Kumbe Waarabu walikuwa watu wabaya kiasi hiki, yadumu mapinduzi matukufu ya Zanzibar

Kumbe Waarabu walikuwa watu wabaya kiasi hiki, yadumu mapinduzi matukufu ya Zanzibar

Hizi ni poropaganda na fitna tu. Waarabu hawakuwa na tatizo na waafrika. Walitupenda sana na tuliishi nao kwa amani na upendo. Hizi mnaleta ni chuki tu..hata mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni chuki tu dhidi ya waarabu. Mtapata laana kubwa kuwa singizia waarabu. Hawana baya kabisa na watu.
Acha upumbavu sasa.Umekuwa mtu mzima unajua?
 
Basra, Iraqi

Many of them are descendants of African slaves brought to Iraq. Many Iraqis still refer to them by their ancestral name, abeed - meaning slaves.
 
Mkuu, hakujawahi kuwa na utumwa mzuri, uwe umefanywa na mweusi, mwarabu au mzungu.

Mkuu hii paragraph iwe rejea muhimu wakati tukichangia mada hii, maana inatuongoza vizuri katika mjadala huu juu ya historia. Na historia inatuongoza tusirudie makosa kuamini kuna utumwa, ukoloni au ubaguzi ulio mzuri.
 
Mkuu mimi ni mwarabu na ni mu oman, Familia zetu wote hukosi watu weusi, tu naona na tunakaa pamoja, huo ubaguzi munauona Nyie. Njoo Tanga uone Familia za Ki oman zilivyomix rangi.

Oman ni nchi ya mixed race mamia ya miaka, watu weusi na waarabu wana exist pamoja that's why unakuta hadi royal family imeathirika hivyo.

Na Hakuna ubaguzi mbaya Mkuu kama systematic/institutional racism, Hao watu weusi walipata hizo nafasi uarabuni sababu mwarabu haamini doctor mweusi ni mbaya ama engineer mweusi hana uwezo kuliko mzungu etc. Ndio maana utakuta Qatar leo wanaenda kucheza World cup 2022 karibia nusu ya wachezaji ni WA Africa. Wangekuwa na systematic racism wangejaza wa Brazil kibao ila wamechukua WA Africa wadogo na kuwakuza.

At same time hizo nchi munazoona zimestaarabika zimejaa institutional racism.

Kuhusu hivyo vita Mkuu vina siasa na uisilamu, kihistoria dola ya kiisilamu Ile pure kabisa iliisha kwa Khalifa wa 4 yaani Alli, waliofuatia kama Umayyad caliphate even scholars wa kiisilamu utaona wana Criticize, na si Viongozi wote walikuwa ni wazuri, mfano Yazid kiongozi wa Umayyad alimuua mjukuu wa mtume, so mambo hayakuwa black and white, kuna complication nyingi na fitnah nyingi, si kila vita ni ya kidini.
Mkuu, Oman is a mixed race community tofauti na nchi nyingi za kiarabu. Nafurahia sana kuona waarabu na waafrika wanaaishi vizuri kwa amani. Hili ni jambo jema sana machoni kwa mwenyezi Mungu. Binafsi napenda kuona Oman na Tanganyika tunaishi kwa upendo kwasababu tuna undugu wa muda mrefu (Hatujakutana Barabarani) ambao uko kwenye damu na siyo siasa. Tunazungumza hadi lugha moja, jambo ambalo siyo dogo na la kupuuzwa......

Japo, ili uhusiano wetu uwe imara na makosa kama haya yasijirudie katika vizazi vijavyo ni lazima tukiri ukweli kwamba biashara ya utumwa ilifanywa baina ya machifu wa kiafrika pamoja na waarabu. Ushahidi mkubwa upo na mikataba hiyo baina ya Masultani wa Zanzibar na Waingereza kuhusu utumwa upo. Mimi binafsi nimeona nyaraka za Ministry of Foreign Affairs zikionyesha Sultan wa Zanzibar akilalamika kwanini hakuhusishwa kwenye mkutano wa Berlin 1884-1885, ambao uligawa Afrika.

Aliwaandikia Waingereza na Wajerumani barua (Diplomatic Note) kusema kwamba majimbo ya Arusha (Aruscha) na Moshi (Moschi) yalikuwa chini ya utawala wa Sultan wa Zanzibar, kwasababu machifu wa Kaskazini walikubaliana iwe hivyo. Mambo kama haya yasipowekwa wazi kisa hofu ya kuwakwaza baadhi ya watu, basi nadhani tutakuwa tunayaweka mahusiano baina ya Tanganyika, Zanzibar na Oman kwenye ukurasa mbaya.

Kile kilichotokea mwaka 1964 kikifanywa na wakina Mzee Nyerere, Karume, Okello na Kambona kilikuwa ni mauaji ya kimbari (Genocide), pia kilichofanywa na Mzee Mkapa mwaka 2001 kule Pemba nacho kilikuwa ni mauji ya kimbari (Genocide). Hata Mzee Nyerere alijutia kabla hajafariki, na Mzee Mkapa naye amejutia. Hakuna kutetea, wala kupunguza uzito wa kilichofanyika, iwe kilifanywa na mweusi au mwarabu. Udhalimu dhidi ya binadamu mwenzako kwasababu ya rangi au dini ni tabia ya kishenzi na kishetani.

Sasa, tusipokuwa wawazi na kutafuta suluhu nadhani haya mambo hayawezi kuisha vizuri. Mpaka leo hii, Muungano unasumbua, chanzo siyo siasa bali ni HISTORIA YA MUDA MREFU, ambayo ndani yake kuna Uarabu, Uafrika, Utumwa, Uislamu na Ukristo.....

WE CALL A SPADE, A SPADE......
 
Basra, Iraqi

Many of them are descendants of African slaves brought to Iraq. Many Iraqis still refer to them by their ancestral name, abeed - meaning slaves.

Hawa weusi (Bantus) ndiyo walianzisha The Zanj Rebellion dhidi ya Abbasid Caliphate mwaka 869.
 
Wote tu waliku wa ovyo....huko kwa wazungu walisitisha biashara ya utumwa baada ya mapinduzi ya viwanda, walikuja kua na mashine zinazowasaidia kwenye uzalishaji kwa gharama nafuu kwahio hawakua na nia tena na watumwa ,kikubwa walitaka wanabaki kwenye maeneo yao ili wawe soko la bidhaa zao na kuwazalishia malighafi za viwanda vyao.......hakuna mwema hapo kila mtu alifanya maamuzi yake tokana na maslahi yake hakuna aliempenda mtu mweusi, mzungu kamaliza utumwa ila akaja kukutawala hukuhuku kwenye nchi yako na hii ilitokea baada ya mapinduzi ya viwanda
 
Hizi ni poropaganda na fitna tu. Waarabu hawakuwa na tatizo na waafrika. Walitupenda sana na tuliishi nao kwa amani na upendo. Hizi mnaleta ni chuki tu..hata mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni chuki tu dhidi ya waarabu. Mtapata laana kubwa kuwa singizia waarabu. Hawana baya kabisa na watu.
Baada ya kupakwa futa la mawese ......umeanza kusifia shughuli Yao......daaa aiseee waswahili mna kazi
 
Uarabu ni rangi, nasaba au bara atokalo mtu ? Maana hata Afrika kama South Africa wazungu wanajihesabu kuwa ni waafrika kwa sababu wamelowea zaidi ya miaka 400. Hata Sultan wa Zanzibar na watu wengine kama walijinasibu kuwa ni waafrika lakini kama walifanya vitendo visivyokubalika basi tunyamaze tuseme hewala yalikwisha tufanye ni siri.

Tujiulize kwanini watu wa rangi zote Africa ya kusini waliokuwa ktk vyama vya ANC, PAC walipinga ubaguzi wa rangi uliokuwa unaendekezwa na waafrika wenzao wenye rangi nyeupe.

Je harakati hizo zilizopinga utumwa Afrika mashariki na ya kati katika dola kubwa ya Zanzibar zina utofauti gani na zile za kupinga ubaguzi Afrika ya Kusini.

Au ubaguzi za rangi ni mbaya zaidi ya utumwa au namna yoyote inayo mnyanyasa mtu utu wake uwe ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa nafasi za mamlaka(siasa) , biashara ya utumwa au ukoloni lazima upingwe na kukemewa pia haustahili historia yake ifukiwe kwa kuwa ni wenzetu hivyo tusikumbushane madhila ya ubaguzi, utumwa na ukoloni?


Blackpast

27 Mar 2016 — Zanzibar was separated from Oman after Said's death in 1856 when his son Majid bin Said became the first sultan of Zanzibar
Uarabu una definition nyingi it depend unatumia definition ipi.

Mkuu Hao walioishi na waarabu hawakugombana nao, kila siku Nasema humu the way wazee wetu wa kiarabu walivyoishi unakuta Mmoja anaishi kijiji hiki, mwengine anaishi kijiji kingine, tofauti na Wahindi na wazungu waarabu si watu wa mjini utawakuta mashambani huko wanafanya biashara na kulima minazi, Kama kweli wangekuwa wanafanya vitu against wazawa, wanawatesa na Kuwanyanyasa why wadumu maelfu ya miaka? Kwanini hawajapigana vita ya mara kwa mara kama Wareno ama wajerumani?

Historia ipo ila Tunataka tu kuifumbia macho tutafute ng'ombe Wa kafara.

Hio link sijafahamu niangalie nini Nimesema ni mambo ya kawaida tu.
 
Mkuu, Oman is a mixed race community tofauti na nchi nyingi za kiarabu. Inafurahia sana kuona waarabu na waafrika wanaaishi vizuri kwa amani. Hili ni jambo jema sana machoni kwa mwenyezi Mungu. Binafsi napenda kuona Oman na Tanganyika tunaishi kwa upendo kwasababu tuna undugu wa muda mrefu (Hatujakutana Barabarani) ambao uko kwenye damu na siyo siasa. Tunazungumza hadi lugha moja, jambo ambalo siyo dogo na la kupuuzwa......

Japo, ili uhusiano wetu uwe imara na makosa kama haya yasijirudie katika vizazi vijavyo ni lazima tukiri ukweli kwamba biashara ya utumwa ilifanywa baina ya machifu wa kiafrika pamoja na waarabu. Ushahidi mkubwa upo na mikataba hiyo baina ya Masultani wa Zanzibar na Waingereza kuhusu utumwa upo. Mimi binafsi nimeona nyaraka za Ministry of Foreign Affairs zikionyesha Sultan wa Zanzibar akilalamika kwanini hakuhusishwa kwenye mkutano wa Berlin 1884-1885, ambao uligawa Afrika.

Aliwaandikia Waingereza na Wajerumani barua (Diplomatic Note) kusema kwamba majimbo ya Arusha (Aruscha) na Moshi (Moschi) yalikuwa chini ya utawala wa Sultan wa Zanzibar, kwasababu machifu wa Kaskazini walikubaliana iwe hivyo. Mambo kama haya yasipowekwa wazi kisa hofu ya kuwakwaza baadhi ya watu, basi nadhani tutakuwa tunayaweka mahusiano baina ya Tanganyika, Zanzibar na Oman kwenye ukurasa mbaya.

Kile kilichotokea mwaka 1964 kikifanywa na wakina Mzee Nyerere, Karume, Okello na Kambona kilikuwa ni mauaji ya kimbari (Genocide), pia kilichofanywa na Mzee Mkapa mwaka 2001 kule Pemba nacho kilikuwa ni mauji ya kimbari (Genocide). Hata Mzee Nyerere alijutia kabla hajafariki, na Mzee Mkapa naye amejutia. Hakuna kutetea, wala kupunguza uzito wa kilichofanyika, iwe kilifanywa na mweusi au mwarabu. Udhalimu dhidi ya binadamu mwenzako kwasababu ya rangi au dini ni tabia ya kishenzi na kishetani.

Sasa, tusipokuwa wawazi na kutafuta suluhu nadhani haya mambo hayawezi kuisha vizuri. Mpaka leo hii, Muungano unasumbua, chanzo siyo siasa bali ni HISTORIA YA MUDA MREFU, ambayo ndani yake kuna Uarabu, Uafrika, Utumwa, Uislamu na Ukristo.....

WE CALL A SPADE, A SPADE......
Amani Mkuu, nimefurahi kuongea na wewe, na nakubaliana na ulichoandika.
 
Maandishi yalosema binadamu wa kwanza alikuwa nyani unapaswa kuyachunguza ili kuyaamini hata yakisemwa bahari ina maji ya chumvi
 
waarabu hawakugombana nao, kila siku Nasema humu the way wazee wetu wa kiarabu walivyoishi unakuta Mmoja anaishi kijiji hiki,

Hata kule Afrika ya Kusini wapo waafrika ya kusini weupe wakati wa ubaguzi waliishi vizuri na wabantu na kujiunga siasa ktk vyama vya ANC, PAC, Communist party of South Afrika. Baadhi ya Waafrika ya Kusini weupe walichukizwa na siasa za kibaguzi na wala hawakuona ni sahihi kuwabagua waafrika wenzao kwa kutumia rangi.


Kwa Zanzibar pia kuna waarabu wazanzibari walijiunga na UMMA Party, ASP kwa kuwa waliona sera za usawa zisizojali rangi zilikuwa nzuri kwa mustakabali wa nchi yao Zanzibar.

Ma comrade wa UMMA party Zanzibar bila kujali rangi, nasaba n.k waliunda chama kilichopinga uonevu bila kujali rangi
1664117486357.png

Comrade Ali Issa Sultani a.k.a Shetani, mwanamapinduzi wa Zanzibar aliyataka usawa kwa wote.

Mapinduzi Daima – Revolution Forever: Using the 1964 Revolution
in Nationalistic Political Discourses in Zanzibar . Source :


Joe Slovo muafrika wa kusini mweupe aliyepinga sera za kibaguzi Afrika ya Kusini

Joe Slovo
Former Minister of Human Settlements of South Africa

1664116828811.jpeg

Joe Slovo was a South African politician, and an opponent of the apartheid system. A Marxist-Leninist, he was a long-time leader and theorist in the South African Communist Party, a leading member of the African National Congress, and a commander of the ANC's military wing Umkhonto we Sizwe
 
Hata kule Afrika ya Kusini wapo waafrika ya kusini weupe wakati wa ubaguzi waliishi vizuri na wabantu na kujiunga siasa ktk vyama vya ANC, PAC, Communist party of South Afrika.


Kwa Zanzibar pia kuna waarabu wazanzibari walijiunga na UMMA Party, ASP kwa kuwa waliona sera za usawa zisizojali rangi zilikuwa nzuri kwa mustakabali wa nchi yao Zanzibar.
Ila South Africa kulikua na vita na resistance za kutosha, zilikuwepo hio miaka elfu ya waarabu pwani?

Even ukisoma Historia ya Kilwa mfalme hakuwa akiongoza makabila ya Africa bali ulikua tu ni kama umoja.
1. Aliinunua Kilwa toka kwa Mfalme Almuli (na sio kuvamia)
2.maeneo mengi ambayo Sultan aliongoza kulikuwa na mutual agreement na sultan aliweka tu ambasador wake, maeneo husika yalikuwa na Full Authority kujiongoza yenyewe.
3. Ilifanyika biashara kwamba kuna kuuza na kununua na sio kama ukoloni ambaye mfaidikaji alikua ni mmoja.

Kuna mambo mengi ya kuongelea ila kufananisha wazungu wa south na waarabu wa pwani ya Africa ni mbingu na ardhi.
 
Wanamapinduzi wa kiZanzibari waliokataa utumwa, Ukoloni, ubaguzi na usultani


Badawi Qullatein zama za uhai wake.
 
Wakoloni wote WaOmani, Waingereza, Portuguese, WaJeremani n.k wote walikuwa watesi wetu kwa namna zote.

Samora Machel : Ukoloni wa kiFikra



Katika hotuba yake motomoto kuhusu kutawaliwa, alihoji vipi mwafrika aliyetawaliwa na mfaransa akajiona m-bora kuliko mwingine kwa kuwa Ufaransa wana tamaduni bora zaidi ya uandishi wa mistari ya mashairi ya mapendo kwa umahiri wa kisomi.

Samora Machel anazidi kuwaza hata wale waliotawaliwa na muingereza wajiona wao ni bora kwa vile Uingereza ilitawala nchi nyingi zaidi na inasemekana ni wazungu 'wastaarabu' zaidi.

Samora Machel anatuasa ingawa Portugal ni nchi masikini zaidi ktk ulaya lakini ni nchi iliyoendekeza ukoloni kama Ufaransa, Uingereza na Ureno / Portugal na sifa za nchi zote hizo za ulaya ni kuwa ziliendekeza ukoloni.

Samora Machel anapigia mstari neno ukoloni na kuwa ukoloni ni unyama hauna utu hivyo kujisifia wewe ni zao la ukoloni huu au ule wenye hadhi ya juu ni kukosa fikra sahihi.

Hivyo maneno ya Samora Machel anasisitiza tuamke na kuwa mapambano lazima yaendelee (2022) dhidi ya ukabila, ujinga, maradhi, njaa, ushirikina na mawazo potofu ya kukumbatia ukoloni wa aina yoyote.

Anamalizia kuwa ukoloni wowote hauna usafi wa kujivunia kwani ni Ukoloni unaogandamiza jamii zingine na kuzigawanisha.
Ok
 
Wanamapinduzi wa kiZanzibari waliokataa utumwa, Ukoloni, ubaguzi na usultani


Badawi Qullatein zama za uhai wake.
Kulikuwa na wapinga serikali zanzibar ni tofauti na mapinduzi. Walikuwepo watu wanaopinga serikali kama vile ambavyo leo kuna Chadema wanaopinga CCM.

Ila kuhalalalisha mauaji ya maelfu ya watu wasio na silaha kwa sababu tu ya rangi yao ni jambo jengine, mkuu MALCOM LUMUMBA ameliongelea vizuri hapo juu.
 
Sheikh Ali Muhsin Barwani aelezea Hizbu kukataa ubaguzi miaka ya mwisho ya 1950 kuelekea uchaguzi 1961



Hizbu na harakati za kuwaunganisha watu wote Zanzibar wawe kitu kimoja, maana kulikuwa na mgawanyiko mganzija, bohora, shirazi, watumbatu, mzanzibara n.k

Pia Mzee Barwani anatupa chimbuko la Afro Shirazi na anakubali utumwa ulikuwepo kote, utumwa ulikuwepo mpaka 1920. Donda hili la utumwa, Hizbu walitaka kuliondoa maana 2/3 ya watumwa walishikiliwa na washirazi huku waarabu wakiwa 1/3 wakishikiliwa na waarabu anabainisha Mzee Barwani .

Source : MzeeBarwani
 
Historia inaonyesha hata Kalifeti (The Umayyad Caliphate) lilianguka na kupoteza majimbo yake mengi barani Afrika kwasababu ya ubaguzi wa waarabu dhidi ya waafrika na weusi. Kibaya zaidi ni kwamba kiongozi wa kalifeti alijisifia kabisa kudhamini huu ubaguzi. Lakini, pia hii tabia imezuka ya kupenda kusema kwamba mwarabu hakumfanyia mtu mweusi jambo baya kisa dini, nadhani siyo ya kiungwana.

Waarabu, wakishirikiana na machifu wa kiafrika walihusika kwenye biashara ya utumwa lakini wengi wenu kwasababu za kidini huwa mnapenda kupindisha ukweli. Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kwamba kuna mkataba wa kumaliza biashara ya utumwa uliosaniwa na dola la Zanzibar chini ya Sultan Bargash, na dila la Britania chini ya Malkia Victoria mnamo mwaka 1870, ambapo Bargash alikubali kufunga soko la watumwa Mkunazini.

Sasa wakuu, mnavyosema kwamba waarabu hawakufanya ubaguzi, wala biashara ya utumwa dhidi ya waafrika mnataka waungwana wawaelewaje labda?
Usichokijua ni kuwa utumwa ulikuwa ni mfumo kamili wa maisha duniani kote kwa nyakati tofauti. Tumesoma kwenye historia kidato cha tatu kuwa hata huku kwetu Afrika Mashariki kulikuwa na slave owning societies mfano mmojawapo ni Wanyakyusa. Hata Ulaya kulikuwa na utumwa na ndiyo maana Roxelana (Hurrem Sultan) alitekwa kwao Poland kama mtumwa na Wazungu wenzie akaja kuuzwa Constantinople akanunuliwa na Sultan Suleyman Khan wa Ottoman Empire na akamuoa. Wazungu ndio walioleta biashara ya utumwa Afrika japo utumwa ulikuwepo Afrika kabla ya hiyo biashara na walishirikiana na Machifu wa Kiafrika. Wareno wamefanya sana hiyo biashara kule Msumbiji na Angola.

Pia, sijui yule aliyemuuza Yusufu utumwani Misri naye ni Mwarabu? Chuki za kidini zisiwafanye mjitoe ufahamu. Nenda pale UDSM Library upande wa Special Reserve kuna encyclopedia kibao za slave trade zitakusaidia kutanua uelewa wako kwenye haya mambo.
 
Back
Top Bottom