Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Mkuu ni hivyohivyo hata kwa hao viongozi wa umma unaowasema unaweza kwenda mahakamani pia...

GSM aka Ghalib anashindwaje kwenda mahakamani pia?...
Umiza kichwa siku zote kwa ajili ya wale wanaokuhusu. Ukifanya kazi huku unawafikiria wengine utakufa ukiumizwa na hali yako kumbuka siku zote utaona wao kukuzidi kumetokana na wizi au ngozi yao kuwapendelea.

Ni aina fulani ya wivu unaosumbua watu weusi wengi na kujikuta wakijiingiza katika ushirikina unaowaumiza kwa kuwaachia laana za vizazi na vizazi.
 
Wakuu ebu tujadili kidogo

Vurugu Kubwa zimezuka Siku ya jumatano ya tarehe 09 March 2022, Kufuatia Ugomvi wa Kugombania nyumba ya ghorofa mbili ambayo Kila mmoja, Paul Makonda na Gharib Mohammed Bilal anadai ni mali yake

Ugomvi huo Umezuka mpaka kufikia hatua ya Paul Makonda kurushiwa risasi zaidi ya 8, baada ya Gharib Mohammed Bilal Kuondoa walinzi na mafundi wa Paul Makonda kisha Kuweka Walinzi wake na Kumzuia Paul Makonda Kufika katika Kiwanja namba 60 Kilichopo mtaa wa Regent Estate Eneo la Mikocheni.

Gazeti na MwanaHabari Lili fanikiwa kuwahoji baadhi ya Watu walioshuhudia tukio hilo la kushangaza, ambao waliokwepo eneo la tukio akiwemo mwenyekiti wa mtaa ambaye alisogea mahala hapo mara baada ya Kusikia milio ya risasi kwa muda mrefu.

Baada ya mwandishi wetu Kufanya Uchunguzi wa Kina Juu ya Paul Makonda ambaye aliwahi Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Gazeti letu limebaini kuwa Kiwanja hicho ni Mali yake halali ambayo ameuziwa na Gharib Bilal terehe 18 november mwaka 2013 kwa Hati za mauziano wakati Makonda hajawa hata Kiongozi wa Serikali Bado, Wakati huo mkewe ndiye aliyekuwa anafanya Kazi Katika shirika lisilo la kiserikali la IFAKARA HEALTH INSTITUTE

Gazeti la MwanaHabari limefanikiwa Kuona nyaraka hizo mbalimbali , ambapo Gharib Mohammed Bilal alisaini Mkataba wa mauziano na Paul Makonda chini ya Kamishina Wa Kiapo Wakili Ibrahim Shinen

(pichani ni Mkataba wa Mauziano ya Kiwanja na Picha za Garib Bilal na Paul Makonda, ukiithibitishwa na Kamishina wa viapo wakili Ibrahim Mashinen)

Uchunguzi wa Gazeti la MwanaHabari umebaini kuwa Paul Makonda na Gharib Mohammed Bilal Wanafahamiana kwa Muda mrefu sana kabla hajawa Kiongozi wa Serikali, Wakati wa awamu ya Nne ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete

pia Gazeti la MwanaHabari limeona nyaraka nyingine ambazo zimesainiwa na Mke wa Gharib Bilal ambaye ni Bi Salha Islam Sahaag ikimruhusu na Kutoa idhini kwa Paul Makonda Kubadili hati ya Umiliki ambayo pia Gharib Bilal alimkabidhi Makonda kama Sehemu ya mauziano yao mbele ya Kamishina Wa viapo wakili Ibrahim Shinen Mwaka huo huo 2013
(Pichani ni Nyaraka ya Kuridhia Kubadili Hati Iliyo ikiwa na Picha ya Mke wa Gharib Mohammed Bilal)


Katika hali ya Kushangaza Gharib Mohammed Bilal ameibuka ghafla wakati huu na Kudai Kiwanja ambacho alimuuzia Paul Makonda ambaye tayari ameshajenga Jengo la Ghorofa mbili za makazi zaidi ya familia moja katika Kiwanja hicho kuwa bado ni Mali yake.

Kitu ambacho kimezua Maswali Kwanini sasa.? na Muhusika alikuwa wapi wakati Kiwanja hicho kimeanza Ujenzi zaidi ya miaka 6 nyuma mwaka mmoja baada ya mauziano mpaka Leo Jengo linakaribia Kuisha.

Uchunguzi wa Gazeti umebaini Kuna Wanasiasa walionyuma ya mpango huu wa kumdhoofisha na Kuhakikisha Paul Makonda

Baadhi ya watu Walio karibu Gharib Mohammed Bilal kwa muda mrefu wa Wameshangazwa na uhasama huo, kwa sababu wanawahamu familia ya Gharib Mohammed Bilal na Paul Makonda ni Familia rafiki kwa muda Mrefu ambazo zimekuwa zikisaidiana kwa raha na matatizo

Watu hao wanasema kuwa Naibu Waziri mmoja wa awamu ya sita kwa Jina la Ridhiwani Kikwete ndiye anaye mchochea mfanyabiashara huyo Kupora nyumba ya Paul Makonda na Kisha kutaka kumilikishwa yeye

Aidha Gharib Bilal anatajwa pia katika Kile Kinachodaiwa mkakati wa Kumdhalilisha Paul Makonda kwa Kufadhili Kesi dhidi ya Pual Makonda ambayo imefunguliwa na mwanasiasa mmoja wa Upinzani ambaye amekuwa kwenye Vita na Paul Makonda yeye na magazeti yake kwa ufadhili wa pesa za Gharib Mohammed Bilal kama Sehemu ya Kumkomoa na Kumdhalilisha Paul Makonda

Baada ya kuona Kesi ile haina tija na haija fanikiwa anachokitaka cha Kumdhalilisha na kumdhoofisha Paul Makonda

Sasa Gharib Mohammed Bilal ameingia Ulingoni yeye mwenyewe mchana kweupe kwa Kutaka kupora mali za Paul Makonda ikiwemo Jengo la ghorofa mbili la Kiwanja namba 60 Mtaa wa Regent Estate, Mikocheni kisha Kumpatia Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete mali hiyo.

Mkakati huo Ulinaswa Kufuatia Kikao cha January 15 2022, Siku saba baada ya Ridhiwani Kikwete Kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Gharib Bilal alimuita mwanasiasa huyo Katika moja ya Majengo yake (Appartment) anazomiliki Masaki kwa ubia wa Kampuni ya GSM na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ambapo mtoto wa Rais Mstaafu Miraji Kikwete anaishi katika jengo hilo

Kikao Kilikuwa ni Kuhusu Kupora jengo la Paul Makonda Mikocheni kisha Kumkabidhi Ridhiwani Kikwete kama atafanikisha Mpango huo ambapo Gharib Bilal amenukuliwa akisema "Kuliko yule Mbwa akae pale Kwemye Kiwanja nilichomuuizia, Bora Uchukue wewe, Kama akitaka pesa yake ya Kiwanja nitamrudishia"

Kazi ambayo Ridhiwani Kikwete alienda Kufanya na Kutoa hati nyingine kwa Jina la Gharib Mohammed Bilal mbali na Kuwa hati ya mwanzo Gharib Bilal alimkabidhi Paul Makonda na anajua ipo wapi ila walitengezea nyingine kwa kisingizio cha ya Kwanza imepotea .

Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete kupitia Wizara ya Ardhi alitoa hati nyingine kwa Jina la Gharib Bilal tarehe 31 January 2022, siku 22 baada ya Kuapishwa Kushika nyadhifa hiyo Wakati Waziri Wa Ardhi Angelina Mabula akiwa mgonjwa Kitandani na bado ajaapishwa kuanza kazi Rasmi.

Baada Ya Paul Makonda kutaarifiwa Mchezo huo na Wasamaria Wema katika Wizara ya Ardhi, alikwenda Wizara ya Ardhi na Kuonyesha Nyaraka za Mauziano na Makabidhiano Wizara ya Ardhi, kiasi Kupelekea maafisa wa Ardhi Kujiridhisha na Kuweka zuio la hati Mpya iliyotoka kutotambulika Kisheria (Caveat)

Watu Walio Karibu na Naibu Waziri huyo wa Ardhi wanasema, Mwanasiasa huyo aliapa Kusaidia mkakati wa Kumdhoofisha na Kumdhalilisha Makonda kama Sehemu ya Kulipa Kisasi kwa Mwanasiasa huyo Kufuatia Kutajwa kwake katika kashfa ya Kujihusisha na madawa ya Kulevya wakati Ule Paul Makonda akiendesha operesheni maalum ya Kuwataja hadharani watu wote wanaojihusha na usafirishwaji na uuzaji wa madawa ya Kulevya


Mwenyekiti Wa mtaa wa Regent Estate,Mikocheni amekiri katika Kikao Kilicho fanyika katika Jengo hilo mara baada ya vurugu na Kurushiana risasi Kilicho fanyika Chini ya Kamanda wa Polisi Wa Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay aliyetambulika kwa Jina moja la Wendo, Kuwa wao manamtambua Paul Makonda kuwa Mmiliki wa Jengo hilo kwa sababu Wamekuwa wa Kumuona Mtaani hapo anajenga na Kuleta Vifaa Vya Ujenzi kwa zaidi ya miaka 5 iliyopita

Alisema "Makonda ameshiriki Katika Kukarabati hata hizi barabara za mtaa huu, Katika Kuleta vifusi na hii lami Unayo iona hapa ilikupata urahisi wa Kufika katika Jengo hili"

Gazeti limewahoji pia baadhi ya Viongozi wa Serikali ambao hawakutaka Kutajwa kwa sasa, wametoa Ufafanuzi kuwa Serikali Inafahamu mikakati yote michafu dhidi ya Paul Makonda ni Visasi na udhalilishaji kwa sababu wao kama Serikali Walitoa wito wenye Ushahidi Kamili wa Kuporwa mali Kwenda Takukuru Kufungua malalamiko lakini Hakuna hata mmoja aliye fanya hivyo.

Badala yake Watu wamekuwa Wanatumia mitandao ya Kijamii na njia nyinginezo, Wakati Swala la Ujenzi Wa Nyumba ya Makonda Serikali Inafahamu kupitia Fomu za Umiliki wa Mali kwa Viongozi wa Umma na mara Kadhaa Vyombo Vya Dola Vimefika eneo la Ujenzi kama Sehemu ya Utejelezaji majukumu Yake asingeweza Kujenga pale alafu Serikali isijue, Kwa sasa Makonda anakaa katika nyumba za Kupanga za Serikali (TBA) pale Oysterbay

Wadau wengine wamekerwa na Madai ya Garib Mohammed Bilal kumuhusisha moja kwa moja Paul Makonda na Hayati Rais John Pombe Magufuli kama Sehemu ya kulipiza Kisasi kwa Serikali Ya awamu ya TANO Kupitia Makonda ambaye aliwahi Kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam.

Wengi Wana amini Serikali ya awamu ya tano ya hayati John Pombe Magufuli imemsaidia sana Garib Mohammed Bilal hasa katika Ugomvi wake wa familia baada ya Kushutumiwa Kumwaga tindikali na Kaka yake Said Mohamed Saad ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Home shopping Center kisha kuhamisha Umiliki wa mali za Kaka yake akiwa Kwenye Matibabu huko Nchini Dubai mpaka kufikia Ndugu hao Kutaka kuuana

Serikali ya awamu ya tano imepata lawama nyingi sana Juu ya kumkingia kifua Gharib Mohammed Bilal katika Maswala ya Ukwepaji Kodi, Utoroshaji wa makontena bandarini na tabia ya Kubadili Majina ya Kampuni kila kukicha wengi Wanahisi Serikali ilimbeba sana, hastahili Kuonyesha Chuki kama anayo onyesha Sasa.
 
Wakuu ebu tujadili kidogo

Vurugu Kubwa zimezuka Siku ya jumatano ya tarehe 09 March 2022, Kufuatia Ugomvi wa Kugombania nyumba ya ghorofa mbili ambayo Kila mmoja, Paul Makonda na Gharib Mohammed Bilal anadai ni mali yake...
Siku zote mali inayopatikana kwa njia ya haramu lazima iwe na matatizo
 
Wakuu ebu tujadili kidogo

Vurugu Kubwa zimezuka Siku ya jumatano ya tarehe 09 March 2022, Kufuatia Ugomvi wa Kugombania nyumba ya ghorofa mbili ambayo Kila mmoja, Paul Makonda na Gharib Mohammed Bilal anadai ni mali yake...
Hilo ni gazeti au ni kipeperushi cha kuchafulia watu na kumsafisha Makonda?
 
Makonda ni jambazi hilo halina ubisha mtu umekua mkuu wa wilaya na mkoa less than 10 years unamiliki utajiri Mkubwa umeupata wapi na sio mfanyabiashara ni picha gani unawafundisha vijana kwamba ukiwa mkuu wa wilaya au mkoa unakua billionaire kama makonda maisha sio marahisi hivyo makonda aliwapora malizake waende wakachukue iwe ni somo
 
issue ni unafiki wa wao kujifanya ndugu zetu aka Watanzania wenzetu halafu gizani wanatumaliza na wakijinadi hapa sio kwao, wakati mwingine hata kunyanyapaa ndugu zetu kwa kuwatumikisha kama watumwa...
Unatumia nguvu nyingi kumtetea uovu, unatuchosha hata kama una uhuru wa maoni
 
Hatuwezi kuukalia kimya UFEDHULI wa Makonda eti kwa sababu na sisi tuna dhambi zetu. Dunia haiendi hivyo, huyu Bashite na Sabaya walikuwa wanamtumikia DIKTETA Magufuli wakidhani hawezi kutoka madarakani au kufa. Walikuwa sawa na Bob Astles na Maliyamungu chini ya Iddi Amini.

"Mkundu ukifa mavi hutawanyika",
Unatamani hata muda huu afe siyo kwa povu hilo.

Bado nasimamia, hata wewe umefanya/unafanya mengi mabaya nani anakufahamu ili kukuanika?

Stand in your time uje uhesabiwe, asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga mawe huyo.

Acha unafiki.
 
Akihojiwa kwenye kipindi cha Clouds 360 CAG mstaafu Uttoh alisema siyo kwamba awamu ya 5 hapakuwa na rushwa ilikuwepo ila kikundi cha watu wachache ndio kilijineemesha kwa dili kubwa kubwa tu " the higher the risk....."

Kiukweli nchi hii Usimwamini yoyote hata Tundu Lisu au Bagonza wewe mwamini Mungu wa mbinguni only.

Maendeleo hayana vyama!
 
Makonda ni jambazi hilo halina ubisha mtu umekua mkuu wa wilaya na mkoa less than 10 years unamiliki utajiri Mkubwa umeupata wapi na sio mfanyabiashara ni picha gani unawafundisha vijana kwamba ukiwa mkuu wa wilaya au mkoa unakua billionaire kama makonda maisha sio marahisi hivyo makonda aliwapora malizake waende wakachukue iwe ni somo
Je unaijua kazi ya mkewe?

Je una uhakika kama hana biashara nyingine ya kumuingizia kipato?

Pia ukumbuke kwamba Makonda anayo haki ya kukopa toka taasisi yoyote ya kifedha nchini.ilimradi anatimiza vigezo na masharti.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.

Mwenye madai halali ya kudhulumiwa asibaki mtandaoni tu bali aende TAKUKURU.

Hizo mali zake pia zimeorodheshwa kwenye daftari la mali za viongozi.
 
Back
Top Bottom