Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Inategemea na kitengo mbona hapa kwa Mo kuna watu wanapiga 15,000 per day

Tena hawa ni wale wanaohakiki mizigo na kuandika ripoti

Hapa nazungumzia wale ambao wanakuwa ndani kusaidia mashine (kuna jina lao la kiufundi nimelisahau) hawa ndio wengi.
Yes hao wa mizigo wanakula hela angalau, na wanakuwaga na nyodo hatari
 
12 na hamna overtime..na kazi za wahindi hamnaga kupumzika..hata kama hamna kazi atawapa fagio mkafagie lami hawajisikii vizuri wakiona watu wamekaa tu.
Mkuu kama wanalipa 4,000/=kwa 12 hours ni dhuruma kubwa sana wanaifanya.

Na wanafanya hivyo kwasababu tu wananchi ni masikini hawajui wakale wapi, so sad!
 
Ndiyo sasa tutamuelewa Nyerere alipokuwa anahimiza uzalendo kwenye viwanda vya umma
Kwamba Nyerere angelipa Laki nne kwa siku ?

Si maviwanda yalimfia akiwa madarakani mpaka akaanza kulialia au unafikiri mchonga meno aling'atuka kwa kupenda ???
 
Nyie ndio hata mkiitwa nyani na wazungu mnabaki mnachekacheka kwakua ni matajiri Sasa Mimi huo ukondoo naukataa aiwezekani watanzania wenzetu wateswe kama GABACHORI kashindwa biashara afunge kampuni kabla sijawa rais
Pumbavu
 
Huyu anatesa sana Watanzania imagine.

Leo nimepita sehemu mada ni kwamba jamaa kiwandani kwake hapa Dar es Salaam analipa 4000 yaani buku nne

Hivi wadau hii ni kazi au mateso na unakuta mtu anaamka asubuhi anaenda kuifanya aisee Mimi siwezi fanya huu ujinga
Ndio hivyo wewe ulitaka alipe ngapi? Jenga kiwanda chako uwalipe 50,000 na uzuri hakuna anaelazimishwa.

Mwisho Huwa nawashangaa sana mnaposemaga vijengwe viwanda vingi watu wapate Ajira wakati kiuhalisia machine ndio zinafanya kazi Kwa wingi lakini hata pale wanahitajila watu Huwa wanaliowa ujira mdogo sana na ndio chanzo Cha siku ya wafanyakazi Duniani baada ya migomo ya wafanyakazi Wa viwandani Toka miaka hiyo huko Ulaya.
 
Mkuu ni sawa kulingana na hali halisi nchini, Viwanda vingi vinalipa 5,000/= hadi 10,000/= kwa siku.

just Imagine 160,000/= sawa na 5,300/= kwa siku au 230,000/= sawa na 7,666/= kwa siku, ni wachache sana wanaochukua zaidi ya 300,000/= kwa mwezi humu kwenye viwanda.

Wanajificha chini ya mwamvuli wa kutoa baadhi ya huduma bure kwa wafanyakazi mfano malazi, maji au umeme na kivuli cha kupunguza masaa ya kazi kwa siku eti masaa8 kwa siku.

Viwanda vinanyonya sana mkuu, kama umeajiriwa sehemu nzuri au umejiajiri shukuru kwa hilo.
Basi awalipe hata 10,000. Hiyo 4,000 sawa kabisa hata kama ndio tuko kwenye soko huria, ni malipo ya udhalilishaji.
 
Sikati kazi, au kufundisha watu kuchagua kazi. Ni uhakika unaongea usichokijua. Ni basi umasikini tu na vijana tunaumia sana sababu ya usimamizi mbovu sana wa serikali yetu.

Sikia mule kwenye ivyo viwanda vya vya MO na bahatesa ni JEHANAMU. Huwezi kunielewa sababu itakuwa hujawahi kubeba hata tofauli wewe.

Bahati nzuri nishawahi kupita kwenye ivyo viwanda vya baharesa na MO buguruni na extetnal..

Wewe nina uhakika wa 100% hujawahi beba hata kiroba hatuwezi ongea lugha moja. Mtoa mada yuko sahihi sana.
Hizo kazi nimefanya naelewa maumivu yako lakini sekta ya viwanda kwetu bado ipo chini sana.

Hata ujira mkubwa ni jambo gumu kweli viwanda vyenyewe maboss wanavyoendesha wakikusimulia unaweza usiamini.

Nchi yetu ina sera za kipuuzi sana hata mpango wa kukuza pato la Mtanzania serikali yetu haina tupo poor sana kwa kila kitu.
 
Sawa.

Lakini naona hujaelewa hoja yangu.

Soma mission statement ya "The Giving Pledge".

"The Giving Pledge is a promise by the world's wealthiest individuals and families to dedicate the majority of their wealth to charitable causes."

Mo Dewji amesaini The Giving Pledge kuwa atatoa sehemu kubwa ya hela zake kwa hiyari yake, buree, ziende kwenye charitable causes, kwa sababu anaamini katika falsafa ya kugawa sehemu kubwa ya utajiri wake kabla hajafa.

Ninashangaa inakuwaje mtu aliyetia saini "The Giving Pledge" kutoa hela zake kwa charitable causes, kwa msaada tu, anashindwa hata kuwalipa vizuri wafanyakazi waje?

Hizo hela ambazo angewalipa wafanyakazi wake kiuchumi wala hazikutakiwa kuongeza bei ya chochote, kwa sababu angeweza kuwapa bonus au mshahara ambao haujali sana market prices.

Kimsingi swali ni hili.

Kama una roho nzuri sana mpaka umeahidi kutoa dola bilioni moja kwa charitable causes mbalimbali, kwa nini usitumie dola milioni chache kati ya hizo kuwaongeza kidogo nishahara wafanyakazi wako wanaokuzalishia mali za biashara zako?

Mo Dewji kweli yuko serious kwenye hiyo giving pledge? Au anatuzuga tu?
Ni kweli sijajibu hoja yako, nimezungumzia mada kuu tu najua nikikuquote wewe hutojibu kwa mihemko

Kuhusu giving pledge bwana.... mimi nina mashaka nayo

Kuna uwezekano mkubwa ni njia ya billionaires kurithisha vizazi vyao mali bila milolongo, mfano kwa US nasikia ni njia ya kukwepa inheritance tax

Billionaires wanajifanya altruistic kufurahisha watu tu, ni kweli kabisa unayosema hapa. Wangetumia mali kusaidia watu

Umenikumbusha leo kuna video nimeangalia mtu anamkosoa bill gates, bills gates anasema; "It's so unjust to hold finite resources" wakati yeye yuko busy kukusanya mali

Mo dewji kahamia dubai kwenye mjengo wa $50M, angeweza kuwa na mjengo wa labda $3M halafu akalipa vibarua vizuri.... Una hoja.
 
Vibarua wanaofanya kazi Pepsi, Bonite, ASAS, Tanga Fresh na Azam wanalipwaje?
Kwa azam nilisoma thread humu inasema unalipwa 4000 ila lazima ule msosi, kwahiyo unakatwa 1500 unapokea 2500

Pia nilisoma eti minimum wage bongo ni 60000/mwezi. Sina uhakika
 
Yupo kijana aliyemaliza chuo ajira zikasitishwa, aliwaomba wenzake wamtafutie tu kibarua hata kama pesa itaishia kwenye nauli ili naye awe anatoka tu hapo nyumbani anarudi jioni. Ukiwa na uthubutu na huna kitu ondoka nyumbani kalipwe 4000 kwa siku huko huko utapata akili ya kitu kingine. Labda kama umeridhika na chakula cha anko au shemeji.
Upo sahihi hivyo ndivyo safari ya maisha inanzia hakuna namna ni kufight tu
 
Vibarua wanaofanya kazi Pepsi, Bonite, ASAS, Tanga Fresh na Azam wanalipwaje?
Pepsi na Cocacola mara nyingi ni Elfu6-8 kwasiku kulingana na mauzo ya kituo na kuchelewa kurudi depo.

Nilichosikitika cocacola watu wanne mnapakia gari1 zile Eicher mpaka ijae - sio kitoto ni kazi ya masaa2 ya nguvu, kisha gari inatoka na vijana wawili, hao vijana wanashusha katoni/Crate za soda vituo tofauti ila malipo ni elfu6 kwa sikuu.

Labda itokee gari tu imelala nje ya mkoa ndipo upewe elfu10 ya guest, ulale kwenye gari hiyo pesa usave - na hii hutokea mara moja moja.

Nimeongea kwa uchungu sana sababu nimewahi kuifanya hii kazi na hapo nilikua nalipwa elfu4 ila sasahivi elfu6.

ASAS analipa 100,000/= kwa mwezi mkuu, japo kula kwake na kulala kwake.

Tanga Fresh na Azam sina taharifa kuwahusu, lakini sidhani kama itakua kubwa zaidi.

Tanwat wanalipa 230,000/= kwa sasa na hapo kuna makato ya NSSF, KODI kama unaishi kwenye nyumba zao, Anayelipwa laki3 ni yule unakuta ana overtime nyingi.
 
Kwa level ya ubilionea wa Mo hata kumtumia contractor anayewalipa watu 4,000 ni scandal.

Mo anaenda kukaa vikao vya matajiri wa dunia kina Bill Gates hizi habari zikifika international media tayari ni bonge la scandal kwa Mo.

Yani ukiachilia mbali ethics, it's not good for the Dewji brand and business.
Ni kwa vile bongo hatuna wapiga kelele wakubwa wa haya masuala wanaoweza kusikika kimataifa, kweli ingekuwa skendo kubwa sana huko nje ingesikika Mo analipa $1.5 per day.
 
Back
Top Bottom