Kumbe Waarabu walikuwa watu wabaya kiasi hiki, yadumu mapinduzi matukufu ya Zanzibar

Acha upumbavu sasa.Umekuwa mtu mzima unajua?
 
Basra, Iraqi
Many of them are descendants of African slaves brought to Iraq. Many Iraqis still refer to them by their ancestral name, abeed - meaning slaves.
 
Mkuu, hakujawahi kuwa na utumwa mzuri, uwe umefanywa na mweusi, mwarabu au mzungu.

Mkuu hii paragraph iwe rejea muhimu wakati tukichangia mada hii, maana inatuongoza vizuri katika mjadala huu juu ya historia. Na historia inatuongoza tusirudie makosa kuamini kuna utumwa, ukoloni au ubaguzi ulio mzuri.
 
Mkuu, Oman is a mixed race community tofauti na nchi nyingi za kiarabu. Nafurahia sana kuona waarabu na waafrika wanaaishi vizuri kwa amani. Hili ni jambo jema sana machoni kwa mwenyezi Mungu. Binafsi napenda kuona Oman na Tanganyika tunaishi kwa upendo kwasababu tuna undugu wa muda mrefu (Hatujakutana Barabarani) ambao uko kwenye damu na siyo siasa. Tunazungumza hadi lugha moja, jambo ambalo siyo dogo na la kupuuzwa......

Japo, ili uhusiano wetu uwe imara na makosa kama haya yasijirudie katika vizazi vijavyo ni lazima tukiri ukweli kwamba biashara ya utumwa ilifanywa baina ya machifu wa kiafrika pamoja na waarabu. Ushahidi mkubwa upo na mikataba hiyo baina ya Masultani wa Zanzibar na Waingereza kuhusu utumwa upo. Mimi binafsi nimeona nyaraka za Ministry of Foreign Affairs zikionyesha Sultan wa Zanzibar akilalamika kwanini hakuhusishwa kwenye mkutano wa Berlin 1884-1885, ambao uligawa Afrika.

Aliwaandikia Waingereza na Wajerumani barua (Diplomatic Note) kusema kwamba majimbo ya Arusha (Aruscha) na Moshi (Moschi) yalikuwa chini ya utawala wa Sultan wa Zanzibar, kwasababu machifu wa Kaskazini walikubaliana iwe hivyo. Mambo kama haya yasipowekwa wazi kisa hofu ya kuwakwaza baadhi ya watu, basi nadhani tutakuwa tunayaweka mahusiano baina ya Tanganyika, Zanzibar na Oman kwenye ukurasa mbaya.

Kile kilichotokea mwaka 1964 kikifanywa na wakina Mzee Nyerere, Karume, Okello na Kambona kilikuwa ni mauaji ya kimbari (Genocide), pia kilichofanywa na Mzee Mkapa mwaka 2001 kule Pemba nacho kilikuwa ni mauji ya kimbari (Genocide). Hata Mzee Nyerere alijutia kabla hajafariki, na Mzee Mkapa naye amejutia. Hakuna kutetea, wala kupunguza uzito wa kilichofanyika, iwe kilifanywa na mweusi au mwarabu. Udhalimu dhidi ya binadamu mwenzako kwasababu ya rangi au dini ni tabia ya kishenzi na kishetani.

Sasa, tusipokuwa wawazi na kutafuta suluhu nadhani haya mambo hayawezi kuisha vizuri. Mpaka leo hii, Muungano unasumbua, chanzo siyo siasa bali ni HISTORIA YA MUDA MREFU, ambayo ndani yake kuna Uarabu, Uafrika, Utumwa, Uislamu na Ukristo.....

WE CALL A SPADE, A SPADE......
 
Basra, Iraqi
Many of them are descendants of African slaves brought to Iraq. Many Iraqis still refer to them by their ancestral name, abeed - meaning slaves.
Hawa weusi (Bantus) ndiyo walianzisha The Zanj Rebellion dhidi ya Abbasid Caliphate mwaka 869.
 
Wote tu waliku wa ovyo....huko kwa wazungu walisitisha biashara ya utumwa baada ya mapinduzi ya viwanda, walikuja kua na mashine zinazowasaidia kwenye uzalishaji kwa gharama nafuu kwahio hawakua na nia tena na watumwa ,kikubwa walitaka wanabaki kwenye maeneo yao ili wawe soko la bidhaa zao na kuwazalishia malighafi za viwanda vyao.......hakuna mwema hapo kila mtu alifanya maamuzi yake tokana na maslahi yake hakuna aliempenda mtu mweusi, mzungu kamaliza utumwa ila akaja kukutawala hukuhuku kwenye nchi yako na hii ilitokea baada ya mapinduzi ya viwanda
 
Baada ya kupakwa futa la mawese ......umeanza kusifia shughuli Yao......daaa aiseee waswahili mna kazi
 
Uarabu una definition nyingi it depend unatumia definition ipi.

Mkuu Hao walioishi na waarabu hawakugombana nao, kila siku Nasema humu the way wazee wetu wa kiarabu walivyoishi unakuta Mmoja anaishi kijiji hiki, mwengine anaishi kijiji kingine, tofauti na Wahindi na wazungu waarabu si watu wa mjini utawakuta mashambani huko wanafanya biashara na kulima minazi, Kama kweli wangekuwa wanafanya vitu against wazawa, wanawatesa na Kuwanyanyasa why wadumu maelfu ya miaka? Kwanini hawajapigana vita ya mara kwa mara kama Wareno ama wajerumani?

Historia ipo ila Tunataka tu kuifumbia macho tutafute ng'ombe Wa kafara.

Hio link sijafahamu niangalie nini Nimesema ni mambo ya kawaida tu.
 
Amani Mkuu, nimefurahi kuongea na wewe, na nakubaliana na ulichoandika.
 
Maandishi yalosema binadamu wa kwanza alikuwa nyani unapaswa kuyachunguza ili kuyaamini hata yakisemwa bahari ina maji ya chumvi
 
waarabu hawakugombana nao, kila siku Nasema humu the way wazee wetu wa kiarabu walivyoishi unakuta Mmoja anaishi kijiji hiki,

Hata kule Afrika ya Kusini wapo waafrika ya kusini weupe wakati wa ubaguzi waliishi vizuri na wabantu na kujiunga siasa ktk vyama vya ANC, PAC, Communist party of South Afrika. Baadhi ya Waafrika ya Kusini weupe walichukizwa na siasa za kibaguzi na wala hawakuona ni sahihi kuwabagua waafrika wenzao kwa kutumia rangi.


Kwa Zanzibar pia kuna waarabu wazanzibari walijiunga na UMMA Party, ASP kwa kuwa waliona sera za usawa zisizojali rangi zilikuwa nzuri kwa mustakabali wa nchi yao Zanzibar.

Ma comrade wa UMMA party Zanzibar bila kujali rangi, nasaba n.k waliunda chama kilichopinga uonevu bila kujali rangi

Comrade Ali Issa Sultani a.k.a Shetani, mwanamapinduzi wa Zanzibar aliyataka usawa kwa wote.

Mapinduzi Daima – Revolution Forever: Using the 1964 Revolution
in Nationalistic Political Discourses in Zanzibar . Source :


Joe Slovo muafrika wa kusini mweupe aliyepinga sera za kibaguzi Afrika ya Kusini

Joe Slovo
Former Minister of Human Settlements of South Africa


Joe Slovo was a South African politician, and an opponent of the apartheid system. A Marxist-Leninist, he was a long-time leader and theorist in the South African Communist Party, a leading member of the African National Congress, and a commander of the ANC's military wing Umkhonto we Sizwe
 
Ila South Africa kulikua na vita na resistance za kutosha, zilikuwepo hio miaka elfu ya waarabu pwani?

Even ukisoma Historia ya Kilwa mfalme hakuwa akiongoza makabila ya Africa bali ulikua tu ni kama umoja.
1. Aliinunua Kilwa toka kwa Mfalme Almuli (na sio kuvamia)
2.maeneo mengi ambayo Sultan aliongoza kulikuwa na mutual agreement na sultan aliweka tu ambasador wake, maeneo husika yalikuwa na Full Authority kujiongoza yenyewe.
3. Ilifanyika biashara kwamba kuna kuuza na kununua na sio kama ukoloni ambaye mfaidikaji alikua ni mmoja.

Kuna mambo mengi ya kuongelea ila kufananisha wazungu wa south na waarabu wa pwani ya Africa ni mbingu na ardhi.
 
Wanamapinduzi wa kiZanzibari waliokataa utumwa, Ukoloni, ubaguzi na usultani


Badawi Qullatein zama za uhai wake.
 
Ok
 
Wanamapinduzi wa kiZanzibari waliokataa utumwa, Ukoloni, ubaguzi na usultani


Badawi Qullatein zama za uhai wake.
Kulikuwa na wapinga serikali zanzibar ni tofauti na mapinduzi. Walikuwepo watu wanaopinga serikali kama vile ambavyo leo kuna Chadema wanaopinga CCM.

Ila kuhalalalisha mauaji ya maelfu ya watu wasio na silaha kwa sababu tu ya rangi yao ni jambo jengine, mkuu MALCOM LUMUMBA ameliongelea vizuri hapo juu.
 
Sheikh Ali Muhsin Barwani aelezea Hizbu kukataa ubaguzi miaka ya mwisho ya 1950 kuelekea uchaguzi 1961


Hizbu na harakati za kuwaunganisha watu wote Zanzibar wawe kitu kimoja, maana kulikuwa na mgawanyiko mganzija, bohora, shirazi, watumbatu, mzanzibara n.k

Pia Mzee Barwani anatupa chimbuko la Afro Shirazi na anakubali utumwa ulikuwepo kote, utumwa ulikuwepo mpaka 1920. Donda hili la utumwa, Hizbu walitaka kuliondoa maana 2/3 ya watumwa walishikiliwa na washirazi huku waarabu wakiwa 1/3 wakishikiliwa na waarabu anabainisha Mzee Barwani .

Source : MzeeBarwani
 
Usichokijua ni kuwa utumwa ulikuwa ni mfumo kamili wa maisha duniani kote kwa nyakati tofauti. Tumesoma kwenye historia kidato cha tatu kuwa hata huku kwetu Afrika Mashariki kulikuwa na slave owning societies mfano mmojawapo ni Wanyakyusa. Hata Ulaya kulikuwa na utumwa na ndiyo maana Roxelana (Hurrem Sultan) alitekwa kwao Poland kama mtumwa na Wazungu wenzie akaja kuuzwa Constantinople akanunuliwa na Sultan Suleyman Khan wa Ottoman Empire na akamuoa. Wazungu ndio walioleta biashara ya utumwa Afrika japo utumwa ulikuwepo Afrika kabla ya hiyo biashara na walishirikiana na Machifu wa Kiafrika. Wareno wamefanya sana hiyo biashara kule Msumbiji na Angola.

Pia, sijui yule aliyemuuza Yusufu utumwani Misri naye ni Mwarabu? Chuki za kidini zisiwafanye mjitoe ufahamu. Nenda pale UDSM Library upande wa Special Reserve kuna encyclopedia kibao za slave trade zitakusaidia kutanua uelewa wako kwenye haya mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…