Pre GE2025 Kumbe RC Makonda yuko Likizo, Uzushi kwamba anaumwa upuuzwe

Pre GE2025 Kumbe RC Makonda yuko Likizo, Uzushi kwamba anaumwa upuuzwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ningeshangaa sana mtu anayeombewa na Maaskofu wote Tanzania ( Kasoro Mwamakula) eti alishwe sumu, ingekuwa ajabu sana!

Pia soma: Tetesi: - Mtoto pendwa kapatwa na nini? Yuko hoi kwa Madiba, inadaiwa ni sumu

Nyie mnaoleta Taharuki mnataka nini?

Taarifa kamili hii hapa

"Kufuatia uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mahali alipo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, Katibu Tawala wa mkoa huo, Missaile Mussa amesema kuwa kiongozi huyo kwa sasa yuko likizo.

"Akihojiwa kwa njia ya simu na mwandishi wa Global TV, Julai 26, 2024 Missaile amesema hana taarifa za ziada tofauti na hizo kwamba Makonda yupo likizo."

Global TV
Sawa. Yupo likizo ICU. Akimalizo likizo yake ama ataruhusiwa kurudi nyumbani au atsrlekea mochwari. Tunamtakia likizo njema.
 
Hayupo likizo, tusifanyane wajinga.

SEMENI Ukweli ijulikane, Likizo ipi hiyo ya ghafla kama tumbo la kuhara.

Haya tumekubali sie Ni mabwege lakini Ni vizuri ukatuelewesha tarehe aliyoanza likizo na tarehe ya mwisho wa likizo yake, pili toka alivyoteuliwa kuwa RC Arusha Ni miezi mingapi mpaka kupewa likizo?
 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ndugu nurdin Babu amesema anakaimu ukuu wa mkoa wa Arusha kwa kuwa makonda aliomba likizo na ana likizo ya siku 28. Amesema hayo alipohojiwa na redio Moja ya mjini Arusha
Mbona hiyo likizo siyo ya kawaida?

Ninavyojua wanasiasa wote, hata kama wako likizo, tutasikia tu habari zao Kwa wao wenyewe kuongea na vyombo vya habari, Kwa kuwa hiyo ndiyo "hobby" yao Kuu.

Sasa kinachoshangaza kuhusu hii issue ya Makonda, kwanza haijulikani likizo hiyo kama kweli kuwa atakuwa yupo likizo, haijulikani yuko wapi na huo ukimya ndiyo unatisha😗
 
Tanzania is a Mystery country. Hatuna vyombo vya habari na wananchi wote ni mazuzu. Yaani nchi nzima wanashindwa kujua alipo Makonda? BTW Makonda ni msanii sana, inawezekana kuwa ''amepotea'' na kuvumisha kuwa amelishwa sumu ili aandae tukio kubwa la ''kupokelewa'' kwa shangwe atakapoibuka tena. Au anaweza kuwa anaumwa ugonjwa kama binadamu wengine na ameenda nje kutibiwa halafu akavumisha kuwa ni sumu. Kama Magufuli alivyokuwa anadanganya eti alilishwa sumu.
 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ndugu nurdin Babu amesema anakaimu ukuu wa mkoa wa Arusha kwa kuwa makonda aliomba likizo na ana likizo ya siku 28. Amesema hayo alipohojiwa na redio Moja ya mjini Arusha
Kwani ameanza lini kazi? Likizo si baada ya mwaka mmoja
 
MAKONDA YUPO KWAKE KIGAMBONI ANAKULA LIKIZO, HAJAFA WALA HAUMWI.

SIKU ZOTE WATU WABAYA HUWA HAWAFI KIRAHISI.
 
Back
Top Bottom