini yeye kafa Kifo cha kawaida Tu cha uzeeni , Which is which!?
Mkuu naongezea nyama kidogo.

Mkuu ukikutana na Habari inayohusu imani hasa kutoka katika vitabu vya kiimani... Basi hauna budi kuwa ni mitizamo/uelewa wa namna mbili.

Mtizamo wa kiroho na mtizamo wa mazingira ya kawaida haya.

Ile Habari ya kuuwawa kwa Yesu kwa mtizamo wa mazingira ya kimwili ni unaona kuwa katika historia kulitokea mwamba mmoja alisurubiwa na kuuwawa baadae akafufuka.

Sasa ukija katika mitazamo au uelewa wa kiroho na ndio uhalisia ulivyo ile habari ya Yesu halikuwa tukio tu bali lilikua ni tukio linalowakilisha kufa kwa mwili wa kale na kuzaliwa upya ukiwa msafi, na tukio lile lilikuwa halimuhusu yeye Yesu bali ilikuwa ni kielelezo/demo kutelekeza sisi wanadamu kwa vitendo kuwa hivi ndio inatakiwa mambo yaende, kama tunataka kumfuata.

"yaani jikane wewe mwenyewe harafu beba msalaba wako umfuate" aloo yaani Acha mambo ya zamani, Acha ku vibrate katika low frequency (kiburi chuki ego fikra hasi nk... Bali inatakiwa uvibrate katika higher frequency (upendo amani shukrani fikra chanya nk).

Unaweza ukaona ni jambo rahisi hivi ndio mpaka asurubiwe si angetuambia tu... Aisee Kuokoka kwa wale watu wa dini na enlightenment kwa ma-open minded people. Ni mtiti ni jambo nzito... Yaani kuivunja ego ya mtu akawa hana ego, kumfanya mtu kajishusha mpaka chini kabisa tena kwa mahasimu zake na kutubu/kuomba radhi /msamaha kwa hiyari yake mwenyewe sio hivyo tu kuwa na nidhamu, na hayo mambo yote yawe na muendelezo (discipline na consistency)

Hapa kwenye ego hapa panachangamoto... Ego ni instinct ambayo tumeumbiwa nayo na inatufelisha sana watu wengi, si kwamba ni mbaya Hapana ila tunashidwa kuitumia kwa usahihi katika kubalance mambo tukiwa tunajamiiana sisi wanadamu(Emotions Intelligence (EQ)).

[ Kiranga amani iwe nawe mkuu]
 
Duuh
Hawezi kukupa mtu pekee ambaye sio mchoyo wa material ni kiranga peke yake ila hao wengine ni ujuaji umewajaa,
Sana sana atakwambia hizi mambo sio za kumpa kila mtu mara hivi vitu ni vya siri sana, nonsense
Duuh... Kama ni kweli basi jamaa atakupa tofauti na tumfiriavyo. Hzo mambo sio za Kila mtu sawa ila in terms of understanding.....
 
Najua sana, ila huwa nakua makini kuzungumza ovyo ovyo kwani si kila mtu anaweza kuelewa hasa hizi zama ambazo kila mtu anajifanya mjuaji. Kumbuka usemi wa Mastermind mkuu Yesu Kristo kuwa,"Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua".
Asiyejua maana haambiwi maana, achana nao hao!
 
Waliokimbia shule mambo ya physics yakijirudia lazima watoke nduki.

Anyway Wacha namimi niongeze vijipoint.

Iko hivi, mtu kaumbwa akiwa na nishati(Roho) ambayo iliingia ndani ya mwili ulipokuwa tumboni mwa mama yako na kuunda kiumbe mpya (Nafsi) ambaye ndie wewe mtu kamili.

Sasa wewe mtu kamili kwa kuwa umeumbwa kwa nishati iliyopo ndani yako, hivyo kama mjuavyo nishati inatabia ya kuatract na ku-disatract positive&negative charge inategemea na wewe kwa wakati huo upo ktk masafa ya energy za aina ipi.

Kila mtu ana energy ambayo huwezi kuiona kwa macho ya kawaida, lkn ipo,

Mfano ukiwa ktk energy ya positive charge kwenye matembezi yako na ukakutana na mtu mwenye positive charge the same to yours, hapa nadhani hata pyhsics haiapply Ile law of magnetism inayo state as alike charge repel, different/unlike charge attract, kwa upande huu ni tofauti, yaani utavuta nishati unayofanana nayo hapa ukikutana na mtu mwenye Charge inayofanana na yako lazima mtaendana kwa mood zenu, reaction zenu na response zenu ktk maongezi, body signs.

Ndiomana hata wale motivation speaker huwafundisha zile kanuni za law of attraction ama nguvu ya USUMAKU za kuvuta vitu unavyovipendelea kwa kuwekeza nguvu zako na akili zako ktk mawimbi sawa na vile vitu uvitakavyo.

Iko hivyo Kila kiumbe kina energy ya USUMAKU na pia umeme kiujumla, na Kila kiumbe kinaweza kudaka mawimbi sawa na kiumbe kingine, ndiomana Kuna muda hutokea, unammiss mtu Fulani ukitaka kumtafuta kwa simu ghafla anakutafuta na kukupa habari kama yako kuwa alikukumbuka, hiyo inaonesha wote mlikuwa ktk state ya mawimbi sawa, yaani akili zenu zilikuwa ktk frequency Moja kwenye mawimbi.

Na ifahamike kuwa kwa Kila kitu ufanyacho ujue kinabeba mawimbi yako na kinahusisha energy yako, iwe tendo jema&baya, ama iwe maongezi mema au mabaya ujuwe yanakuwa ktk mawimbi energy yako ivyo ni rahisi kwa viumbe wengine kukufikia kupitia mawimbi ya energy yako uliyonayo kwa wakati huo iwe matendo/maneno/mood yako na matamanio yako.

Kiumbe yeyote asiye na mwili(Roho) anauwezo wa kuisoma energy yako ndiyo itaamua kama anauwezo wa kukumudu ama vipi.

Ndiomaana huwa tunapinga sana hizi stories za kusadikika hasa kutoka kwa walokole na wafia dini wanaosema Kila jambo baya limetendwa kwa ushirikina/uchawi/shetan, hii si kweli, msababishi mkuu wa maovu dunian ni binadamu mwenyewe kwa kufungua Izo Channel za kusafirisha bad energies ktk maisha ya uhalisia.

Mchawi hawezi kukudhuru bila kupata sababu kwako, hawezi kukuloga bila kupata upenyo/mlango wa matendo yako.

Pepo hawezi kukuvamia bila sababu, na hii iwaendee wale walokole wanaodai watu huanguka makanisani sababu ya mapepo, acheni utani jmn hivyo viumbe havifanyi kazi kwa namna mnayoidhania, na pengine watu wenye mapepo ni wale tunaowaamini watusaidie kiroho, hao ndio ambao hupagawa na mapepo, kwa sababu maalumu ya kupotosha jamii.

Hao wanaodondoka makanisani na wengine kuleta stories za ajabu ajabu hao wote ni wagonjwa wa akili yaani waliologwa akili ama kiufupi waliopagawa na nguvu za Pepo ambao wameletwa na hao viongozi wenu wa kidini kwa kujua ama kutokujua.

Pepo hawezi kukuingia bila sababu za msingi, mchawi hawezi kukuloga bila sababu ya msingi, inaweza kuwa sababu ya kipumbavu kiuhalisia lkn kwake ni sababu ya msingi.

Yaani mshirikina/Pepo ili akuvamie lazima muwe ktk hali Moja ya charge, yaani kama hukuwa na doa lolote la kuatract energy ya Pepo ama kufungua channel ya energy ktk mwili wako huwezi kulogwa hata mchawi wa aina gani hawezi kukufanya lolote, isipokuwa kunafanyika jambo la kukufanya uendane na frequency zao ama ufanye jambo lolote la kufungua mlango wa energy ktk utu wako ndipo unapovamiwa, either kupitia watu wengine ambao wanaweza kukuletea ugomvi, hasira, ama matamanio yako hasa tamaa mbaya.

Niishie hapa, kiufupi hii elimu ni kubwa sana lkn ndio hivyo watu wengi hawana sababu viongozi wao wa kidini wamebase kwenye mafundisho mepesi yasiyohitaji akili, yaani mmebaki kufundishwa Kila siku mambo Yale Yale na stories zile zile kumbe Kuna mambo mengi ya msingi ambayo watu ilitakiwa wayajue.
Vipi kwa wale wanaoshinda usiku wa manane,wakiangalia porn kwa vifaa vyao vya kielekronic na mwishowe kuishia kujichua/punyeto.

Ni kwa kiasi hii inaweza kumuhathiri mhusika?
 
Yesu Kristo ndio Master of masters ndio maana anaitwa Lord of Lords Mfalme wa wafalme yeye ndie Binadamu na kiumbe pekee aliyefika rank za mwisho za Consciousness na kiumbe yeyote anayefikia hapo Uungu unamvaa 💯%
Na anakua kwenye Eternity yaani Alfa na Omega au non of existence beyond limitations,
Hii siri ukiijua na ukaelewa hutaastajabu kwanini Yashua Amashiach alisema
Mimi na Baba ni wamoja (Baba ni kiwakilishi cha Supreme power)

Pia kuna nukuu anasema yeye ndie njia ya kweli na uzima (means mtu yeyote atakaye fuata njia yake yaani kua Consciousness 💯% ataingia kwenye Eternity na kwenye Eternity hakuna wingi kila kitu kinakua the one)

Pia kuna andiko anasema "mimi ndie njia ya kweli na uzima"
(Means mtu ukimfuata yeye ile njia ya kua Consciousness itakufanya kufika level zake na kua mmoja pamoja naye yaani eternity)

Sasa watu wengi hatujui siri za Uungu that's why code hizi zinatupiga chenga na kutufanya kua week endapo mtu akipata hata nusu ya Haya maarifa atafanya miujiza mikubwa sana!
Ina maana basi hatupaswi kumuabudu bali tunapaswa kufanya alivyofanya nasi tufikie level yake ya uungu
 
Back
Top Bottom