Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha upumbavu sasa.Umekuwa mtu mzima unajua?Hizi ni poropaganda na fitna tu. Waarabu hawakuwa na tatizo na waafrika. Walitupenda sana na tuliishi nao kwa amani na upendo. Hizi mnaleta ni chuki tu..hata mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni chuki tu dhidi ya waarabu. Mtapata laana kubwa kuwa singizia waarabu. Hawana baya kabisa na watu.
Mkuu, hakujawahi kuwa na utumwa mzuri, uwe umefanywa na mweusi, mwarabu au mzungu.
Mkuu, Oman is a mixed race community tofauti na nchi nyingi za kiarabu. Nafurahia sana kuona waarabu na waafrika wanaaishi vizuri kwa amani. Hili ni jambo jema sana machoni kwa mwenyezi Mungu. Binafsi napenda kuona Oman na Tanganyika tunaishi kwa upendo kwasababu tuna undugu wa muda mrefu (Hatujakutana Barabarani) ambao uko kwenye damu na siyo siasa. Tunazungumza hadi lugha moja, jambo ambalo siyo dogo na la kupuuzwa......Mkuu mimi ni mwarabu na ni mu oman, Familia zetu wote hukosi watu weusi, tu naona na tunakaa pamoja, huo ubaguzi munauona Nyie. Njoo Tanga uone Familia za Ki oman zilivyomix rangi.
Oman ni nchi ya mixed race mamia ya miaka, watu weusi na waarabu wana exist pamoja that's why unakuta hadi royal family imeathirika hivyo.
Na Hakuna ubaguzi mbaya Mkuu kama systematic/institutional racism, Hao watu weusi walipata hizo nafasi uarabuni sababu mwarabu haamini doctor mweusi ni mbaya ama engineer mweusi hana uwezo kuliko mzungu etc. Ndio maana utakuta Qatar leo wanaenda kucheza World cup 2022 karibia nusu ya wachezaji ni WA Africa. Wangekuwa na systematic racism wangejaza wa Brazil kibao ila wamechukua WA Africa wadogo na kuwakuza.
At same time hizo nchi munazoona zimestaarabika zimejaa institutional racism.
Kuhusu hivyo vita Mkuu vina siasa na uisilamu, kihistoria dola ya kiisilamu Ile pure kabisa iliisha kwa Khalifa wa 4 yaani Alli, waliofuatia kama Umayyad caliphate even scholars wa kiisilamu utaona wana Criticize, na si Viongozi wote walikuwa ni wazuri, mfano Yazid kiongozi wa Umayyad alimuua mjukuu wa mtume, so mambo hayakuwa black and white, kuna complication nyingi na fitnah nyingi, si kila vita ni ya kidini.
Basra, Iraqi
Many of them are descendants of African slaves brought to Iraq. Many Iraqis still refer to them by their ancestral name, abeed - meaning slaves.
Baada ya kupakwa futa la mawese ......umeanza kusifia shughuli Yao......daaa aiseee waswahili mna kaziHizi ni poropaganda na fitna tu. Waarabu hawakuwa na tatizo na waafrika. Walitupenda sana na tuliishi nao kwa amani na upendo. Hizi mnaleta ni chuki tu..hata mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni chuki tu dhidi ya waarabu. Mtapata laana kubwa kuwa singizia waarabu. Hawana baya kabisa na watu.
Uarabu una definition nyingi it depend unatumia definition ipi.Uarabu ni rangi, nasaba au bara atokalo mtu ? Maana hata Afrika kama South Africa wazungu wanajihesabu kuwa ni waafrika kwa sababu wamelowea zaidi ya miaka 400. Hata Sultan wa Zanzibar na watu wengine kama walijinasibu kuwa ni waafrika lakini kama walifanya vitendo visivyokubalika basi tunyamaze tuseme hewala yalikwisha tufanye ni siri.
Tujiulize kwanini watu wa rangi zote Africa ya kusini waliokuwa ktk vyama vya ANC, PAC walipinga ubaguzi wa rangi uliokuwa unaendekezwa na waafrika wenzao wenye rangi nyeupe.
Je harakati hizo zilizopinga utumwa Afrika mashariki na ya kati katika dola kubwa ya Zanzibar zina utofauti gani na zile za kupinga ubaguzi Afrika ya Kusini.
Au ubaguzi za rangi ni mbaya zaidi ya utumwa au namna yoyote inayo mnyanyasa mtu utu wake uwe ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa nafasi za mamlaka(siasa) , biashara ya utumwa au ukoloni lazima upingwe na kukemewa pia haustahili historia yake ifukiwe kwa kuwa ni wenzetu hivyo tusikumbushane madhila ya ubaguzi, utumwa na ukoloni?
Blackpast
27 Mar 2016 — Zanzibar was separated from Oman after Said's death in 1856 when his son Majid bin Said became the first sultan of Zanzibar
Amani Mkuu, nimefurahi kuongea na wewe, na nakubaliana na ulichoandika.Mkuu, Oman is a mixed race community tofauti na nchi nyingi za kiarabu. Inafurahia sana kuona waarabu na waafrika wanaaishi vizuri kwa amani. Hili ni jambo jema sana machoni kwa mwenyezi Mungu. Binafsi napenda kuona Oman na Tanganyika tunaishi kwa upendo kwasababu tuna undugu wa muda mrefu (Hatujakutana Barabarani) ambao uko kwenye damu na siyo siasa. Tunazungumza hadi lugha moja, jambo ambalo siyo dogo na la kupuuzwa......
Japo, ili uhusiano wetu uwe imara na makosa kama haya yasijirudie katika vizazi vijavyo ni lazima tukiri ukweli kwamba biashara ya utumwa ilifanywa baina ya machifu wa kiafrika pamoja na waarabu. Ushahidi mkubwa upo na mikataba hiyo baina ya Masultani wa Zanzibar na Waingereza kuhusu utumwa upo. Mimi binafsi nimeona nyaraka za Ministry of Foreign Affairs zikionyesha Sultan wa Zanzibar akilalamika kwanini hakuhusishwa kwenye mkutano wa Berlin 1884-1885, ambao uligawa Afrika.
Aliwaandikia Waingereza na Wajerumani barua (Diplomatic Note) kusema kwamba majimbo ya Arusha (Aruscha) na Moshi (Moschi) yalikuwa chini ya utawala wa Sultan wa Zanzibar, kwasababu machifu wa Kaskazini walikubaliana iwe hivyo. Mambo kama haya yasipowekwa wazi kisa hofu ya kuwakwaza baadhi ya watu, basi nadhani tutakuwa tunayaweka mahusiano baina ya Tanganyika, Zanzibar na Oman kwenye ukurasa mbaya.
Kile kilichotokea mwaka 1964 kikifanywa na wakina Mzee Nyerere, Karume, Okello na Kambona kilikuwa ni mauaji ya kimbari (Genocide), pia kilichofanywa na Mzee Mkapa mwaka 2001 kule Pemba nacho kilikuwa ni mauji ya kimbari (Genocide). Hata Mzee Nyerere alijutia kabla hajafariki, na Mzee Mkapa naye amejutia. Hakuna kutetea, wala kupunguza uzito wa kilichofanyika, iwe kilifanywa na mweusi au mwarabu. Udhalimu dhidi ya binadamu mwenzako kwasababu ya rangi au dini ni tabia ya kishenzi na kishetani.
Sasa, tusipokuwa wawazi na kutafuta suluhu nadhani haya mambo hayawezi kuisha vizuri. Mpaka leo hii, Muungano unasumbua, chanzo siyo siasa bali ni HISTORIA YA MUDA MREFU, ambayo ndani yake kuna Uarabu, Uafrika, Utumwa, Uislamu na Ukristo.....
WE CALL A SPADE, A SPADE......
Kweli?Acha upumbavu sasa.Umekuwa mtu mzima unajua?
waarabu hawakugombana nao, kila siku Nasema humu the way wazee wetu wa kiarabu walivyoishi unakuta Mmoja anaishi kijiji hiki,
Ila South Africa kulikua na vita na resistance za kutosha, zilikuwepo hio miaka elfu ya waarabu pwani?Hata kule Afrika ya Kusini wapo waafrika ya kusini weupe wakati wa ubaguzi waliishi vizuri na wabantu na kujiunga siasa ktk vyama vya ANC, PAC, Communist party of South Afrika.
Kwa Zanzibar pia kuna waarabu wazanzibari walijiunga na UMMA Party, ASP kwa kuwa waliona sera za usawa zisizojali rangi zilikuwa nzuri kwa mustakabali wa nchi yao Zanzibar.
OkWakoloni wote WaOmani, Waingereza, Portuguese, WaJeremani n.k wote walikuwa watesi wetu kwa namna zote.
Samora Machel : Ukoloni wa kiFikra
Katika hotuba yake motomoto kuhusu kutawaliwa, alihoji vipi mwafrika aliyetawaliwa na mfaransa akajiona m-bora kuliko mwingine kwa kuwa Ufaransa wana tamaduni bora zaidi ya uandishi wa mistari ya mashairi ya mapendo kwa umahiri wa kisomi.
Samora Machel anazidi kuwaza hata wale waliotawaliwa na muingereza wajiona wao ni bora kwa vile Uingereza ilitawala nchi nyingi zaidi na inasemekana ni wazungu 'wastaarabu' zaidi.
Samora Machel anatuasa ingawa Portugal ni nchi masikini zaidi ktk ulaya lakini ni nchi iliyoendekeza ukoloni kama Ufaransa, Uingereza na Ureno / Portugal na sifa za nchi zote hizo za ulaya ni kuwa ziliendekeza ukoloni.
Samora Machel anapigia mstari neno ukoloni na kuwa ukoloni ni unyama hauna utu hivyo kujisifia wewe ni zao la ukoloni huu au ule wenye hadhi ya juu ni kukosa fikra sahihi.
Hivyo maneno ya Samora Machel anasisitiza tuamke na kuwa mapambano lazima yaendelee (2022) dhidi ya ukabila, ujinga, maradhi, njaa, ushirikina na mawazo potofu ya kukumbatia ukoloni wa aina yoyote.
Anamalizia kuwa ukoloni wowote hauna usafi wa kujivunia kwani ni Ukoloni unaogandamiza jamii zingine na kuzigawanisha.
Kulikuwa na wapinga serikali zanzibar ni tofauti na mapinduzi. Walikuwepo watu wanaopinga serikali kama vile ambavyo leo kuna Chadema wanaopinga CCM.
Usichokijua ni kuwa utumwa ulikuwa ni mfumo kamili wa maisha duniani kote kwa nyakati tofauti. Tumesoma kwenye historia kidato cha tatu kuwa hata huku kwetu Afrika Mashariki kulikuwa na slave owning societies mfano mmojawapo ni Wanyakyusa. Hata Ulaya kulikuwa na utumwa na ndiyo maana Roxelana (Hurrem Sultan) alitekwa kwao Poland kama mtumwa na Wazungu wenzie akaja kuuzwa Constantinople akanunuliwa na Sultan Suleyman Khan wa Ottoman Empire na akamuoa. Wazungu ndio walioleta biashara ya utumwa Afrika japo utumwa ulikuwepo Afrika kabla ya hiyo biashara na walishirikiana na Machifu wa Kiafrika. Wareno wamefanya sana hiyo biashara kule Msumbiji na Angola.Historia inaonyesha hata Kalifeti (The Umayyad Caliphate) lilianguka na kupoteza majimbo yake mengi barani Afrika kwasababu ya ubaguzi wa waarabu dhidi ya waafrika na weusi. Kibaya zaidi ni kwamba kiongozi wa kalifeti alijisifia kabisa kudhamini huu ubaguzi. Lakini, pia hii tabia imezuka ya kupenda kusema kwamba mwarabu hakumfanyia mtu mweusi jambo baya kisa dini, nadhani siyo ya kiungwana.
Waarabu, wakishirikiana na machifu wa kiafrika walihusika kwenye biashara ya utumwa lakini wengi wenu kwasababu za kidini huwa mnapenda kupindisha ukweli. Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kwamba kuna mkataba wa kumaliza biashara ya utumwa uliosaniwa na dola la Zanzibar chini ya Sultan Bargash, na dila la Britania chini ya Malkia Victoria mnamo mwaka 1870, ambapo Bargash alikubali kufunga soko la watumwa Mkunazini.
Sasa wakuu, mnavyosema kwamba waarabu hawakufanya ubaguzi, wala biashara ya utumwa dhidi ya waafrika mnataka waungwana wawaelewaje labda?