Kumbe tunahesabu awamu za Serikali bila kuwa na sheria au utaratibu maalum unaotuongoza? Si muhimu sasa kuweka utaratibu rasmi?

Determinant factor hapa ni rasi, hivyo makamu wa raisi atabadilika jina kulingana na raisi aliyepo. Ndio maana Mapngo ni makamu wa raisi wa awamu ya sita. Makamu wa raisi wa awamu ya tano alikuwa na raisi wa awamu hiyo.
 
Samia hataweza kugombea vipindi vitatu sababu amerithi awamu ya pili ya utawala wa raisi wa tano kwa zaidi ya miaka mitatu, ila kama angerithi kwa chini ya miaka mitatu angeweza kugombea mara mbili na angeweza kuwa raisi kwa zaidi ya miaka 10+.

Hii ndio inaipa nguvu Ibara ya 37(5) na hoja ya jamaa kuwa utawala wa raisi wa 5 bado haujaisha zaidi umerithiwa na raisi wa 6, labda tuseme Samia ni raisi wa 6 wa JMT aliyerithi awamu ya pili ya raisi wa 5 wa JMT
 
Kwenye kumalizia muda wa mtangulizi Katiba haijataja muda uliobaki ila imeenda kutaja mambo ya muda uliobaki kwenye ishu za mrithi kutaka kugombea ndio hayo ya miaka zaidi ya mitatu kugombea kwa awamu moja ya miaka 5.
... by implication, kwa kuwa amenyimwa kugombea mara mbili maana yake kipindi chake cha kwanza kilishapita.
 
Rais angejiuzuru aliyepokea angekua bado awamu wa tano...

Ila Rais alifariki ndiyo maana...
Katiba imetaja mambo manne
1. Kufariki
2. Kujiudhuru
3. Kushindwa kumudu majukumu
4. Kupoteza sifa

Atakayeingia kushika nafasi kukitokea hayo atakuwa anatekeleza awamu ya aliyetoka
 
Hatujafanya uchaguzi.Baraza la mawaziri halijavunjwa.Hii ni awamu ya tano kipindi cha pili.Ni awamu ya Mwendazake ambayo ni extended to Samia
 
Hiyo awamu ya sita inatumia ilani ya wapi?ya mwaka gani na chama gani?
 
No. Amechukuwa awamu ya Magufuli anamalizia japo ni rais kamili. Tulifanya ''uchaguzi'' wa kutafuta serikali ya awamu ya tano, na ndiyo iliyoko bado madarakani. Awamu nyingine inaanza 2025.
Hii awamu bana inachekesha.inatumia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 ambayo ilikuwa awamu ya tano na bado inajiita awamu ya sita!!hahahaaaa
 
Ilani ndicho kigezo cha kuamua awamu?
Awamu inaongoza kwa kufuata ilani ya uchaguzi .sasa sijui awamu ya sita inatumia ilani gani ya uchaguzi?? Katiba inabidi itueleze.
 
Awamu inaongoza kwa kufuata ilani ya uchaguzi .sasa sijui awamu ya sita inatumia ilani gani ya uchaguzi?? Katiba inabidi itueleze.
... ni Katiba ipi au sheria ipi inasema hivyo? Kwamba kigezo cha awamu ni ilani ya uchaguzi? Utawala wa Nyerere wa miaka 24 ulipitia chaguzi ngapi? Ulinadi ilani ngapi? Mwinyi naye? Ilani ngapi? Mkapa? Kikwete? Kwa kigezo chako cha ilani kuna awamu ngapi hapo? Kubalini kwamba hili suala lina utata.
 
Mfumo wa makamu kupendekezwa na mgombea mkuu unamnyima power makamu kiutendaji
 
Wabongo wanaongoza kwa kujadili mada useless kabisa
 
Ndio maana tunataka Katiba Mpya
 
Siyo kweli kwa sababu ilani ya uchaguzi inayotumika ni ya awamu ya tano
Hakuna ilani ya awamu ya sita.
Awamu ni kipindi alichohudumu rais sio miaka kwahiyo awamu ya Magufuli iliisha pale alipofariki hivyo Rais Samia hamalizii awamu ya yeyote bali ni yake.
 
Wanajifanya hawaelewi!
 
Hakuna kitu kama hicho, umepotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…