Kumbe Waarabu walikuwa watu wabaya kiasi hiki, yadumu mapinduzi matukufu ya Zanzibar

Kumbe Waarabu walikuwa watu wabaya kiasi hiki, yadumu mapinduzi matukufu ya Zanzibar

Usichokijua ni kuwa utumwa ulikuwa ni mfumo kamili wa maisha duniani kote kwa nyakati tofauti. Tumesoma kwenye historia kidato cha tatu kuwa hata huku kwetu Afrika Mashariki kulikuwa na slave owning societies mfano mmojawapo ni Wanyakyusa. Hata Ulaya kulikuwa na utumwa na ndiyo maana Roxelana (Hurrem Sultan) alitekwa kwao Poland kama mtumwa na Wazungu wenzie akaja kuuzwa Constantinople akanunuliwa na Sultan Suleyman Khan wa Ottoman Empire na akamuoa. Wazungu ndio walioleta biashara ya utumwa Afrika japo utumwa ulikuwepo Afrika kabla ya hiyo biashara na walishirikiana na Machifu wa Kiafrika. Wareno wamefanya sana hiyo biashara kule Msumbiji na Angola.

Pia, sijui yule aliyemuuza Yusufu utumwani Misri naye ni Mwarabu? Chuki za kidini zisiwafanye mjitoe ufahamu. Nenda pale UDSM Library upande wa Special Reserve kuna encyclopedia kibao za slave trade zitakusaidia kutanua uelewa wako kwenye haya mambo.
Utumwa hata kama ukifanywa na Malaika wa mbinguni, haiondoi uhalisia kwamba ni USHENZI. Pia hata kama ulikuwa ni mfumo wa maisha, haiupi uhalali wowote ule. CHAUVINISM IS NOT, AND WILL NEVER BE RATIONAL. Nashangaa kuona mnavyotetea huu ufedhuli kana kwamba ni kitu cha kujivunia sana. Waarabu wenyewe wanakiri kwamba walihusika na biashara ya utumwa, lakini ninyi mlioletewa dini na mashua mnakomaa na kubisha kivu ambacho kipo.

Hii hapa ni Video ya marehemu Muhamar Gaddafi wa Libya akiomba msamaha kwa niaba ya waarabu kwasababu ya biashara ya utumwa. Mwarabu aliyekuletea wewe dini anakiri makosa mbele ya wenzake, lakini wewe mwafrika unaendelea kubishana na ushahidi ambao upo. ACHA UNAFIKI MKUU:
 
lakini wewe mwafrika unaendelea kubishana na ushahidi ambao upo

Mifano ya historia ipo kibao, na waafrika tunapewa habari za kuwa tulifanyiwa utumwa lakini tunajaribu kufukia ukweli huku wenzetu wanahifadhi historia hiyo ili wasifanye tena biashara ya utumwa.
 
Mifano ya historia ipo kibao, na waafrika tunapewa habari za kuwa tulifanyiwa utumwa lakini tunajaribu kufukia ukweli huku wenzetu wanajifadhi historia hiyo ili wasifanye tena biashara ya utumwa.
It is immoral to downplay slavery, eti kisa utumwa ulifanywa na makabila ya kiafrika au mataifa ya watu waliotuletea dini. Mtu yoyote yule muungwana na mwenye akili timamu, ni lazima aulaani na kuuchukia utumwa, bila kijalisha ulifanywa na nani. Hata Papa Francis mwenyewe alikiri na kuomba msamaha kwa Wayahudi kwa makosa ambayo kanisa lake liliwafanyia miaka zaidi ya 500 iliyopita kule Uhispania. Juzi, tena kule nchini Canada ameomba msamaha kwa wahindi wekundu waliouwawa na viongozi wa kanisa lile miaka mingi iliyopita.......

......................Romanticising slavery and racism, defies the common precepts of descency.........
 
Mkuu, hakujawahi kuwa na utumwa mzuri, uwe umefanywa na mweusi, mwarabu au mzungu. Mwarabu anaendelea kulalamikiwa kwasababu hapendi kukubali ukweli kwamba alifanya biashara ya utumwa. Wazungu huwa wanakubali makosa na wengi wao wamejitahidi sana kubadilika, lakini waarabu mpaka leo hii wamekumbatia biashara ya kishenzi kama utumwa na ubaguzi wa rangi.
Wazungu hawajaacha utumwa mpaka leo, wamebadilisha style tu
 
Hizi ni poropaganda na fitna tu. Waarabu hawakuwa na tatizo na waafrika. Walitupenda sana na tuliishi nao kwa amani na upendo. Hizi mnaleta ni chuki tu..hata mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni chuki tu dhidi ya waarabu. Mtapata laana kubwa kuwa singizia waarabu. Hawana baya kabisa na watu.
Inasemwa katika records, asilimia 80 ya watumwa walikwenda Asia. Tatizo baada ya ukoloni hakuna watu weusi huko, sadaka yake tunawaona Amerika ya Kusini walikokwenda wachache. Waafrika walipelekwa Arabuni waliishia wapi?
 
Inasemwa katika records, asilimia 80 ya watumwa walikwenda Asia. Tatizo baada a ukoloni hakuna watu weusi huko, sadaka yake tunawaona Amerika ya Kusini walikokwenda wachache. Waafrika walipelekwa Arabuni waliishia wapi?
Aliyesema hivyo ni mtumwa wa Waroma Nyerere?
 
Back
Top Bottom