Kumbe tunahesabu awamu za Serikali bila kuwa na sheria au utaratibu maalum unaotuongoza? Si muhimu sasa kuweka utaratibu rasmi?

Kumbe tunahesabu awamu za Serikali bila kuwa na sheria au utaratibu maalum unaotuongoza? Si muhimu sasa kuweka utaratibu rasmi?

Determinant factor hapa ni rasi, hivyo makamu wa raisi atabadilika jina kulingana na raisi aliyepo. Ndio maana Mapngo ni makamu wa raisi wa awamu ya sita. Makamu wa raisi wa awamu ya tano alikuwa na raisi wa awamu hiyo.
Mimi nafikiri hivi,
Rais na makamu wa Rais ni pacha, ndio maana wanagombea pamoja.
Katiba inampa mamlaka makubwa Pacha wa kwanza na mamlaka madogo pacha wa pili,
Mathalani akifa makamu wa Rais, makamu atakayemrith hawezi kuwa Makamu wa Awamu ya sita atakuwa chini ya Rais wa Awamu ya tano,
Sasa amekufa Rais wa awamu ya Tano maana yake Makamu wa awamu ya Tano ndio anakuwa Rais wa awamu hiyo, kumalizia muda uliobakia, Japo kwa namba anakuwa Rais wa Sita.
 
Kwa akili ya kawaida ukifanya hivyo maana yake unampa nafasi yule anayeshika kiti cha urais kugombea awamu tatu jambo ambalo si sawa.Hivyo katiba imeweka wazi ili anayeshika kiti cha urais baada ya mtangulizi kufariki atanbue kabisa kuwa yupo na awamu mbili tu
Samia hataweza kugombea vipindi vitatu sababu amerithi awamu ya pili ya utawala wa raisi wa tano kwa zaidi ya miaka mitatu, ila kama angerithi kwa chini ya miaka mitatu angeweza kugombea mara mbili na angeweza kuwa raisi kwa zaidi ya miaka 10+.

Hii ndio inaipa nguvu Ibara ya 37(5) na hoja ya jamaa kuwa utawala wa raisi wa 5 bado haujaisha zaidi umerithiwa na raisi wa 6, labda tuseme Samia ni raisi wa 6 wa JMT aliyerithi awamu ya pili ya raisi wa 5 wa JMT
 
Kwenye kumalizia muda wa mtangulizi Katiba haijataja muda uliobaki ila imeenda kutaja mambo ya muda uliobaki kwenye ishu za mrithi kutaka kugombea ndio hayo ya miaka zaidi ya mitatu kugombea kwa awamu moja ya miaka 5.
... by implication, kwa kuwa amenyimwa kugombea mara mbili maana yake kipindi chake cha kwanza kilishapita.
 
Rais angejiuzuru aliyepokea angekua bado awamu wa tano...

Ila Rais alifariki ndiyo maana...
Katiba imetaja mambo manne
1. Kufariki
2. Kujiudhuru
3. Kushindwa kumudu majukumu
4. Kupoteza sifa

Atakayeingia kushika nafasi kukitokea hayo atakuwa anatekeleza awamu ya aliyetoka
 
Kifo cha Magufuli kimethibitisha pasipo shaka kuwa sisi kama nchi hatuna utaratibu wowote rasimi wa kikatiba, kisheria au usio wa kisheria unaotuongoza katika kuhesabu au kuzitambua awamu za serikali.

Kama utaratibu rasimi huo, basi ni wazi hauleweki na unapaswa kutazamwa upya ili kuondoa huu mkanganyiko unaojitokeza sasa tena ukiwahusisha viongozi wakubwa tu katika nchi yetu.

Hivyo, tunapaswa kuwa na utaratibu unaotamka rasimi kama awamu ya serikali inahesabiwa pale anapoingia Raisi mpya hata ikitokea Raisi aliepo madarakani anafariki na kurithiwa na makama wake au vinginevyo. .

Tujiulize, ikitokea tunapata Raisi mwingine kutokana na sababu zilizoainishwa na katiba yetu, Raisi huyo atakuwa ni wa serikali ya awamu ya tano, ya sita at saba?

Kwakuwa hatuna utaratibu unaoeleweka, hata awamu ya Nyerere inaweza isiwe ni awamu ya kwanza kwani zilikuwepo serikali za kikoloni kabla ya Nyerere kuwa Raisi.

Tujifunze kutokana na makosa kwa kuupatia suluhisho huu mkanganyiko uliopo sasa.

Kama ambavyo mikutano ya Bunge na vikao vyake viko well defined, basi na hizi awamu pamoja na chaguzi zake ziwe well defined.
Hatujafanya uchaguzi.Baraza la mawaziri halijavunjwa.Hii ni awamu ya tano kipindi cha pili.Ni awamu ya Mwendazake ambayo ni extended to Samia
 
Hiyo awamu ya sita inatumia ilani ya wapi?ya mwaka gani na chama gani?
 
No. Amechukuwa awamu ya Magufuli anamalizia japo ni rais kamili. Tulifanya ''uchaguzi'' wa kutafuta serikali ya awamu ya tano, na ndiyo iliyoko bado madarakani. Awamu nyingine inaanza 2025.
Hii awamu bana inachekesha.inatumia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 ambayo ilikuwa awamu ya tano na bado inajiita awamu ya sita!!hahahaaaa
 
Ilani ndicho kigezo cha kuamua awamu?
Awamu inaongoza kwa kufuata ilani ya uchaguzi .sasa sijui awamu ya sita inatumia ilani gani ya uchaguzi?? Katiba inabidi itueleze.
 
Awamu inaongoza kwa kufuata ilani ya uchaguzi .sasa sijui awamu ya sita inatumia ilani gani ya uchaguzi?? Katiba inabidi itueleze.
... ni Katiba ipi au sheria ipi inasema hivyo? Kwamba kigezo cha awamu ni ilani ya uchaguzi? Utawala wa Nyerere wa miaka 24 ulipitia chaguzi ngapi? Ulinadi ilani ngapi? Mwinyi naye? Ilani ngapi? Mkapa? Kikwete? Kwa kigezo chako cha ilani kuna awamu ngapi hapo? Kubalini kwamba hili suala lina utata.
 
ukweli ni kwamba samia anaongoza awamu ya tano siyo ya sita. Kungeitishwa uchaguzi mkuu baada ya JPM kufariki ndipo tungesema tuko awamu ya sita. Hata waziri mkuu wake ni yule yule wa awamu ya tano na wala hakutangaza kuvunja baraza lote la mawaziri akaunda jipya. Alikubali kurithi la awamu ya tano akafanya marekebisho madogo tu kuwaondoa asiowapenda hasa wasukuma.

Kusema hii ni awamu ya sita ni janja ya kukwepa failures za kipindi cha JPM akiwa rais na Samia akiwa Makamu.
Mfumo wa makamu kupendekezwa na mgombea mkuu unamnyima power makamu kiutendaji
 
Wabongo wanaongoza kwa kujadili mada useless kabisa
 
Kifo cha Magufuli kimethibitisha pasipo shaka kuwa sisi kama nchi hatuna utaratibu wowote rasimi wa kikatiba, kisheria au usio wa kisheria unaotuongoza katika kuhesabu au kuzitambua awamu za serikali.

Kama utaratibu rasimi huo, basi ni wazi hauleweki na unapaswa kutazamwa upya ili kuondoa huu mkanganyiko unaojitokeza sasa tena ukiwahusisha viongozi wakubwa tu katika nchi yetu.

Hivyo, tunapaswa kuwa na utaratibu unaotamka rasimi kama awamu ya serikali inahesabiwa pale anapoingia Raisi mpya hata ikitokea Raisi aliepo madarakani anafariki na kurithiwa na makama wake au vinginevyo. .

Tujiulize, ikitokea tunapata Raisi mwingine kutokana na sababu zilizoainishwa na katiba yetu, Raisi huyo atakuwa ni wa serikali ya awamu ya tano, ya sita at saba?

Kwakuwa hatuna utaratibu unaoeleweka, hata awamu ya Nyerere inaweza isiwe ni awamu ya kwanza kwani zilikuwepo serikali za kikoloni kabla ya Nyerere kuwa Raisi.

Tujifunze kutokana na makosa kwa kuupatia suluhisho huu mkanganyiko uliopo sasa.

Kama ambavyo mikutano ya Bunge na vikao vyake viko well defined, basi na hizi awamu pamoja na chaguzi zake ziwe well defined.
Ndio maana tunataka Katiba Mpya
 
Siyo kweli kwa sababu ilani ya uchaguzi inayotumika ni ya awamu ya tano
Hakuna ilani ya awamu ya sita.
Awamu ni kipindi alichohudumu rais sio miaka kwahiyo awamu ya Magufuli iliisha pale alipofariki hivyo Rais Samia hamalizii awamu ya yeyote bali ni yake.
 
... ni Katiba ipi au sheria ipi inasema hivyo? Kwamba kigezo cha awamu ni ilani ya uchaguzi? Utawala wa Nyerere wa miaka 24 ulipitia chaguzi ngapi? Ulinadi ilani ngapi? Mwinyi naye? Ilani ngapi? Mkapa? Kikwete? Kwa kigezo chako cha ilani kuna awamu ngapi hapo? Kubalini kwamba hili suala lina utata.
Wanajifanya hawaelewi!
 
Samia ni Raisi wa Sita wa Tanzania anayetawala katika awamu ya tano ya utawala.wa hii nchi awamu kwa tafsiri ya kimantiki ni kipindi cha uongozi wa sarikali (naomba tusitumia tafsiri ya uchanguzi ama kuhesabu namba ya viongozi) kwani Kwa dhana ya uchaguzi Nyerere na Mwinyi hawakuchaguliwa na wananchi hivyo dhana idadi au namba haina mashiko
Hivyo Nyerere ni Raisi wa awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi iliyodumu kwa miaka 21, mwinyi ni Raisi wa awamu ya pili ya uongozi iliyodumu kwa miaka 10 kama ilivyokuwa kwa awamu ya tatu na awamu ya nne Zilizongozwa na Mkapa na Kikwete mpaka kufikia kwa Raisi wa tano aliyeongoza awamu ya Tano ya serikali ya hii nchi

Na hapa ndipo likaja swala la Samia katiba iko wazi kuwa makamu wa Raisi huwa mgombea mwenza hii inamaanisha hushirikiana na mgombea wa nafasi ya uraisi kuunda serikali majukumu yake pamoja na mengine ni kushika nafasi ya raisi anapokuwa hawezi kufanya majukumu yake na hasa kuwa raisi pale raisi anapofariki ....

Naomba nigusie kidogo swala la serikali kuundwa kwa mujibu wa katiba yetu raisi huunda(huunda sio hubadili) baraza la.mawaziri kwa kuanza na waziri mkuu na hii hutokea baada ya uchaguzi mkuu na ikitokea Raisi akalivunja baraza la mawaziri italazimu kuitishwa kwa uchaguzi ......

So far kwa ubora wa uelewa wangu Samia ni Raisi wa Sita Wa Tanzania katika awamu ya Tano ya uongozi wa serikali ya JMT siku akichaguliwana wananchi au akivunja serikali au akifanya.mageuzi na kuunda serikali yake mpya atakuwa raisi wa sita wa Tanzania katika awamu ya sita
Hakuna kitu kama hicho, umepotoka.
 
Back
Top Bottom