Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

View attachment 1342730
View attachment 1342609
Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu.
Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na matendo maovu dhidi ya makundi maalum.
Marekani ina hofu kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na kupuuzwa kwa utawala wa sheria nchini Tanzania.
Kifungu namba 7031(c) kinampa uwezo Waziri wa Mambo ya nje kuweka zuio kama hili endapo mhusika amefanya ufisadi mkubwa au uvunjifu wa Haki za Binadamu. Pia kinamruhusu kuweka zuio kwa familia yake hivyo mke wa Makonda, Bi. Mary Felix Massenge amezuiwa pia.
Serikali ya Marekani inaikumbusha Serikali ya Tanzania kuheshimu utawala wa Sheria na Haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika.
View attachment 1342609

Hata hawa Wamarekani ni wivu tuu dhidi ya Makonda.

Kiukweli hawa mabeberu Wamarekani ni washenzi sana!, Wanamuonea bure Makonda tena kwasababu safari za Makonda US ni safari binafsi za yale mambo ya kifamilia, kumzuia Makonda kuingia US ni ukiukwaji wa haki ya msingi ya binaadamu.

Wito kwa Rais Magufuli, toa waraka hakuna kiongozi yoyote wa serikali yako ataomba Visa kuingia US, wanataka kutudhalilisha tuu, kwani Marekani ndio nini?. Twende China!.
To hell with America!.
Let's say no to American with their filthy blood stained, stinking money except " kwa msaada wa watu wa Marekani" zikiwemo ARV.
P
 
Mafanikio![emoji41][emoji41][emoji41]
Screenshot_20200201-062516-picsay.jpeg
Screenshot_20200201-062303-picsay.jpeg
 
Hata hawa Wamarekani ni wivu tuu dhidi ya Makonda.

Kiukweli hawa mabeberu Wamarekani ni washenzi sana!, Wanamuonea bure Makonda tena kwasababu safari za Makonda US ni safari binafsi za yale mambo ya kifamilia, kumzuia Makonda kuingia US ni ukiukwaji wa haki ya msingi ya binaadamu.

Wito kwa Rais Magufuli, toa waraka hakuna kiongozi yoyote wa serikali yako ataomba Visa kuingia US, wanataka kutudhalilisha tuu, kwani Marekani ndio nini?. Twende China!.
To hell with America!.
Let's say no to American with their filthy blood stained, stinking money except " kwa msaada wa watu wa Marekani" zikiwemo ARV.
P
Tunangoja nini?

Makonda si awapige ban Wamarekani wote kwenye jiji lake na Rais amuunge mkono kwa kuwapiga ban kuingia Tanzania?

Yanini tunaandikia mate na wino upo?

Hatuwezi na hatutoweza.

"We are dependents and not independents".

Tutaijuwa faida ya kuwa ombaomba, kama hatujanyang'anywa sahani mdomoni.

Juzi hao hao tunaowaita "mabeberu" wamechelewesha kutupakulia pilau la wanafunzi, tunalalamika.

China tayari kwa sasa hivi kuna ban ya Allah. Nenda tu kama unaweza.
 
Tunangoja nini?

Makonda si awapige ban Wamarekani wote kwenye jiji lake na Rais amuunge mkono kwa kuwapiga ban kuingia Tanzania?

Yanini tunaandikia mate na wino upo?

Hatuwezi na hatutoweza.

"We are dependents and not independents".

Tutaijuwa faida ya kuwa ombaomba, kama hatujanyang'anywa sahani mdomoni.

Juzi hao hao tunaowaita "mabeberu" wamechelewesha kutupakulia pilau la wanafunzi, tunalalamika.

China tayari kwa sasa hivi kuna ban ya Allah. Nenda tu kama unaweza.
Ni wewe kweli dada yangu uliyeandika?
Utawala huu kila mtu ananena kwa namna yake
 
Dah, nikajua umeleta vyeti vyake Mkuu.. Kumbe wale wale tu, umejipambanua sana mwanzoni kwa Mkwara kua mwandishi mtafiti, acha kiki mkuu.

[HASHTAG]#vyetimubashara[/HASHTAG]
Acha uzuzu wewe funguka. Kwani vladmir putin alipokua bagamoyo miaka ya 70 akifundisha wpigania uburu aliitwa putin? Aitwe chochote makonda ameshiriki kukomesha wauza dawa za kulevya. Fisadi hao wana kisasi wanahitaji damu yake.
 
Hata hawa Wamarekani ni wivu tuu dhidi ya Makonda.

Kiukweli hawa mabeberu Wamarekani ni washenzi sana!, Wanamuonea bure Makonda tena kwasababu safari za Makonda US ni safari binafsi za yale mambo ya kifamilia, kumzuia Makonda kuingia US ni ukiukwaji wa haki ya msingi ya binaadamu.

Wito kwa Rais Magufuli, toa waraka hakuna kiongozi yoyote wa serikali yako ataomba Visa kuingia US, wanataka kutudhalilisha tuu, kwani Marekani ndio nini?. Twende China!.
To hell with America!.
Let's say no to American with their filthy blood stained, stinking money except " kwa msaada wa watu wa Marekani" zikiwemo ARV.
P
Mama yangu aliwahi kuniambia;
"Mtoto wangu, ukienda huko maduniani, ukakutana na mtu mwenye NGUVU SANA akataka kukupiga hata akikusukuma wewe nyamaza kimya, hii haimaanishi kuwa huwezi kujibu ila mtu mkimya hapigwi"

Kwa mtazamo wangu, naona suala la kutoa waraka tutakuwa tumekwenda mbali sana kwani bado tunawahitaji sana kwenye science na technology hivyo tunaweza kufanya hivyo ila kimya kimya...

Japo cha kushangaza zaidi ni kuwa;
Mheshimiwa Makonda sio msemaji wa Serikali ya TZ hivyo hata kama hawakufurahishwa na baadhi ya maelekezo kwa Mkoa wake, sijui kwa nini wasifuate utaratibu wa kuwasiliana na Msemaji wa Serikali ili kupata ufafanuzi na msimamo wa serikali; hapo naona kuna ukiukwaji wa upatikanaji wa habari (wanasheria watatusaidia hapa)

Nafikiri tunakokwenda, Serikali itabidi iwe inatoa ufafanuzi mara moja pale kunapokuwa na maelekezo kutoka kwa viongozi ambayo yakaonekana kuleta ukinzani wakimtazamo wa kimataifa ili kuepusha changamoto kama hizi
 
Wakuu ebu tujadili kidogo

Vurugu Kubwa zimezuka Siku ya jumatano ya tarehe 09 March 2022, Kufuatia Ugomvi wa Kugombania nyumba ya ghorofa mbili ambayo Kila mmoja, Paul Makonda na Gharib Mohammed Bilal anadai ni mali yake

Ugomvi huo Umezuka mpaka kufikia hatua ya Paul Makonda kurushiwa risasi zaidi ya 8, baada ya Gharib Mohammed Bilal Kuondoa walinzi na mafundi wa Paul Makonda kisha Kuweka Walinzi wake na Kumzuia Paul Makonda Kufika katika Kiwanja namba 60 Kilichopo mtaa wa Regent Estate Eneo la Mikocheni.

Gazeti na MwanaHabari Lili fanikiwa kuwahoji baadhi ya Watu walioshuhudia tukio hilo la kushangaza, ambao waliokwepo eneo la tukio akiwemo mwenyekiti wa mtaa ambaye alisogea mahala hapo mara baada ya Kusikia milio ya risasi kwa muda mrefu.

Baada ya mwandishi wetu Kufanya Uchunguzi wa Kina Juu ya Paul Makonda ambaye aliwahi Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Gazeti letu limebaini kuwa Kiwanja hicho ni Mali yake halali ambayo ameuziwa na Gharib Bilal terehe 18 november mwaka 2013 kwa Hati za mauziano wakati Makonda hajawa hata Kiongozi wa Serikali Bado, Wakati huo mkewe ndiye aliyekuwa anafanya Kazi Katika shirika lisilo la kiserikali la IFAKARA HEALTH INSTITUTE

Gazeti la MwanaHabari limefanikiwa Kuona nyaraka hizo mbalimbali , ambapo Gharib Mohammed Bilal alisaini Mkataba wa mauziano na Paul Makonda chini ya Kamishina Wa Kiapo Wakili Ibrahim Shinen

(pichani ni Mkataba wa Mauziano ya Kiwanja na Picha za Garib Bilal na Paul Makonda, ukiithibitishwa na Kamishina wa viapo wakili Ibrahim Mashinen)

Uchunguzi wa Gazeti la MwanaHabari umebaini kuwa Paul Makonda na Gharib Mohammed Bilal Wanafahamiana kwa Muda mrefu sana kabla hajawa Kiongozi wa Serikali, Wakati wa awamu ya Nne ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete

pia Gazeti la MwanaHabari limeona nyaraka nyingine ambazo zimesainiwa na Mke wa Gharib Bilal ambaye ni Bi Salha Islam Sahaag ikimruhusu na Kutoa idhini kwa Paul Makonda Kubadili hati ya Umiliki ambayo pia Gharib Bilal alimkabidhi Makonda kama Sehemu ya mauziano yao mbele ya Kamishina Wa viapo wakili Ibrahim Shinen Mwaka huo huo 2013
(Pichani ni Nyaraka ya Kuridhia Kubadili Hati Iliyo ikiwa na Picha ya Mke wa Gharib Mohammed Bilal)


Katika hali ya Kushangaza Gharib Mohammed Bilal ameibuka ghafla wakati huu na Kudai Kiwanja ambacho alimuuzia Paul Makonda ambaye tayari ameshajenga Jengo la Ghorofa mbili za makazi zaidi ya familia moja katika Kiwanja hicho kuwa bado ni Mali yake.

Kitu ambacho kimezua Maswali Kwanini sasa.? na Muhusika alikuwa wapi wakati Kiwanja hicho kimeanza Ujenzi zaidi ya miaka 6 nyuma mwaka mmoja baada ya mauziano mpaka Leo Jengo linakaribia Kuisha.

Uchunguzi wa Gazeti umebaini Kuna Wanasiasa walionyuma ya mpango huu wa kumdhoofisha na Kuhakikisha Paul Makonda

Baadhi ya watu Walio karibu Gharib Mohammed Bilal kwa muda mrefu wa Wameshangazwa na uhasama huo, kwa sababu wanawahamu familia ya Gharib Mohammed Bilal na Paul Makonda ni Familia rafiki kwa muda Mrefu ambazo zimekuwa zikisaidiana kwa raha na matatizo

Watu hao wanasema kuwa Naibu Waziri mmoja wa awamu ya sita kwa Jina la Ridhiwani Kikwete ndiye anaye mchochea mfanyabiashara huyo Kupora nyumba ya Paul Makonda na Kisha kutaka kumilikishwa yeye

Aidha Gharib Bilal anatajwa pia katika Kile Kinachodaiwa mkakati wa Kumdhalilisha Paul Makonda kwa Kufadhili Kesi dhidi ya Pual Makonda ambayo imefunguliwa na mwanasiasa mmoja wa Upinzani ambaye amekuwa kwenye Vita na Paul Makonda yeye na magazeti yake kwa ufadhili wa pesa za Gharib Mohammed Bilal kama Sehemu ya Kumkomoa na Kumdhalilisha Paul Makonda

Baada ya kuona Kesi ile haina tija na haija fanikiwa anachokitaka cha Kumdhalilisha na kumdhoofisha Paul Makonda

Sasa Gharib Mohammed Bilal ameingia Ulingoni yeye mwenyewe mchana kweupe kwa Kutaka kupora mali za Paul Makonda ikiwemo Jengo la ghorofa mbili la Kiwanja namba 60 Mtaa wa Regent Estate, Mikocheni kisha Kumpatia Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete mali hiyo.

Mkakati huo Ulinaswa Kufuatia Kikao cha January 15 2022, Siku saba baada ya Ridhiwani Kikwete Kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Gharib Bilal alimuita mwanasiasa huyo Katika moja ya Majengo yake (Appartment) anazomiliki Masaki kwa ubia wa Kampuni ya GSM na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ambapo mtoto wa Rais Mstaafu Miraji Kikwete anaishi katika jengo hilo

Kikao Kilikuwa ni Kuhusu Kupora jengo la Paul Makonda Mikocheni kisha Kumkabidhi Ridhiwani Kikwete kama atafanikisha Mpango huo ambapo Gharib Bilal amenukuliwa akisema "Kuliko yule Mbwa akae pale Kwemye Kiwanja nilichomuuizia, Bora Uchukue wewe, Kama akitaka pesa yake ya Kiwanja nitamrudishia"

Kazi ambayo Ridhiwani Kikwete alienda Kufanya na Kutoa hati nyingine kwa Jina la Gharib Mohammed Bilal mbali na Kuwa hati ya mwanzo Gharib Bilal alimkabidhi Paul Makonda na anajua ipo wapi ila walitengezea nyingine kwa kisingizio cha ya Kwanza imepotea .

Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete kupitia Wizara ya Ardhi alitoa hati nyingine kwa Jina la Gharib Bilal tarehe 31 January 2022, siku 22 baada ya Kuapishwa Kushika nyadhifa hiyo Wakati Waziri Wa Ardhi Angelina Mabula akiwa mgonjwa Kitandani na bado ajaapishwa kuanza kazi Rasmi.

Baada Ya Paul Makonda kutaarifiwa Mchezo huo na Wasamaria Wema katika Wizara ya Ardhi, alikwenda Wizara ya Ardhi na Kuonyesha Nyaraka za Mauziano na Makabidhiano Wizara ya Ardhi, kiasi Kupelekea maafisa wa Ardhi Kujiridhisha na Kuweka zuio la hati Mpya iliyotoka kutotambulika Kisheria (Caveat)

Watu Walio Karibu na Naibu Waziri huyo wa Ardhi wanasema, Mwanasiasa huyo aliapa Kusaidia mkakati wa Kumdhoofisha na Kumdhalilisha Makonda kama Sehemu ya Kulipa Kisasi kwa Mwanasiasa huyo Kufuatia Kutajwa kwake katika kashfa ya Kujihusisha na madawa ya Kulevya wakati Ule Paul Makonda akiendesha operesheni maalum ya Kuwataja hadharani watu wote wanaojihusha na usafirishwaji na uuzaji wa madawa ya Kulevya


Mwenyekiti Wa mtaa wa Regent Estate,Mikocheni amekiri katika Kikao Kilicho fanyika katika Jengo hilo mara baada ya vurugu na Kurushiana risasi Kilicho fanyika Chini ya Kamanda wa Polisi Wa Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay aliyetambulika kwa Jina moja la Wendo, Kuwa wao manamtambua Paul Makonda kuwa Mmiliki wa Jengo hilo kwa sababu Wamekuwa wa Kumuona Mtaani hapo anajenga na Kuleta Vifaa Vya Ujenzi kwa zaidi ya miaka 5 iliyopita

Alisema "Makonda ameshiriki Katika Kukarabati hata hizi barabara za mtaa huu, Katika Kuleta vifusi na hii lami Unayo iona hapa ilikupata urahisi wa Kufika katika Jengo hili"

Gazeti limewahoji pia baadhi ya Viongozi wa Serikali ambao hawakutaka Kutajwa kwa sasa, wametoa Ufafanuzi kuwa Serikali Inafahamu mikakati yote michafu dhidi ya Paul Makonda ni Visasi na udhalilishaji kwa sababu wao kama Serikali Walitoa wito wenye Ushahidi Kamili wa Kuporwa mali Kwenda Takukuru Kufungua malalamiko lakini Hakuna hata mmoja aliye fanya hivyo.

Badala yake Watu wamekuwa Wanatumia mitandao ya Kijamii na njia nyinginezo, Wakati Swala la Ujenzi Wa Nyumba ya Makonda Serikali Inafahamu kupitia Fomu za Umiliki wa Mali kwa Viongozi wa Umma na mara Kadhaa Vyombo Vya Dola Vimefika eneo la Ujenzi kama Sehemu ya Utejelezaji majukumu Yake asingeweza Kujenga pale alafu Serikali isijue, Kwa sasa Makonda anakaa katika nyumba za Kupanga za Serikali (TBA) pale Oysterbay

Wadau wengine wamekerwa na Madai ya Garib Mohammed Bilal kumuhusisha moja kwa moja Paul Makonda na Hayati Rais John Pombe Magufuli kama Sehemu ya kulipiza Kisasi kwa Serikali Ya awamu ya TANO Kupitia Makonda ambaye aliwahi Kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam.

Wengi Wana amini Serikali ya awamu ya tano ya hayati John Pombe Magufuli imemsaidia sana Garib Mohammed Bilal hasa katika Ugomvi wake wa familia baada ya Kushutumiwa Kumwaga tindikali na Kaka yake Said Mohamed Saad ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Home shopping Center kisha kuhamisha Umiliki wa mali za Kaka yake akiwa Kwenye Matibabu huko Nchini Dubai mpaka kufikia Ndugu hao Kutaka kuuana

Serikali ya awamu ya tano imepata lawama nyingi sana Juu ya kumkingia kifua Gharib Mohammed Bilal katika Maswala ya Ukwepaji Kodi, Utoroshaji wa makontena bandarini na tabia ya Kubadili Majina ya Kampuni kila kukicha wengi Wanahisi Serikali ilimbeba sana, hastahili Kuonyesha Chuki kama anayo onyesha Sasa.
Asante Sana kwa taarifa hii, naomba Mimi Mwanajeiefu mwenzenu, niwe mtu wa kwanza kuwajulisha kuwa hii vita ya kutaka kumdhalilisha mpakwa mafuta wa Bwana, Paul Makonda, sasa ndio mwanzo wa mwisho wa hasidi huyu!. Karma ndio itamaliza kila kitu. Simaanishi Makonda ni malaika, bali, ni binaadamu kama binadamu wengine, hakuna mkamilifu, hivyo na yeye kuna makosa ametenda na tayari karma imeisha mshughulikia, hivyo kwa maonevu anayotendewa na hasidi huyu, ni Mungu, Baba ndiye atamlipia.
Kwanza mafanikio yake ni kutoka kwa Mungu.

Kisha, Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Hivyo, hata kampeni batili ya kutaka kumpora kiwanja, ni upepo tuu na utapita.

Watu kumfanyia fitna na majungu, Makonda, hawakuanza leo

Yote haya yatapita, na Makonda atasimama.
P
 
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia mtandao wa Instagram amechapisha akilalamika kuwa kuna makundi 5 ya watu wanaopanga kumuangamiza.

Makonda amesema makundi hayo yanataka kuhakikisha anapata kesi ya uhujumu uchumi au auwawe kabisa kwa manufaa yao binafsi.

"Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida a familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi" Makonda ameandika.

Aidha makonda amebainisha makundi hayo yanaundwa na wauza madawa ya kulevya, mashoga, mafisadi, wanufaika na madawa ya kulevya na kundi la mwisho ambalo hakuliweka wazi. Ameandika kuwa licha ya kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa ofisini lakini bado kuna watu wanataka kumpoteza.

Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndivo malipo yake?, mtu aliejenga hospital , aliejenga ofisi za CCM, magari ya police ofisi za walimu, vituo vya polisi, shule za secondari na msingi, kutibu wagonjwa mpaka meli kuja Tanzania, kuhudumia makundi mbalimbali mpaka kuiunganisha serikali na viongozi wa dini leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa?" amehoji.

Sio mara ya kwanza Makonda kulalamika ingawaje hapo awali alisema kuwa kuna watu wana muhujumu kutaka kupora mali zake kwa maksudi.

Malalamiko haya ya Makonda yanaibua hisia na maswali mengi ambayo mtu anaweza kujiuliza ni nini kinamsibu Makonda?
Alipo sema kuwa wanataka kumnyang'anya mali ikaonekana ni jambo dogo lakini kufika kuhofia uhai wake ni jambo kubwa linalohitaji kujulikana.

Kama kweli kuna watu wanataka kumdhuru makonda ni akina nani hao na kwanini wasichukuliwe hatua?

Makonda anadai hayo makundi 5 ya watu wanootaka kumpoteza yanajulikana kwanini asipeleke malalamiko kwenye vyombo vya dora Mahakama na polisi kwa hatua za kisheria zaidi?

Tuseme kwamba Makonda haviamini vyombo vya dora hadi anakimbilia mitandaoni kulalamika ili apate huruma ya raia wa kawaida?

Hatuwezi kufikiria kuwa Makonda aliyetatua migogoro lukuki akiwa mkuu wa Mkoa hajui taratibu za kufuata ili kuripoti matukio kama haya?

Hapana kabisa bado kuna maswali mengi tunapaswa kujiuliza ili tupate kujua makonda ana hofu gani inayomtafuna na kumfanya alalamike kila kukicha.

Hatuwezi kujua ukubwa wa madaraka ya watu hao alio wataja katika makundi matano pengine ni wakubwa kimamlaka anohofia hawezi kupata haki, lakini mahakama na polisi ni vyombo huru anaogopa nini?

Bila shaka serikali ina miongozo yake katika kuwasaidia viongozi wake wastaafu kwanini Makonda hajatumia nafasi hiyo kulalamika?
Malalamiko ya Makonda Mitandaoni yanafikirisha na yanahitaji majibu.

Peter Mwaihola

View attachment 2184198
P
 
Asante Sana kwa taarifa hii, naomba Mimi Mwanajeiefu mwenzenu, niwe mtu wa kwanza kuwajulisha kuwa hii vita ya kutaka kumdhalilisha mpakwa mafuta wa Beans, Paul Makonda, sasa ndio mwanzo WA mwisho wa hasidi huyu!. Karma ndio itamaliza kila kitu. Simaanishi Makonda ni malaika, bali, ni binaadamu kama binadamu wengine, hakuna mkamilifu, hivyo na yeye kuna makosa ametenda na tayari karma imeisha mshughulikia, hivyo kwa maonevu anayotendewa na hasidi huyu, ni Mungu, Baba ndiye atamlipia.
Kwanza mafanikio yake ni kutoka kwa Mungu.

Kisha, Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Hivyo, hata kampeni batili ya kutaka kumpora kiwanja, ni upepo tuu na utapita.

Watu kumfanyia fitna na majungu, Makonda, hawakuanza leo

Yote haya yatapita, na Makonda atasimama.
P
Atasimama lini?
 
Back
Top Bottom