Wewe umezaliwa mwaka gani wewe hujui kuhusiana na masuala ya utani? Hilo vyula ni utani wa Jadi km ilivyokua Queens wakati Simba wanajiita Queens wakawa wanataniwa maana Queens ukiipeleeka kwenye Kiswahili maana yake ni Wanawake sasa klabu inajiita Queens na wanacheza wanaume wewe hapo unasemaje, tukija kwenye utani wa makolo kwa Simba na utopolo kwa Yanga (muasisi Haji Manara) hayo ni majina ya utani, vyula ni Jina la utani sababu uwanja wa Jangwani mvua ikinyesha panajaa na pale ndio kuna HQ ya Yanga na maji yakijaa hayakosi vyula ndio ukaanza utani wa vyula, sijui unanielewa na mautani mengine mengi tu yamepita hizi timu 2 ni timu zenye utani mwingi km makabila yanayoshabihiana lazima wataniane