Kumbe Tanzania siyo Maarufu kihivyo kama tunavyokaririshana

Wenyewe wanajua kuna nchi inaitwa afrika na mjii kuu wake ni South afrika.


.
hapa ndo umenifanya nikupuuze kuna kombe la dunia kila michuano nchi kibao za Africa huwa zinaingia kwenye michuano[/QUOTE]
ilikuwa kabla ya WC. Ila pia hata kama, kila sehemu kuna watu wenye uelewa na upenzi tofauti.Nasikia hata Beckaham aliwahi kwenda hollywood majamaa yakamshangaa ni nani tena huyu mbona hatumjui.

Suala nadhani tujitangaze. Tusashumu tunajulikana. Itakula kwetu. Unadhani kwa nini wakenya walipata ujasiri wa kutumia tununzetu kujiyangazia huko ulaya. Kwa sababu walijua Gianti kalala mkuu. Ni mwendo wa kutumia fulsa bila kumuamsha.
 



Karibuni nilisikia kuna nchi wamesema Tanzania kuna maasai na wanyama tu!
 
Karibuni nilisikia kuna nchi wamesema Tanzania kuna maasai na wanyama tu!
Hatarii.
hao kama niko huko nawala kelebu moja matata. na sisi tupo bwana.
Ila tujiuze kwa kujitangaza kwa Nguvu zote.
Nimeawahi kuona wikipedia jamaa ameandika ziwa Viktoria liko Nigeria. Baadae alibadilisha lakini.
sio fea.
 
Siwezi kuona ajabu ya hilo . Ishu ni kwamba hawakufundishwa historia ya dunia nzima tangu wakiwa wadogo.
Walisoma zaidi historia ya nchi zao.
Ndomana sisi wabongo tunajua miji mikuu ya nchi zote, tunajua denmark ni maarufu kwa kufuga ngombe, australua kondoo. Jikubali mzeee na Tanzania yetu kuwa mzalendo.
 
Sio ajabu. Watu wengi wa nje wanaifahamu Afrika.
Hata wewe hapo, Marekani ni muunganiko wa nchi kama 50 hivi. Lakini sidhani kama unazifahamu nchi zote zaidi ya Marekani kama Marekani.
Russia, ni muunganiko wa vi nchi vingi, ila sana sana wewe utakuwa unaifahamu Moscow.
China vile vile, ni muunganiko wa nchi nyingi but wewe utakuwa unaifahamu Shanghai na Hong Kong.
Ulaya pia sidhani kama unazifahamu nchi zote. Kuna nchi ukitajiwa majina unabaki unashangaa!
 
mkuu shule ya msingi mwalimu Tofiki alinisababishia kujua dunia kama mitaa ya kariakoo.
ukiniamsha hata usiku ntakwambia Burma mji mkuu uko wapi, wanafanya nini kiuchumi, majirani zake ni wakina nani. siku hizi inaitwa Myanmar.
 
Wee mwenyewe hapo ulipo kuna wilaya za hapa Tanzania hata hujui ziko mkoa gani?
Kwa mfano nikikuuliza wilaya ya Mbogwe, Itimila hata hujui zilipo na uko hapa hapa Tanzania, sembuse wazungu huko ulimwengu wa juu !!!
Sababu zipo vijijini/chaka nizijue za nini.
Ndio maana hata wao hawawezi wakazifahamu nchi ambazo zinafanana na kiji*
 
Da, Zanzibar walifahamikaje mkuu. au sultani anamkono wake. kwa nini sisi tunakuwa wa mwishomwisho tu.
Kile kisiwa kinatembelewa na watalii wengi sana toka duniani kote na wanapokuwa hapo ndipo hukodi ndege kwenda kwenye hifadhi zetu za Wanyama na kurudi kwenye mahoteli ya fukwe Zanzibar, kama wiki mbili zilizopita kuna dada mmoja raia wa Botswana ameolewa na Mromania mmoja walikuja huko Zanzibar basi nikwambia utaenda kutembea mainland Tanzania akashangaa sana na kusema ni wapi huko!!
 
Pia kuna watanzania kibao hawajui pia Bolivia iko wapi au nini. Kutokujua sehem nadhani ni ujinga wa mtu mwenyewe maana hufungwi kujua sehemu yeyote hapa dunian hata kwa kutumia Atlas.
 
Sioni la ajabu hata hapa tu nchini watu hawapafahamu kwingine..

Kwa wao kufika huko na kujiongelea ndio wamechangia kuwafahamisha walioongea nao. Kesho kutwa wakikutana na Mtanzania mwingine atasema wanaijua nchi yetu..

Vitu vingine vinashangaza kuvisikia kama vile tumeajiri ndege wa angani warukao watutangazie nchi yetu..
 
Wawe wanajitambulisha kuwa watokea nchi ambapo maalbino wanauawa
 
Basi hao watu ni wajinga sana,ina maana hata elimu ya jiographia hawana....kweli ulaya kuna wajinga wengi.... nenda tz muulize mtoto yyte wa darasa la sita Panama ipo wp? ama Kisiwa cha Cyprus watakwambia....
 
Mimi binafsi nimewahi kutana na watasha kibao Tanzania hawaijui...
kweli mkuu, masikini inabidi ukomae ujipendekeze na kujitangaza, ukisubiri ujulikane automatic utangoja sana.
 
Basi hao watu ni wajinga sana,ina maana hata elimu ya jiographia hawana....kweli ulaya kuna wajinga wengi.... nenda tz muulize mtoto yyte wa darasa la sita Panama ipo wp? ama Kisiwa cha Cyprus watakwambia....
wanaangalia penye maana. Kuna shemu hata usipopajua hupati shida.
Jiografia ya afrika na tanzania ilikuwa muhimu kwa mababu zao enzi wanatafuta rasilimali.
sasa hivi wanalia kivulini.
Tujitahidi kujitangaza na kujipendekeza ni aibu wakati mwingine. Kufa maskini na dhahabu mfukoni kisa hakuna anayejua kama unayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…