Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Coronavirus ipo. Kasome side effects za Corona.
Tunajua ipo na inaua, imeua wengi lakini sio kila kifo source ni Corona, kuongea vitu hatuna uhakika navyo ni kosa kisheria. Kama kweli ingekuwa Corona watu wasingejiachia namna walivyofanya tangu juzi mzee alivyong'ata shuka.
 
Sizungumzi uwepo wa cardiac unit ilikuwepo kabla ya JKCI na ipo ,nachosema kwa sasa JKCI wana huduma za Cardic bora zaidi. Nadhani hukunielewa vizuri. JKCI ni taasisi inayojitegejemea haiko chini ya Muhimbili. Kuna tofauti ya kuwa na Cardiac Unit na Cardiac Institute. Anyway kama unasema hapo wana utaalamu na huduma bora kuhusu Cardiac issues kuliko JKCI sawa. Shukran Mkuu

Ndio ilikua maana yangu hiyo
Pamoja mkuu
 
Sijui wataalamu, cardiac arrest ni mara moja tu, sio upate jumatano ufariki Ijumaa

Mbili, issue cardiac nilitegemea angepelekwa Hospitali yetu ya mabingwa wa moyo pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute na sio Hospitali Mzna

Tungeacha tu kujadili tumzike Mzee wetu tuendelee na mengine maana tunazidi kuleta mkanganyiko
Wewe akili ndio huna, alikua anaumwa Malaria na anaendelea vzr akifuatilia habari ktk Tv, alipokua amekaa kwenye kiti akajisikia ghafla vibaya Cardiac arrest, sasa ww ulitaka wampeleke Jakaya Kikwete Cardiac kwa tatizo la Malaria ?
 
Sijajua kwa nini mnatafuta mengi ili hali Mzee alishagonga 80's...anayepaswa kutushughulisha ni yule anayeondoka kwenye 20's,30's,40's,50's.

Tutosheke kwa huo muda wote tumekuwa naye.
 
Uko vizurii chief
Asante Kaka Mimi maamuma tu Muuza Al kasus Tandale sema ninapenda kusoma vitabu vya elimu tofauti km alivyosema MAREHEMU Mkapa kuwa TUPENDE KUJISOMEA na tusiwe MAKANJANJA MALOFA km baadhi ya wale waandishi.....watu wakamchukia Mkapa kumbe aliwaambia ukweli maskini mzee wa watu.
Rip BWM,aamen
 
Tunajua ipo na inaua, imeua wengi lakini sio kila kifo source ni Corona, kuongea vitu hatuna uhakika navyo ni kosa kisheria. Kama kweli ingekuwa Corona watu wasingejiachia namna walivyofanya tangu juzi mzee alivyong'ata shuka.
Kwani kuna familia wanasema wana mgonjwa wa corona siku hizi? Kila mtu anafanya siri huficha kisha kusingizia magonjwa mengine
 
Inaonyesha umri pia ni sababu muhimu za kupata heart arrest.
20200726_131121.jpeg
 
Kikwete: "Jana jioni nilikwenda kumuona hospitali, tulizungumza sana. Alikuwa na maumivu lakini siyo yale ambayo ukitoka kumuangalia mgonjwa unawaambia nimemuona mgonjwa lakini"

Binafsi kama itanihitaji nidescribe hali anayokua nayo mgonjwa wamalaria nisingetumia maneno kma kua namaumivu nafikir kusema kua Hakua nahoma kali nahis ingekua nataswira sahihi ya mtu anaeumwa malaria
 
Ungonjwa unaoua viongozi wakubwa huwa hawausemi watabaki kudanganya tu kwakuwa msemaji kashasema basi "ITOSHE KUSEMA NI MALARIA NA CARDIAC ARREST".
 
Kwani kuna familia wanasema wana mgonjwa wa corona siku hizi? Kila mtu anafanya siri huficha kisha kusingizia magonjwa mengine
Umeona watu wanavyojiachia? Sijui lakini naamini ingekuwa Corona tahadhari ingechukuliwa. Kingine, kumbuka Mkapa alikuwa 82 yo, Mungu alimpa maisha marefu tu, wengi miaka hii tunakata kamba 30s, 40s na 50s.
 
Kwa mazingira aliyoyazungumza mtoto sijui kikwete alienda kumuona wapi
Erio kasema ALIKUWA anaangalia taarifa ya hbr na uchaguz wa viti maalum,baadaye akasimama...alipokaa ndo ukawa UMAUTI...Sasa Jakaya kikwete anashindwaje kuwa alimuona a day or two before?
 
Umeona watu wanavyojiachia? Sijui lakini naamini ingekuwa Corona tahadhari ingechukuliwa. Kingine, kumbuka Mkapa alikuwa 82 yo, Mungu alimpa maisha marefu tu, wengi miaka hii tunakata kamba 30s, 40s na 50s.
Wananchi wamejipaka vitakasa mikono na pia ukumbuke kwa Tanzania Corona ilishatangazwa imekwisha lazima wajiachie tu ingawa corona ipo
 
Naam. Cardiac arrest ni final product ya magonjwa mbalimbali. Cardiac arrest ndio kifo chenyewe. Kwa lugha ya kitaalam kifo = cardiac arrest (aka cardio-pulmonary arrest). Cardiac arrest/kifo kinaweza kusabishwa na magonjwa mbalimbali. Kwa Mkapa tumeambiwa ni severe malaria ndio imesababisha cardiac arrest yake. That makes sense. Ukitaka kulazimisha iwe cardiac/heart attack basi kabishane na madaktari wake. Siyo wanaJF.
In most cases heart attack inasababisha Cardiac arrest.
 
Back
Top Bottom