Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Yupo kijana aliyemaliza chuo ajira zikasitishwa, aliwaomba wenzake wamtafutie tu kibarua hata kama pesa itaishia kwenye nauli ili naye awe anatoka tu hapo nyumbani anarudi jioni. Ukiwa na uthubutu na huna kitu ondoka nyumbani kalipwe 4000 kwa siku huko huko utapata akili ya kitu kingine. Labda kama umeridhika na chakula cha anko au shemeji.
Kwa mwezi ni zaidi ya 100,000. Ni bora hiyo kuliko kutopata hata 100.
 
Matajiri karibu wote WA kiafrika Huwa ni wanyonyaji sana Kwa wafanyakazi wao!

Yaani Huwa wanafanya ile total exploitation of labor.

Na hii ni Kwa sababu ya ukosefu mkubwa wa ajira uliopo kwenye hizi nchi zetu ambapo watu wengi wako tayari kufanya kazi Kwa ujira wowote ule mradi wapate kula tu na sababu nyingine ni kutokuwepo Kwa mamlaka za usimamizi wa haki za wafanyakazi ambazo zingeweza kufanya kazi Kwa ufanisi.

Kiukweli kumlipa mtu 4,000/= Kwa siku haingiii akili hata kidogo hata kama kazi yake ni kukufutia vumbi tu ofisini.
 
Watanzania Acheni Ujuaji na unafiki kwani huko maofisini mtu anayelipwa laki 2 ukipiga hesabu kwa siku n sh ngapi?
Mabaamedi wanalipwa sh ngapi kwa siku? Wauza vyakula migahawani na mahotelini mnajua wanacholipwa?
Housegirl na Houseboy? Wanaouza maduka kkoo ya Wachaga na wakinga kwa siku unajua analipwa bei gani?
Issue sio MO ni mfumo wa Nchi nzima tu watu wananyonywa sana.
Wewe ni kajakazi wake sio unakuja hapa kumtetea
 
Huyu anatesa sana Watanzania imagine.

Leo nimepita sehemu mada ni kwamba jamaa kiwandani kwake hapa Dar es Salaam analipa 4000 yaani buku nne

Hivi wadau hii ni kazi au mateso na unakuta mtu anaamka asubuhi anaenda kuifanya aisee Mimi siwezi fanya huu ujinga
Tafuta hela umzidi afu uwalipe watu 1000000 kwa kutwa
 
Back
Top Bottom