Mkuu iko hivi, ni wachache sana wanaoweza tofautisha sare za jeshi letu na za nchi zingine kwa kuwa zinafanana kwa kiasi fulani, wengi wakiona mabaka baka wanajua ni za jWtZ, hivyo mtu akivaa na kufanya uhalifu lawama zinarudi kwa jeshi letu, kwahyo wao wameamua kupunguza hilo
Sent from my TECNO KB8 using
JamiiForums mobile app
Tundu la panya halizibwi kwa mkate.
Anaekamatwa kwa uhalifu huku akiwa na sare za JWTZ awajibishwe kwa mujibu wa sheria na wale wote waliowezesha yeye kupata hizo uniform nao wawajibishwe.
Elimu kuhusu JWTZ, JKT, SUMAJKT, POLICETZ zitolewe nchini kote kwa uendelevu Kama zilivyo kampeni za makampuni ya Betting kwenye vituo vya Tv na Radio na Mitandao ya kijamii.
Wanajeshi warudi kwenye jamii. Washirikiane na jamii katika kazi mbali mbali za ujenzi wa taifa. Washiriki matukio ya kijamii yatakayowapa fursa ya kujumuika na jamii bila vikwazo wala vizingiti vya nidhamu ya uoga na Vitisho vya udhalilishaji.
Wanajeshi wawe sehemu ya jamii Kama ilivyokusudiwa wakati wa uumbwaji wao na kupewa majina [emoji117] JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA na JESHI LA KUJENGA TAIFA + SHIRIKA LA UZALIZASHAJI MALI JKT.
Kuna watanzania wapo nchi hii hii na hawaijui bendera ya Tanzania na wala hawajui kwamba tunayo bendera ya Tanganyika.
Uzalendo juu ya chochote hautengenezwi kwa vitisho ama manyanyaso, binaadam sio mbwa, utii wake Una kikomo kulingana na uwezo wa uvumilivu wake.
Wananchi wanapaswa kupenda vya nyumbani kwao na sio vya majirani Kama mipaka shume.
Uoga huzaa chuki, Chuki huzaa uovu, Uovu huzaa dhambi na Dhambi huzaa Mauti.
Hivi yule binti (nyumba ndogo) aliyejipiga Selfie na uniform ya sijui kanali mwaka 2016/2017 akatuwekea Facebook aliishia wapi?