Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Huyu anatesa sana Watanzania imagine.

Leo nimepita sehemu mada ni kwamba jamaa kiwandani kwake hapa Dar es Salaam analipa 4000 yaani buku nne

Hivi wadau hii ni kazi au mateso na unakuta mtu anaamka asubuhi anaenda kuifanya aisee Mimi siwezi fanya huu ujinga
Kuna ubaya gani hapo 4000x28 =112,000?
 
Huyu anatesa sana Watanzania imagine.

Leo nimepita sehemu mada ni kwamba jamaa kiwandani kwake hapa Dar es Salaam analipa 4000 yaani buku nne

Hivi wadau hii ni kazi au mateso na unakuta mtu anaamka asubuhi anaenda kuifanya aisee Mimi siwezi fanya huu ujinga
Kama huwezi kufanya huu ujinga kauze uduvi uolewe. Kwa sauti ya mkuu wa mkoa Chalamila 31.12.24
 
Huyo tunaweza kumpa udhuru ni mama lishe, lakini pia wafanyakazi wake wanakula hapo na wateja wengine wanaacha chenji au wanahonga. Mo kulipa kiwango sawa cha ujira na mama Lishe mdogo sio sawa hata kidogo.
Siko hapa kumtetea mo ndio maana nimeomba mleta Uzi anitajie kiwanda kinacholipa 20k kwa siku. Nenda kwa barmaids ujue wanalipwa kiasi gani? Kifupi mtaani hali ni mbaya.
 
mkiambiwa kuwa ubaguzi umekithiri Tanzania mnakataa! Kulikuwa na haja gani ya kutaja uasili wake? Kwani yeye sio mtanzania kama wewe? Grow up wacha ubaguzi wa rangi! Kama unaona afanyalo ni kosa unahaki kulisema lakini sio kwa kutumia lugha za kibaguzi.
Acha atajwe mzee, Ndio ni Mhindi kwa huo Ujira aisee hapo ni kutafuta Maximum profit tu punda afe mzigo ufike, Na ivo Viwanda vya Hao wahindi ni very risk mzee hata regulatory Bodies za Safety sijui zinafanya kazi gani mtu hajali safety ya wafanyakazi bado ujira ni duni,
Bado tunamchekea tu
 
Kama hao hawana kazi ya kuwapa hata mia ,na wana kula hapo hapo na wamaeneo ya karibu na hapo kiwandani hiyo 4000 sio tatizo kwa kazi za kiwandani ila kama ni tofauti na hivyo ukue ni. Utumwa
 
10,000 kwa siku.
Angalau buku moja kwa lisaa, sasa hivi ni kama analima 400 kwa lisaa! Mpiga debe anayipga debe kwa dakika 10 tu anapewa 500 na konda.

Na hapo gari zinapita nyingi najaribi kuwaza ni 500 ngapi wanaingiza wapiga debe. Afadhali kuliko kushindankwa Mo siku nzima!
 
Wakati unamalumu Mo kulipa 4000,unaweza kutuambia wewe na familia yako mmetoa ajira ngapi kwa Watanzania hata za kuwalipa 2000 kwa siku?
Kwa taarifa tu kwako ndio muajiri mkuu katika sekta binafsi Tanzania na hiyo 4000 unay
oikandia binadamu wenzetu wanafanya maisha na kusomesha watoto zao.
Lastly naona damu ya kibaguzi imekujaa mwilini na kujiona wewe ndio Mtanzania zaidi kuliko Mo kisa rangi ya ngozi yako sio?
Acha upumbavu wako huwezi kumuacha mtu awanyanyase ndugu zako eti kisa ametoa ajira nyingi huko ni kunyonya watu na kuwatumia kama watumwa.
Kwenye hili serikali inatakiwa kubeba lawama huwezi kuwaachia matajiri wajiamulie wanavyotaka kisa wanalipa kodi ni lazima utanzania uheshimie na watanzania waheshimike kwenye kila sehemu hasa maeneo ya kazi.

Basi angalau wangesema kima cha chini kwa kazi za dayworker kiwe 10000 angalau.
Kama waajili wataona ni nyingi wawepe mikataba hao wafanyakazi japo ya miezi mitatu kwa hiyo mishahara ya kima cha chini nadhani ni laki na 90 kwa sasa..
 
Unafikiri kwa nini Serikali inakamata wauza dawa za kulevya? Kwa nini isiwaambie tu watu wasinunue??
Serikali hiyo hiyo pia imeweka sheria na miongozo mbali mbali ya kuwalinda hao wafanyakazi,unadhani msimamizi wa hizo sheria ni Mo Dewji?
Kima cha chini cha serikali kinafahamika na masaa ya kazi yanafahamika huyo mleta uzi ameleta thread ya kibaguzi na sio hoja ndio maana nimepinga hata yale ya msingi yaliyo katika thread uzi wake.
 
Acha upumbavu wako huwezi kumuacha mtu awanyanyase ndugu zako eti kisa ametoa ajira nyingi huko ni kunyonya watu na kuwatumia kama watumwa.
Kwenye hili serikali inatakiwa kubeba lawama huwezi kuwaachia matajiri wajiamulie wanavyotaka kisa wanalipa kodi ni lazima utanzania uheshimie na watanzania waheshimike kwenye kila sehemu hasa maeneo ya kazi.

Basi angalau wangesema kima cha chini kwa kazi za dayworker kiwe 10000 angalau.
Kama waajili wataona ni nyingi wawepe mikataba hao wafanyakazi japo ya miezi mitatu kwa hiyo mishahara ya kimacha chini nadhani ni laki na 90 kwa sasa..
Kwa namna hii siwezi kuacha upumbavu boss,shida sio Mo Dewji shida ni serikali yako hilo tunaweza jadili mimi na wewe boss...Labda tuanzie hapo hao unaowaita ndugu zako wewe umewapa mbadala upi wa kufanya maisha ambao ni bora zaidi? au unaimba tu humu ili uonekane na wewe Watanzania wote ni ndugu zako kinafiki?
 
Huyu anatesa sana Watanzania imagine.

Leo nimepita sehemu mada ni kwamba jamaa kiwandani kwake hapa Dar es Salaam analipa 4000 yaani buku nne

Hivi wadau hii ni kazi au mateso na unakuta mtu anaamka asubuhi anaenda kuifanya aisee Mimi siwezi fanya huu ujinga
Umechelewa kujua mkuu mbona kitambo sana,bakhresa ndo pekee analipa vizuri,ila kupata nafasi ngumu,ukibahatika unaweza ingia mara Moja,pale kipawa.
 
Huyu anatesa sana Watanzania imagine.

Leo nimepita sehemu mada ni kwamba jamaa kiwandani kwake hapa Dar es Salaam analipa 4000 yaani buku nne

Hivi wadau hii ni kazi au mateso na unakuta mtu anaamka asubuhi anaenda kuifanya aisee Mimi siwezi fanya huu ujinga

Waswahili wengi wao sio watu wa kazi, ni heri kuajiri wahindi au wachina hata mshahara utakayolipa itakua ni halali.

Najua kufanya kazi na wahindi ni changamoto japo sidhani kama ni wote wapo hivyo.
 
Huku kibarua cha kupanda mpunga kuanzia saa2 hadi saa9 ni 5000-7000 kula ni kwa mwenye shamba na ni msosi wa uhakika. hapo hakuna hela itatoka kwa ajiri ya usafiri yaani unafikisha home5000 ama 7000 nzima nzima.

Usitete unyonyaji na utumwa ili hali wenzetu wanaibwa kwani serkali ikisema atoe angalau15k atafunga hicho kiwanda kwa kushindwa kuwalipa hiyo hela? jibu ni hamna na pengine mo hajui watu wanalipwa vile ila alio waamini ndo wanafanya hivyo.

hata hivyo wahindi wako hivyo. Apingwe na mtu yeyote mwenye akili timamu
Kwa hiki kizazi cha wavivu wanaopenda maisha laini kinacholazimisha kuishi Dar es Salam umedhani rahisi kumshawishi enda shika jembe kwenye majaruba??
 
Kwa hiki kizazi cha wavivu wanaopenda maisha laini kinacholazimisha kuishi Dar es Salam umedhani rahisi kumshawishi enda shika jembe kwenye majaruba??
Isiwe kisingizio eti maisha laini wangekuwa wavivu kiasi hicho hata hiyo kazi wasingepeta mkuu.Tukemee kwa nguvu zote watu walipwe vizuri kulingana na kinachozalishwa asee
 
Back
Top Bottom