Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

hata huyu bloger, Robert Alai Onyango -
ni muongo tuu, ni mzushi, na anamuonea wivu kwa mafanikio yake, ndio maana anamzushia!, naye pia apuuzwe tuu, kama walivyopuuzwa, wale waliomzushia amefoji vyeti!. Uzushi pia nao ni kama upepo, nao utapita tuu!.

P.
 
hata huyu bloger, Robert Alai Onyango -
ni muongo tuu, ni mzushi, na anamuonea wivu kwa mafanikio yake, ndio maana anamzushia!, naye pia apuuzwe tuu, kama walivyopuuzwa, wale waliomzushia amefoji vyeti!. Uzushi pia nao ni kama upepo, nao utapita tuu!.

P.
Kwa hiyo alikuonyesha vyeti vyako wewe tu? Na kama una ushaidi kwa nini usivilete hapa tuvione kama mwandishi wa habari mwenye kwenda na ushaidi au vielelezo vya habari. Maana yeye alishindwa kuvionyesha ila wewe kama mwandishi wa habari mwenye kuhabarisha kwa vielelezo tupe hizo habari vinginevyo na wewe utakuwa fake na mwandishi wa kuandika kwa miemuko
 
Kwa hiyo alikuonyesha vyeti vyako wewe tu? Na kama una ushaidi kwa nini usivilete hapa tuvione kama mwandishi wa habari mwenye kwenda na ushaidi au vielelezo vya habari. Maana yeye alishindwa kuvionyesha ila wewe kama mwandishi wa habari mwenye kuhabarisha kwa vielelezo tupe hizo habari vinginevyo na wewe utakuwa fake na mwandishi wa kuandika kwa miemuko
Kuna sheria yoyote, taratibu na kanuni inayomtaka mwajiriwa yoyote kuonyesha vyeti vyake kwa mwandishi wa habari?.

Vyeti vyake viko kwa mamlaka yake ya ajira. Kama mwajiri wake amejiridhisha, who are you kuhoji?.

Mwandishi fake ni yule ambaye siye, mimi ndiye!. Ila mwandishi anaweza kuwa mwandishi kweli lakini akaandika fake news. Hii sio fake news.
P.
 
Wanabodi.

Naanza na kanuni ya haki duniani "presumption of innocence until proven guilty" Yaani mtuhumiwa yoyote anahesabiwa kuwa hana hatia hadi atakapotiwa hatiani, hivyo Paul Christian Makonda anaendelea kuwa ni Paul Christian Makonda na Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mpaka itakapo thibitishwa, without any reasonable doubt kuwa Paul Christian ni mtu mwingine, na Daudi Albert Bashite ni kweli alifeli na kupata sifuri, akaiba jina na vyeti vya Paul Christian na kuvitumia kujiendeleza as if yeye ni Paul Christian hivyo ni kweli huyu Paul Christian Makonda, Mkuu wa Mkoa ni fake na mtu halisi ni Daudi Albert Bashite.

Declaration of interest, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu kwenye hii fani hivyo kuweza Kufanya habari yoyote ya kiuchunguzi, ila nimeamua kujikita katika kuandika habari za kimaendeleo, "developmental news" habari zenye maslahi na impact kwa maendeleo ya taifa. Hivyo siwezi kufutilia habari yoyote ambayo haina maslahi chanya kwa taifa, hivyo hapa nitatoa maelekezo namna ya kupata uthibitisho wa uzushi na uongo huu unaoenezwa kumhusu Makonda kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite, na kuwa ameiba jina baada ya kufeli shule, na ame foji vyeti na kujiendeleza.

Tangu kuibuka kwa Tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kughushi vyeti, savers za JF zimezidi kujazwa kwa ma thread na mathread kuhusu sakata hili.

Hata mimi niliwahi kumshinikiza Makonda ajitokeze kukanusha kwa hoja kuwa Uongo ulisemwa sana, bila kukanushwa mwishowe kugeuka kuwa ni ukweli.
Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Sasa nimebadili msimamo baada ya kugundua kuwa, uongo siku zote utabaki kuwa ni uongo tuu hata ukisemwa vipi au mara ngapi, hauwezi hata siku moja kugeuka ni ukweli.

Na ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli tuu hata usiposemwa. Ukituhumiwa kwa tuhuma zozote za uongo au kuzushiwa jambo baya lolote, as long as unajua ni uongo, huna haja ya kukanusha, wewe jinyamazie tuu kimya, ule msemo wa "tell the truth and the truth will set you free" ni msemo wa uongo, kanuni yangu ni "just keep silent about the truth, and the truth will remain the truth".


Uthibitisho kuwa tuhuma hizi ni uzushi, ni huu ukweli bayana uliopo mbele yetu hadi sasa kuwa Mhe. Paul Christian Makondo ni mteule wa rais wa JMT aliyefanyiwa vetting na vyombo husika na kuthibitisha pasipo shaka wasifu wake hivyo akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mpaka sasa hapa tunavyozungunza, Paul Christian Makonda, ndiye Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, na huu ndio ukweli bayana na ukweli halisi uliopo, mkubali, mkatae, ukweli unabaki kuwa ukweli, mengine yote ni uzushi tuu!.

Jee wewe Mtanzania mwenzangu, kati ya wazushi hawa wanaomzushia Makonda kuwa ana jina la bandia na vyeti vya kughushi, na rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyemwamini Makonda hadi kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na kuendelea kumwani mpaka hii leo, licha ya kuibuka kwa tuhuma hii, unamwamini nani kati ya wazushi na rais wako?.

Kwa maoni yangu Mkweli ni Rais wa JMT, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, kwa sababu tangu kuibuka kwa tuhuma hii, serikali kupitia vyombo vyake, ingeishafanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki.

Anne Kilango alipodangwanywa tuu, alitumbuliwa pale pale!. Kitwaga alipopata kidogo tuu pale Bungeni, alitumbuliwa pale pale lakini kitendo cha Paul Makonda, hadi dakika hii, bado ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwangu ni uthibitisho tosha kuwa tuhuma hizi ni za uongo, ni za uzushi, ni za kutunga na za kubuni, haiwezekani kabisa mteule wa rais Paul Christian Makonda akaiba jina, akafoji cheti!. Huu ni uzushi wa kupuuzwa kabisa na ndio maana hata Makonda mwenyewe amezipuuza, na Rais hajachukua hatua yoyote, na wala hata chukua hatua yoyote kwa sababu soon wengi mnaojua Kuwait Paul Makonda ndiye yule ambages... "Huyu ndiye mwanangu mpendwa wangu, ninaye pendezwa naye", hata akifanya nini, mtapiga tuu kelele za kujisumbua bure!, ndio maana mpaka sasa watu wametulia tuu na kuzipuuzia hizi kelele zote za kizushi huku wazushi wakiendelea kupiga kelele.

Wengi mliujua uwezo wa Makonda, alipoanza vita na wauza unga, sisi wengine, tuliujua uwezo wa Makonda toka akiwa DC na tulitoa ushauri ufuatao kwa Magufuli
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
Tena tumependekeza
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana ...

Watanzania tupunguze kushadadia uzushi, tujiunge na rais wetu kumtia moyo Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda endelea kuchapa kazi, na sisi wengine wote katika umoja wetu, tuwapuuze kabisa watu hawa wasiolitakia mema taifa letu.

Nawatakia Jumatano Njema ya Majivu, leo ni siku ya kufunga kwa sisi Wakristo Wakatoliki, tunaanza mfungo wa siku 40 za Kwaresma.
Kwaresma Njema
Paskali
Update.
huu pia ni uthibitisho wa jinsi watu walivyo waongo na wazushi kumhusu mtu huyu. Mkuu wetu wa Mkoa jina lake halisi na la ukweli ni Mhe. Paul Christian Makonda. Vyeti vyake viko kwenye mamlaka yake ya ajira ambayo sio hapa jf. Zile habari za Daudi Albert Bashite ni uongo wa mchana kweupe wala hakuna mtu kama huyo duniani, wala hakuna yoyote mwenye vyeti vya Bashite ulikuwa ni uongo tuu.

Mkuu wetu wa mkoa anaendelea kuchapa kazi za ujenzi wa taifa as if nothing has happened. Kelele za mlango hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi.

Paskali.
Running a Government is not like family matters in other words A Country is Not a Company
 
Vyeti ni sawa na kitambulisho chako ulichopewa na taasisi,kuna ugumu gani wa kuonyesha kitambulisho?
RC Makonda hapaswi kuogopa kuonyesha vyeti vyake,ndio maanake watu walio wengi wamemtilia shaka anavyotoa maelezo mengi yasioleta vyeti.
Paskali call a spade is spade not a big spoon,RC alitakiwa aonyeshe vyete,iwe leo au kesho,issue ni vyeti issue si u RC wake.
 
Huyu dogo kuna mambo anayafanya ni ya kipuuzi na mengine ni ya kibinadamu.

Jambo la kipuuzi ni kuvamia usiku ukiwa na wanajeshi wenye bunduki kwenye studio za Clouds.

Lingine la kijinga ni kumdhihaki mtu wa chini yake kwenye kikao cha hadharani mpaka jamaa akapandisha presha na kuanguka.

Yapo mema ya huyu dogo, Bunju B kulikuwa na mtendaji mmoja mpenda rushwa na alikuwa mpiga dili. Alishiriki katika kuwatapeli watu viwanja.

Siku mkutano ulipofanyika pale Mabwe mtendaji aliumbuliwa na kuondoka na landrover ya polisi, baadae akalipa pesa alizotapeli hao aliowauzia viwanja vilivyoshakuwa na umiliki wa watu wengine.

Dogo apunguze ulevi wa madaraka, dunia ilikuwa na watu ambao wakitembea hawataki kugusa ardhi, na watu wakalazimika kuwabeba ili wasichafuke lakini wapo ardhini kwa sasa.

Kuna tajiri kwenye mikoa ya pwani alikuwa hagusi chini anapotoka kwenye boti, wafanya kazi wake ndio waliolazimika kuloweshwa na maji ya bahari. Jamaa alikuja kufa baada ya kuteseka kwa sababu ya miguu yake kuoza.

Dogo ajifunze, bado hajafika hata miaka 40.
 
Mh. Mayala The time has come sasa ujikite zaidi kwenye kufahamu ukweli na uhalisia utakuwa muandishi mzuri sana. Nakushauri mtu akikwambia kwenye mkoba huu kuna maembe tafadhali omba kuyaona kama kweli ni maembe, usikubali tu kama kweli ni maembe, utajipambanua na naona mafanikio makubwa mbele yako
Mkuu Dharra, kwanza asante kwa ushauri. nimekuleta hapa kwa sababu, hapa niliwahi kuijibu hii hoja yako ya kuwa mwandishi mzuri. Kwa sasa nimeisha staafu newsroom, hivyo waandishi wenye muda wa kwenda kushuhudia idadi ya maembe ndani ya kikapu, kwetu sisi wastaafu, baada ya kikapu kufunguliwa, tumeonyeshwa maembe na tumeyaona, hivyo kuhalalisha kuyaandikia.
Wanabodi.
declaration of interest,
mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu kwenye hii fani hivyo kuweza kufanya habari yoyote ya kiuchunguzi, IJ, ila nimeamua kujikita katika kuandika habari za kimaendeleo, "developmental news" habari zenye maslahi na impact kwa maendeleo ya taifa. Hivyo siwezi kufutilia habari yoyote ambayo haina maslahi chanya kwa taifa, hivyo hapa nitatoa maelekezo

Paskali.
P.
 
FINDINGS:
Huyu RC hata kama hana PhD asiitafute kwa kuwa imeonyesha hawa wenye hizi degree wameshindwa hata kusababisha maendeleo si tu kwa maandiko ya PhD zao bali hata kwao wenyewe. Sasa mfano mkubwa ni PhD holder anapokimbilia siasa katika nchi changa kama Tanzania na kuacha job creation, inaonesha hamna creativity and so big failure. Kuwa kiongozi wa kisiasa sio professionalism, it is about moral judgement and ethics. Hawa wasomi wetu hawana moral judgement and ethics. Example: Samani zipite, zitanufaisha wengi na tutapata leverage ya kodi. Kimsingi nchi ilipasa kupamtia RC comission kwa kufanya jambo kama hili na siyo kuhitaji tena kitu kidogo kuotka kwake. Yeye alishafanya homework yake. Sasa kila mtanzania akifanya jambo creative la kimaendeleo baada ya mwaka mmoja sisi ni first world ikiwa viongozi wote wangekuwa kama huyu RC na siyo kama hawa wengine..

Naomba kuwasilisha
 
Nadhani hata hii ya kuyazuia makontena yake na kutaka kuyapiga mnada, ni vivu tuu dhidi ya mafanikio yake!.

Jee endelee tuu kuwapuuza, or this time, awazingatie?.
P
Mi naona this time azingatie tu alipe Kodi, maana nchi haijiendeshi bila kodi hii mkuu, awalipe tu kodi yao achukue makontena walimu wakakalie, kwan msamaha wa kodi ukikataliwa unapigana usamehewe au unaenda kutafuta chao,

Hapa naona ni Kaisari katunisha msuli anataka Hela yake, na makonda yeye ni mzalendo naona ili iwe uzalendo zaidi aingize tu hela kwenye kibubu cha TRA itatumika kwa maendeleo ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Yericko, sio kuamua kujilipua bali kuwa mkweli!.

P.
Ndugu mayalla and co.,
Kila siku naomba sana kwa Mwenyezi Mungu,muishi maisha marefu sana ili vizazi vijacho vikija uliza maswali,angalau muwepo na muweze kujibu maswali yao, mimi kama sitakuwepo ninahakika kaburi langu halitapigwa viboko,
Hayo tuu kwa sasa
Wasalaaam
 
FINDINGS:
Huyu RC hata kama hana PhD asiitafute kwa kuwa imeonyesha hawa wenye hizi degree wameshindwa hata kusababisha maendeleo si tu kwa maandiko ya PhD zao bali hata kwao wenyewe. Sasa mfano mkubwa ni PhD holder anapokimbilia siasa katika nchi changa kama Tanzania na kuacha job creation, inaonesha hamna creativity and so big failure. Kuwa kiongozi wa kisiasa sio professionalism, it is about moral judgement and ethics. Hawa wasomi wetu hawana moral judgement and ethics. Example: Samani zipite, zitanufaisha wengi na tutapata leverage ya kodi. Kimsingi nchi ilipasa kupamtia RC comission kwa kufanya jambo kama hili na siyo kuhitaji tena kitu kidogo kuotka kwake. Yeye alishafanya homework yake. Sasa kila mtanzania akifanya jambo creative la kimaendeleo baada ya mwaka mmoja sisi ni first world ikiwa viongozi wote wangekuwa kama huyu RC na siyo kama hawa wengine..

Naomba kuwasilisha
Mmh! Sheria ni sheria tuu na haitakiwi ibague. Kama ni sheria mbaya inatakiwa kubatilishwa kwa kufuata taratibu na kanuni. Ni hatari sana kuruhusu double standards. Lipa kodi stahiki kwa maendeleo ya Taifa.
 
Mmh! Sheria ni sheria tuu na haitakiwi ibague. Kama ni sheria mbaya inatakiwa kubatilishwa kwa kufuata taratibu na kanuni. Ni hatari sana kuruhusu double standards. Lipa kodi stahiki kwa maendeleo ya Taifa.
KODI, Kaisari anataka hela yake, sasa mteule anasema anaonewa kwa kuwa anataka kupitisha burebureeee, hii KODI hii KODII itamtoa mtu kwenye kiti chake cha kuzunguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hata hii ya kuyazuia makontena yake na kutaka kuyapiga mnada, ni vivu tuu dhidi ya mafanikio yake!.

Jee endelee tuu kuwapuuza, or this time, awazingatie?.
P
Uongozi wa kuacha alama hautaki VYETI bali kipaji cha kuzaliwa nacho amabacho anacho tayari. Wana-Darisalama mmepata jembe
 
Back
Top Bottom