MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Utumwa hata kama ukifanywa na Malaika wa mbinguni, haiondoi uhalisia kwamba ni USHENZI. Pia hata kama ulikuwa ni mfumo wa maisha, haiupi uhalali wowote ule. CHAUVINISM IS NOT, AND WILL NEVER BE RATIONAL. Nashangaa kuona mnavyotetea huu ufedhuli kana kwamba ni kitu cha kujivunia sana. Waarabu wenyewe wanakiri kwamba walihusika na biashara ya utumwa, lakini ninyi mlioletewa dini na mashua mnakomaa na kubisha kivu ambacho kipo.Usichokijua ni kuwa utumwa ulikuwa ni mfumo kamili wa maisha duniani kote kwa nyakati tofauti. Tumesoma kwenye historia kidato cha tatu kuwa hata huku kwetu Afrika Mashariki kulikuwa na slave owning societies mfano mmojawapo ni Wanyakyusa. Hata Ulaya kulikuwa na utumwa na ndiyo maana Roxelana (Hurrem Sultan) alitekwa kwao Poland kama mtumwa na Wazungu wenzie akaja kuuzwa Constantinople akanunuliwa na Sultan Suleyman Khan wa Ottoman Empire na akamuoa. Wazungu ndio walioleta biashara ya utumwa Afrika japo utumwa ulikuwepo Afrika kabla ya hiyo biashara na walishirikiana na Machifu wa Kiafrika. Wareno wamefanya sana hiyo biashara kule Msumbiji na Angola.
Pia, sijui yule aliyemuuza Yusufu utumwani Misri naye ni Mwarabu? Chuki za kidini zisiwafanye mjitoe ufahamu. Nenda pale UDSM Library upande wa Special Reserve kuna encyclopedia kibao za slave trade zitakusaidia kutanua uelewa wako kwenye haya mambo.
Hii hapa ni Video ya marehemu Muhamar Gaddafi wa Libya akiomba msamaha kwa niaba ya waarabu kwasababu ya biashara ya utumwa. Mwarabu aliyekuletea wewe dini anakiri makosa mbele ya wenzake, lakini wewe mwafrika unaendelea kubishana na ushahidi ambao upo. ACHA UNAFIKI MKUU: