Kumbe Watanganyika wanaweza kushikamana na kuongea sauti moja kwa ukubwa wake!

Wakisusiwa mapambano yao wasilalamike, watarudi walikotoka..ngumi zilikuwa hazina thamani na mabondia walikuwa na majina makubwa bila vipato.Haya acha tuone tukivuka D9 hali itakuwaje kama mabondia wakiingilia waandamanaji.
 
Hao mabondia hawajaona wala kusikia kilio cha wanamuziki na waigizaji? Watalia kilio ambacho hawajawahi kulia na wasimpate wakuwabembeleza. Sijui kina nani wataingia kwenye michezo yao ya ngumi. Ohooooo!!!!!
🤣
 
Hii spirit ya GenZ imekumbusha hili shairi la Claude Mckay "If we Must Die" nilisoma high school. Hawa watoto wamekataa kufa kinyonge. Hili shairi liliandikwa na Claude McKay wakati wa "Red Summer" ya 1919 nchini Marekani, wakati vurugu za kipinga ubaguzi kwa jamii ya Watu Weusi.

Lilito
wito wa kudai haki dhidi ya ukandamizaji. McKay anasisitiza kwamba hata kama wamezidiwa nguvu lazima wapigane ili damu yao isimwagike bure.

" If We Must Die"

If we must die, let it not be like hogs
Hunted and penned in an inglorious spot,
While round us bark the mad and hungry dogs,
Making their mock at our accursed lot.

If we must die, O let us nobly die,
So that our precious blood may not be shed
In vain; then even the monsters we defy
Shall be constrained to honor us though dead!

O kinsmen! We must meet the common foe!
Though far outnumbered let us show us brave,
And for their thousand blows deal one death-blow!

What though before us lies the open grave?

Like men we’ll face the murderous, cowardly pack,
Pressed to the wall, dying, but fighting back!

Tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi

"Kama ni lazima Tufe"

Kama ni lazima tufe, isiwe kama nguruwe,
Tukiwindwa na kubananishwa kwa aibu,
Huku mbwa vichaa na wenye uchu wakibweka kutuzunguka,
Wakitucheka na kutudhihaki
Wakililaani kundi letu na kuliita la hovyo.

Kama ni lazima, basi tufe kwa heshima,
Ili damu yetu hii ya thamani isipotee bure;
Hata madhalimu tunaowapinga
Walazimike kutuheshimu hata tukiwa tumefariki!

Enyi ndugu zangu! Tupambane na adui wa taifa letu!
Hata kama wametuzidi idadi na nguvu, tuonyeshe ujasiri,
Na kwa mapigo yao elfu, sisi tupige pigo moja la kifo!

Hata kama mbele yetu kuna kaburi la wazi
Kama wanaume, lazima tukabiliane na genge hili la wauaji, wenye hofu,waoga, wakitembea kwa makundi,

Tupambane kijasiri! Hata kama tukisukumwa ukutani, karibu ya kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…