Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Mkuu kwani Kati ya mtu aliyepokea pass ya mwisho na kutumbukiza kitu nyavuni na mtu aliyewalamba vyenga mabeki wote hadi golikipa Kisha akatoa pasi kwa mfumania nyavu ,nani Kati ya hao wawili amefunga goli

Umedadavua vyema mkuu zaidi ya hapo kuna kukataa kuelewa. Yale yale ya ng'ombe kwenda kunywa maji mtoni.
 
Yani mimi hata unichinje bado naamini kilichomsukuma mzee wetu Mkapa ni COVID 19. Full stop na tusipochukua tahadhari na kuendelea kama tulivyo basi itafika hawa wazee wameisha wote!
 
BADO JAMBO MOJA HALIJAWEKWA WAZI. NI HOSPITALI GANI ALIKOFIA? HAYA MAMBO YA KUFICHA FICHA NI USHAMBA. KANUNI ZA TANGAZO KWA UMMA (PRESS RELEASE) NI KWAMBA LIJIELEZE LENYEWE (SELF EXPLANATORY) USITOE TANGAZO LENYE KUIBUA MASWALI YASIYO YA LAZIMA.
Kafia hospitali ya hapo Makumbusho yani simple kabisa. Hii tabia ya watanzania kufuata mawazo ya mfalme na kumnyenyekea kwa kumuogopa yatatumaliza. How come unaambiwa Tanzania Corona imepotea na wewe kwa uzuzu huku ukiwa na elimu kichwani unaamini? Huo ni ulemavu wa aina yake!
 
Wanabodi,
Kumbe sababu ya kifo cha Mpendwa wetu, Benjamin William Mkapa ni Cardiac Arrest!.

Asante sana Mwanafamilia wa familia ya Mkapa, William Erio, kuusema ukweli huu na kumaliza rasmi ile sintofahamu ya chanzo cha kifo, ambayo imezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo JF.

Kama Tangazo la kifo lingezingatia sheria tangu pale mwanzo, wala kusingetokea sintofahamu yoyote!.

Hivyo japo haijasemwa ni JF, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Japo yanalaumiwa kwa kuonekana watu wana mind vitu vidogo vidogo ambayo sio vya msingi, lakini yanasaidia.

Chanzo cha kifo cha ghafla cha any state leader ambaye hajawahi kutamkwa kusumbuliwa na maradhi yoyote, automatically kita send a shock wave kwenda viral.

Baada ya kauli hii, sasa minongo yote kuhusu chanzo cha kifo imemalizwa rasmi.
Naombeni sana, wanabodi, tuwe na heshima kwa viongozi wetu na tuwe na heshima kwa marehemu, mkiisha ambiwa ukweli wa familia, then tuupokee ukweli huu, tuuamini, na kumheshimu Marehemu kwa kuto toa comments zozote negative based on hisia!.

RIP, Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

Paskali
Mvumilivu hula mbivu, Mayalla (njaa) amamrithi Hassan Abbas kama Msemaji mkuu wa Serkali, njaa kwisha! Rais mstaafu au mtu yeyote maarufu kifo chake au sababu ya kifo chake haitangazwi na mkeb au jamaa wa karibu.
 
Kwahivyo hakukuwa na shida ya cardial arrest before corona?
Still connecting the relation of Malaria with Cardiac arrest sipati jibu? but kuna uhusiano mkubwa kati ya upumuaji na shambulio la moyo.

Jiongezeni wakubwa, Israel mtoa bado anawinda roho za watu wenye shingo ngumu.
 
Duh una elimu gani?? Mnaboa sana waswahili

Nimepoteza dada mwaka 2001 alitumia alfan kutibu malaria ambayo side effects yake inaongeza mapigo ya moyo....

Pia kwa umri wa mzee cardiac arrest ingeweza kutokea bila hata kuumwa malaria...any slight weakness ya mwili inaweza ku trigger hilo tatizo

Tatizo una majibu yako, so endelea kuwaA unavyoona rahisi
 
Ukishajua ugonjwa wa marehemu itakusaidia nini kwenye SHIDA ZAKO?.
Kwa jamii iliyostaarabika ambayo kila wakati hujipanga kuzuia na kupambana na changamoto zote kwa ajili ya kesho iliyo bora zaidi kuliko leo na jana, ugonjwa au sababu ya kifo cha marehemu haiwezi kuwa siri. (Labda mkuu, ulimaanisha zile sera za Mrema).

Ndiyo maana huwa kuna autopsy, postmortem na hata inquests ilikujua sababu halisi ya kifo pasi na shaka yoyote..

Ikumbukwe kuwa kama ni sababu au ugonjwa, mbona unabakia kuwa ni huo huo uliomwua marehemu hata nani afanye je?

Hayo ndiyo mambo yake mola. Kazi yake haina makosa.

Apumzike kwa amani Jabari la Muziki.

Apumzike kwa amani mzee wetu rais mstaafu Mkapa.

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Cardial Arrest inakukuta uwe ama huna malaria. Na sometimes dawa kali zinaweza kuchangia cardial arrest.

Corona haina tabia ya kuua kirafiki kwamba utaongea na watu kisha unakufa gafla. Corona inakubana upumuaji kwa muda mrefu na mateso ya kupumua hayakupi nafasi ya kupiga hadithi.

Mitazamo tu ... am not mjuaji wala mtaalam
Hivi cardiac arrest huwa mgonjwa analazwa hospitali, anapiga stori na wanaomtembelea wee ndipo inamuua? Hapa kuna walakini. Itoshe tu kusema RIP Mkapa. Mambo mengine wanafamilia waendelee kuyafanya siri yao, wasiingie kwenye mtego wa kutuliza uvumi unaoendelea.
 
Wanabodi,
Kumbe sababu ya kifo cha Mpendwa wetu, Benjamin William Mkapa ni Cardiac Arrest!.

Asante sana Mwanafamilia wa familia ya Mkapa, William Erio, kuusema ukweli huu na kumaliza rasmi ile sintofahamu ya chanzo cha kifo, ambayo imezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo JF.

Kama Tangazo la kifo lingezingatia sheria tangu pale mwanzo, wala kusingetokea sintofahamu yoyote!.

Hivyo japo haijasemwa ni JF, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Japo yanalaumiwa kwa kuonekana watu wana mind vitu vidogo vidogo ambayo sio vya msingi, lakini yanasaidia.

Chanzo cha kifo cha ghafla cha any state leader ambaye hajawahi kutamkwa kusumbuliwa na maradhi yoyote, automatically kita send a shock wave kwenda viral.

Baada ya kauli hii, sasa minongo yote kuhusu chanzo cha kifo imemalizwa rasmi.
Naombeni sana, wanabodi, tuwe na heshima kwa viongozi wetu na tuwe na heshima kwa marehemu, mkiisha ambiwa ukweli wa familia, then tuupokee ukweli huu, tuuamini, na kumheshimu Marehemu kwa kuto toa comments zozote negative based on hisia!.

RIP, Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

Paskali
Mabandiko mengine ni ya kipuuzi kweli, kama hili hapa!
 
Back
Top Bottom