Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Halafu tulipe. Mungu anakuona saa100
 
Kuna guarantee gani kuwa DP world wataweza kuongeza mapato!!?
 

Akisharudisha hela yake anawarudishia TPA?
Hiyo kitu iko wapi kwenye conditions na terms?
 

Akisharudisha hela yake anawarudishia TPA?
Hiyo kitu iko wapi kwenye conditions na terms?
 
SAS jmn tumsikilize Nani mbn kila upande una hoja zake
 
Sasa ulifikiri bandari yote ile imejengwa na nani< Waliaza Waarabu,wakaja Eajerumani, Wakaja Waingereza, Ikaja serikali ya Tanzania, wote wameijenga mpaka walivyofikia.



Unafikiri mkataba uliopo ni wa kujenga bandari? Huo kwa sasa hapa Dar hakuna, wa Dar ni wa kuendesha tu shughuli za makontena bandarini. Tena siyo bandari yote.

Bagamoyo, Tanga ndiyo mikataba yake ya brand new Bandari na uendeshaji.

Hawa labda mizigo ikizidi waingie mkataba mwengine wa kujenga, na hata wakijenga usifikiri kwa pesa zao, inakuwa ni grant tu. Maana yake kitachotumika kitarudishwa bila riba. Na huku kazi zinaendelea.

Ni kama ukodishe nyumba halafu wewe mpangaji uitengeneza na kuiboresha halafu mnakatiana kwenye kodi.

Hivi unafikiri DP World wana kazi ipi pale? Wao wanakodisha tu bandari wanailipia kodi. Na wao wanatukodisha huduma zao. Basi. Hakuna zaidi.
 
Mkataba wa IGA ni wa miaka mingapi?
Huu uliopo ni miezi 12 au chini ya hapo. Iwe tayari kuna mkataba wa HGA ambao huo sasa ndiyo utaainisha kila mradi utakuwa wa muda gani.

Soma kifungu cha 5:4
 
Huu uliopo ni miezi 12 au chini ya hapo. Iwe tayari kuna mkataba wa HGA ambao huo sasa ndiyo uytainisha kila mradi utakuwa wa muda gani.
Hiyo miezi 12 ni kwa mujibu wa mkataba au ni matamanio yako tu? Kifungu cha UKOMO kwenye huo mkatana kimesema ni miezi 12? Au we ymesoma mkataba wako na baba mwenyenyumba wako?
 
Wewe uko nchi gani ndugu?
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Kama kiongozi wa chini kashindwa Ina maana mkubwa wake kashindwa na mkubwa wa wote kwenye utendaji kwa njia hii ni Rais
 
Huo ndo ukweli na tatizo ni lipi waseme bayana siyo kuwa too general na kupotosha umma. Kama mtu hana capacity ya kuchambua hili bora kukaa kimya.

Tulishashindwa miaka kibao mpaka KAGAME alitucheka tukamjibu kwa kuwatimua Raia wa nchi yake.
Kagame aliwacheka raia au alimcheka Rais ili tujue tatizo liko wapi
 
Hiyo miezi 12 ni kwa mujibu wa mkataba au ni matamanio yako tu? Kifungu cha UKOMO kwenye huo mkatana kimesema ni miezi 12? Au we ymesoma mkataba wako na baba mwenyenyumba wako?
Kasome kifungu cha 5:4
 
Utakuta unaandika haya hata sehemu ya kulala hauna.
 
Upuuzi umeongea
 
Acha ujinga wewe, yaani watoke kwao kote huko ati waje kusaidia serikali yako ipate mapato? Mapato yaongezeke Kwa kiasi Gani na wao watakuwa wamechukuwa ngapi?
Hivi na hao TICS walitokea wapi? Kuja kuwekeza bandari? Mgekua mnayaweka wazi maana sisi wengine ma mbumbumbu
 
Akisharudisha hela yake anawarudishia TPA?
Hiyo kitu iko wapi kwenye conditions na terms?
Imesemwa mara kadhaa mkataba utaisha project activities/agreements. zitakapoisha.

Ila ana option ya kuomba kuongezewa muda, akikubaliwa huo sasa ni mkataba wa management tu, tofauti na mikataba ya mwanzo. Na si lazima TPA imwongezee muda.
 
Kasome kifungu cha 5:4
Pia kasome kile kifungu kinachosema mkataba ni hadi shughuli za kibandari zitakapokoma, sasa siju ni lini shughuli za kibandari ziliwahi kukoma hapa duniani. Na hairuhusiwi kujitoa kwenye mkataba, hata tukipigana nao vita, mkataba hauvunjiki, hata wakakiuka masharti ya mkataba, hauvunjiki.
 
kwa hiyo kwa lugha nyengine, ni kwamba tulikopa pesa world bank kuendeleza bandari ya DP WORLD? ila kulipa tutalipa sisi wananchi. is that what you mean?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ