Kumbe Urusi ililenga silaha za NATO zilizohifadhiwa karibu na makazi ya watu? Nani alaumiwe hapa

Kumbe Urusi ililenga silaha za NATO zilizohifadhiwa karibu na makazi ya watu? Nani alaumiwe hapa

Kikosi cha Wanaanga cha Urusi kilianzisha shambulizi la anga la "usahihi wa hali ya juu" dhidi ya hifadhi za ndege za Ukraine zilizokuwa na silaha na risasi katika eneo la kati la Poltava siku ya Jumatatu, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema jana (Jumanne).

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, shambulizi hilo lililolenga silaha zilizotolewa na Marekani na nchi za Ulaya, lilitekelezwa kwa silaha za usahihi wa hali ya juu za vikosi vya anga vya Urusi na makombora ya Kalibr. Shambulizi hilo liliharibu silaha na zana zilizotengenezwa Magharibi ambazo zingewasilishwa kwa wanajeshi wa Ukraine huko Donbass, iliongeza.

"Ulipuaji wa risasi zilizohifadhiwa ulisababisha moto katika kituo cha ununuzi kisichofanya kazi karibu na vifaa vya mtambo huo," wizara ilisema. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kwenye Telegram kwamba shambulizi hilo liligonga jumba la maduka liliokuwa na zaidi ya watu 1,000 ndani.
Pro Russia sijui mnawaza kutumia nini siraha zipo kwenye majumba ya watu
Screenshot_2022-06-30-16-47-00-054_com.gbinsta.android.jpg
 
Pro Russia sijui mnawaza kutumia nini siraha zipo kwenye majumba ya watu View attachment 2277512
Huu ndio ushahidi umemaliza
Huu ndio wakati sahihi sasa wa NATO kwenda kulinda RAIA hapo UKRAINE kama walivyoenda kufanya kule LIBYA
RUSSIA kama TAIFA TEULE itapiga popote panapofuka moshi hatakama patakua WODINI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom