Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Fungua na wewe kampuni...



...Ni Hayo Tu!
 
Ukitaka kuwa tajiri we wakandamize watu
Wote wakina wakina baresa day waka zao wanalalia

Ova
 
Ugonjwa wa UCHAWA umekufikia.
 
MO halipi watu 4,000

MO ametoa tenda kwa makampuni binafsi ambayo yanajishughulisha na kutoa vibarua kwa watu.

Kwa mfano hapo Vingunguti kwenye viwanda vya MO kuna kampuni linaitwa UPAMI.

Hili kampuni limechukua tenda kwa MO, maana yake MO kafanya makubaliano na hilo kampuni na kulilipa kiasi ambacho wamekubaliana, halafu hilo kampuni linaajiri vibarua ambao linawalipa 4,000.

Kwa hiyo hapo wakulaumiwa sio MO ni hilo kampuni. Kwasababu waajiriwa rasmi huwezi kusikia wanalipwa kiwango hicho.
 
Kulipo kulipa mtu Dar 4000 ni bora anunue tu mashine tujue watu hawana ajira...huo ni Utumwa na ndio chanzo cha umaskini, watu wana relax kwa kazi za elfu nne hawajui zinaishia kwenye nauli na chakula cha mchana tu...bora waende vijijini wakalime.
 
Ila Mo anauwezo wa kucontrol hao watu walipwe shingapi kulingana na hela anayo mlipa contractor wake, haiwezekani contractor alipwe kila kichwa 12k yeye akawape 4k, bila kupepesa macho Mo atakua anawalipa 5k tu kwa kichwa
 
Hakuna jipya mkuu zaidi ya unafiki tu sababu ni Mo ila Unaweza kuta mleta mada wewe ni shahidi maana umeshuhidia beki tatu wenu akiwalea kwa mshahara wa elfu hamsini kwa mwezi.
 
Fuatilia kwa kina mkuu, Hiyo elfu4 ni kwa kazi gani?

Lakini pia ni masaa mangapi kwa siku, usikute kazi ni masaa6 tu kwa siku ili na wengine wapate.
 
Ni yale yale tu.
 
hili suala sio kwamba lipo kimfumo zaidi?

kwamba kwa vile tanzania ni nchi maskini sana MeTL haiwezi kumudu kulipa vibarua vizuri, ikifanya hivyo bidhaa zitakuwa na bei kubwa halafu hazitoweza kushindana kwenye soko(ambalo pia ni la watu wenye kipato kidogo sana cha matumizi)

hivi hamna mwanauchumi huku kweli atufafanulie?
 
Hakuna jipya mkuu zaidi ya unafiki tu sababu ni Mo ila Unaweza kuta mleta mada wewe ni shahidi maana umeshuhidia beki tatu wenu akiwalea kwa mshahara wa elfu hamsini kwa mwezi.
Angefanya nini kama mtoto??
Halafu hata kama ingekuwa kweli 50,000 kwa mwezi ni sawa na 1700 kwa siku, beki tatu halipi nauli ya usafiri, anakula na kulala hapo anapofanyia kazi, akiumwa anatibwa na mwajiri, wengine wanajiongoza wanajifunza cherehani, hotel skills au urembo wakiwa hapo hapo kwa mwajiri wao. Hii ni zaidi ya 4000 kwa siku japo bado ni duni.
 
1. Huyo naye ni Mtanzania kama Watanzania wengine!
2. Siyo vizuri kumkosoa ikiwa wewe hujaweza kufanya vizuri zaidi yake. Kama unawalipa wafanyakazi wako shilingi elfu tano kwa siku, basi utakuwa na uhalali wa kumkosoa anayelipa upungufu ya elfu tano
3. Wanaoenda kufanya kazi kwake ni watoto? Kama ni watu wazima na hawajalazimishwa, acha waendelee kufanya. Hiyo 4,000 inawasaidia kwa namna moja au nyingine
 
Sio elf 4000 Bwana ni elf 7500, ambayo unakatwa 1500 chakula cha mchana na unapata 6000 ambayo unaichukua kwa wiki, elf 36, ambayo ukipiga kwa mwezi ni Sh. 144000/=, Muda wa kuingia ni saa 1:30 asubh, muda wa kutoka ni saa 11 jioni, Kuna overtime ukitaka sh. 500 kwa kila saa moja utayoongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…