Pre GE2025 Kumbe RC Makonda yuko Likizo, Uzushi kwamba anaumwa upuuzwe

Pre GE2025 Kumbe RC Makonda yuko Likizo, Uzushi kwamba anaumwa upuuzwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu habari??

Leo nina swali.

Siyo kawaida kabisa kwa Ndugu Paul kutoonekana kwenye runinga wala mitandao ya kijamii kwa muda mrefu hivi.

Yuko wapi Paul Makonda?

Hakuna duru zozote zinazoweza kutuhabarisha alipo bwana mkubwa?

Mwananchi Wa Kawaida.
Dodoma.
Muambiwe mara yuko likizo

Ova
 
Huyu mama tangu aingie madarakani mnamsema sana, shida nini?

Dini yake?
Mzanzibari?
Mwanamke?
Mwarabu?
 
Kwa akili yangu ndogo,kama angelikua likizo ama hakuna tatizo lolote basi naamini mhe.Paul angesema lolote.
Ninamuombea sana uzima na Mungu amsaidie
 
Mtoa mada unaonekana huna taaluma ya sheria na hujui taratibu za utumishi.
hata hivyo mahojiano hayo hukuyasikiliza live.
RAS mwenyewe ni kama alikua hana uhakika na majibu yake, lkn ngoja nikujuze kikanuni ili mtumishi aende likizo ni lazima sio hiari ni lazima mtumishi wa umma awe amefanya kazi kwa muda wa miezi sita au nane kama nitakua nimekosea ndipo aende likizo ya mwaka.
RC Makonda tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo nadhani hata miezi mitatu haijaisha.
Kwa sheria ipi aende likizo?
 
Usikariri Kwenda likizo unaweza kwenda muda wowote kutegemea na sababu. Mfano umeajiriwa una mwezi mmoja na mke wako ni mgonjwa mahututi hapo likizo inakubalika

Pia ukweli ni kwamba senior officials wana exception kwenye mambo mengi kuliko other officials. RC, waziri, katibu, n.k hawa hawana kubanwa kama ww au yule mwalimu aliyepo namtumbo
 
Back
Top Bottom