Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

Paul Makonda, usikubali kusingiziwa na kuaibishwa, tunaomba tukuchangie hiyo Billion 1.2, ulipe kodi yao, makontena yatoke, kisha sambaza vifaa hivyo mbele ya waandishi wa habari, ili waliokusingizia kuwa unapiga deal's, waaibike.

Endelea kumtegemea Mungu, hata hili la makontena, litapita tuu kama upepo.

P
Mbele ya waandishi wa habari? Hizo sofa na vitanda?
 
Mbele ya waandishi wa habari? Hizo sofa na vitanda?
Tulionyeshwa pale containers zimefunguliwa zina viti, meza na ubao za kuandikia.

Ndio maana tumeshauri, tumchangie hiyo pesa, alipe kodi, tuvigawe vifaa hivyo huku media ikishuhudia, ili kuwaaibisha, waongo hawa, wazushi hawa, wapiga fitna na majungu dhidi ya mafanikio yake!.

P.
 
FINDINGS:
Huyu RC hata kama hana PhD asiitafute kwa kuwa imeonyesha hawa wenye hizi degree wameshindwa hata kusababisha maendeleo si tu kwa maandiko ya PhD zao bali hata kwao wenyewe. Sasa mfano mkubwa ni PhD holder anapokimbilia siasa katika nchi changa kama Tanzania na kuacha job creation, inaonesha hamna creativity and so big failure. Kuwa kiongozi wa kisiasa sio professionalism, it is about moral judgement and ethics. Hawa wasomi wetu hawana moral judgement and ethics. Example: Samani zipite, zitanufaisha wengi na tutapata leverage ya kodi. Kimsingi nchi ilipasa kupamtia RC comission kwa kufanya jambo kama hili na siyo kuhitaji tena kitu kidogo kuotka kwake. Yeye alishafanya homework yake. Sasa kila mtanzania akifanya jambo creative la kimaendeleo baada ya mwaka mmoja sisi ni first world ikiwa viongozi wote wangekuwa kama huyu RC na siyo kama hawa wengine..

Naomba kuwasilisha
Haya ni mawazo yako,lakini sheria inasemaje katika jambo hilo?
Watanzania wengi tunalaumu au kupongeza mambo kwa hisia tu!
Sheria ipo wazi,samani zote zinazotoka nje ya nchi lazima zitozwe kodi ili kulinda soko la samani za ndani!

Imetoa maelekezo vema,nani mwenye mamlaka ya kutoa msamaha wa kodi,anakuja mtu anaagiza samani,analazimisha zisilipiwe kodi pasipo kufuata sheria,na bado mtu anasimama hadharani kumtetea kwa kisingizio kwamba ni jambo la maendeleo!

Hivi kama wakuu wote wa mikoa,wakiomba misaada ya aina hiyo,(jambo ambalo linawezekana) wakataka kuingiza walivyosaidiwa kwa mtindo aliotaka kuulazimisha makonda,nini matokeo yake?

Bunge lilipoipitisha sheria ya kodi na kutuwekea utaratibu wa misamaha ya kodi hizo,haikuwa bahati mbaya.Tujifunze kutafiti mambo kabla ya kutoa lawama!

Hongera waziri wa fedha,Dr.Mpango,Hongera zaidi kwa Mh.Rais JPM kwa kuliweka sawa jambo hili,japo nikiliangalia kwa jicho la tatu,RC alivuka mipaka na kumdharau sana waziri wa fedha,hili halikupaswa kuachwa lipite!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulionyeshwa pale containers zimefunguliwa zina viti, meza na ubao za kuandikia.

Ndio maana tumeshauri, tumchangie hiyo pesa, alipe kodi, tuvigawe vifaa hivyo huku media ikishuhudia, ili kuwaaibisha, waongo hawa, wazushi hawa, wapiga fitna na majungu dhidi ya mafanikio yake!.

P.
Nakuelewa sana brother Pascal Mayalla,sanaaa!!!
Hahahaaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hata hii ya kuyazuia makontena yake na kutaka kuyapiga mnada, ni vivu tuu dhidi ya mafanikio yake!.

Jee endelee tuu kuwapuuza, or this time, awazingatie?.
P
Pascal mchambuzi ninayekuaminini ktk hili sakata la makonda na makontena umeteleleza sana sijui ni kwa bahati mbaya au kwa maslahi binafisi?

Bora iwe kwa bahati mbaya lakini isiwe kwa maslahi binafisi.

Unaweza kurudi na kurekebisha makosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal mchambuzi ninayekuaminini ktk hili sakata la makonda na makontena umeteleleza sana sijui ni kwa bahati mbaya au kwa maslahi binafisi?

Bora iwe kwa bahati mbaya lakini isiwe kwa maslahi binafisi.
Unaweza kurudi na kurekebisha makosa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Nyamnini,
Sijateleza niko right, ila kwenye hili sheria ndio imeteleza!. Likitokea jambo ambalo sheria imeteleza, japo sheria ndio itafuatwa, but it's not necessarily ndio iko right!.

Kuna wanaoangalia tuu sheria inasemaje, na kuna akina sisi tunaoangalia logic, kwenye hili la makontena ya Makonda, assuming yote ni ya vifaa kweli vya shule, then hakuna logic kuyatoza kodi!.

Nchi yetu ni masikini wa kutupwa, shule zetu hazina vifaa vya kutosha, serikali yetu haina uwezo wa kutosheleza mahitaji yote!. Wamejitokeza wasamaria, wamejitolea vifaa vya bure, vyenye thamani ya mabilioni, wewe unavitoza kodi ya 1.2 na kuvipiga mnada ili upate hiyo 1.2 ya kodi!. Halafu unakuja kutumia 20 billions kununulia vifaa kama vile vile!.

Mkuu,zama hizi paskal amebadiri mbinu anaandika kwa kuanzia kulia kwenda kushoto,ili kuunga mkono juhudi.

Na ikumbukwe ilisha semwa na jiwe kua yeyote anaepingana na bashite ni mpiga dili na sio mzalendo.acheni kumuonea wivu mkamata madawa ya kulevya au na nyie ni wauza madawa ya kulevya?[emoji16] [emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Nyamnini,
Sijateleza niko right, ila kwenye hili sheria ndio imeteleza!. Likitokea jambo ambalo sheria imeteleza, japo sheria ndio itafuatwa, but it's not necessarily ndio iko right!.

Kuna wanaoangalia tuu sheria inasemaje, na kuna akina sisi tunaoangalia logic, kwenye hili la makontena ya Makonda, assuming yote ni ya vifaa kweli vya shule, then hakuna logic kuyatoza kodi!.

Nchi yetu ni masikini wa kutupwa, shule zetu hazina vifaa vya kutosha, serikali yetu haina uwezo wa kutosheleza mahitaji yote!. Wamejitokeza wasamaria, wamejitolea vifaa vya bure, vyenye thamani ya mabilioni, wewe unavitoza kodi ya 1.2 na kuvipiga mnada ili upate hiyo 1.2 ya kodi!. Halafu unakuja kutumia 20 billions kununulia vifaa kama vile vile!.

P.
Kweli haileti maana kabisa, Mh Pascal Mayalla hii sheria ibadilishwe, huu uonevu wa kulipishana KODI wakati tunapenda kufanya misaada lukuki uishe kabisa, badiliko la sheria litaleta unafuu kwa sisi wenye roho nzuri km Makonda kuweza kuleta misaada na kuendesha taifa letu kizalendo zaidi, nakuunga mkono mheshimiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa huyu bwana...unalipwa uandike, mwingine akitoa dau unabadili msimamo unaanza kutetea huko. Tumbo bwana
 
Paschal Mayala tuhuma hazikanushwi kwa kukaa kmya. Viongozi wangekuwa wanatuhumiwa wanakaa kimya tungepata taifa gani. Kama unataka kujikomba bora mpe makonda amuoe binti yako ujikombe vizuri kuliko kuja hapa kupotosha mambo ambayo yanatufanya tushindwe kuelewa weledi unaojipanua nao kila siku ni upi.

Mkuu hapo you have crossed the line. Let’s learn to argue bila kejeli
 
Back
Top Bottom