Kumbe Yesu alikua mfuasi wa Buddha

umekuja na mifano yako sasa.nabii tito
 
Nadhan tunaambiwa biblia ingeandika kila Yesu alichofanya basi dunia nzima ingejaa vitabu ndo maana yaliandikwa yale ambayo yanaweza kukuza imani
 
nadhani kikubwa nilichokiona ni kwamba karibia kila mtu anaeabudu nakuamini dini ambayo haimpingi yesu au nabii issa sote tupo kwenye njia moja ila ndio hivyo tunakazaga tuu vichwa kikubwa nimejifunza kwenye hii post sisi sote tunamuabudu MUNGU mmoja kwa dini zinazomkubali na kumuamini YESU au NABII ISSA
 
Ni kweli nadhani vitabu vyengine waliona vitachanganya watu au labda sababu waandishi walimjua zaidi yesu ujanani sana kuliko miaka hiyo unayosema ..au laΙ“da Ζ™ilichowekwa ndo muhimu zaidi wangeweka vitaΙ“u vyengine vilikuwa na mΙ“wemΙ“we nyingi kuliko kutoa kile kinachosaidia kukuza imani ya ukristo...ndo maana kuna kati ya machapisho ya hvyo vtaΙ“u vya injili kuna sehem wameweka mabano na kuandika kuwa yesu alifanya miujiza mingi zaidi Ζ΄a kilichoandikwa..
 
Kuna faida nyingi kwenye hoja yako.

Katika dunia ya sasa watu wanang'ang'ana na dini zao wakidhani ni ucha Mungu. Dini si Uchamungu bali ni mfumo wa kanuni, sheria pamoja na miongozo itakayomwezesha mtu kuwa mcha Mungu.

Hivyo kundi fulani kudai tu nabii fulani ni wetu na mwingine ni wetu, haina faida yoyote katika kumwabudu Mungu. Kikubwa ni kuwa manabii wote walieneza upendo pamoja na mambo ambayo yakitendwa na mja yatamfanya kuwa mcha Mungu.

Pia ni lazima waja wapate kusoma vitabu vyote vyenye kufunza elimu yaani Maandiko Matakatifu (Sacred scriptures) Pamoja na vitabu vya elimu (knowledge books) kwa kufanya hivyo tutaweza kupata utambuzi wa kweli pasipo kutishana wala kulaumiana.
 
Kwa hiyo mlitaka hata michezo ya kombolela sijui ukuti ukuti nayo ingeandikwa kwenye biblia
 
mleta mada asante kwa mada nzuri japo inaweza kua haina ukweli bali ni documentary za bbc zisizo n a mashiko.

lakini pia nimepitia maoni ya wadau kuhusiana na mada hii nimepata vya kujifunza vingi kuhusu imani yangu kwa Yesu na Mungu na wale walio ipokea imani hapo kabla.

ninachozidi kujua ni kua kuna vitu badso haviko sawa kwa habari za Yesu kama alivuo bainisha ndugu
zitto junior kwamba ni kikundi cha watu wachache walikaa waka amua hii iwe hivi ni hii iwe vile.

japo mimi ni mkatoliki nilie mtiifu na mkereketwa bado sisiti kutoa kosoa kwa kanisa langu kulitaka liitishe mtaguso mpya maana kume kucha mno.

hio ni moja kwa upande mwingine namuunga mkono ndugu mitale na midimu kwamba Yesu hivi au vile yote ya yote alizaliwa alikufa kwa msalba alifufuka na atarejea teena.

lakini kwa mujibu post kadha wa kadha zinazo endelea kujadiliwa hapa jamii intelligence kuna muonekano wa mapungufu makubwa yamebainika juu ya muundo wa Biblia, lakini pia zama hivi za leo kuna watu maarufu walio waalimu wa Biblia kama manabii mitume wachungai na waalimu na hapa kwetu tz wsapo sana , nawanatoa ushuhuda kwamba Mungu ame zungumza nao na kuwapa ujumbe na mafunua na mistari ya maandiko ya Biblia hii hii inayo onekana kupungua. swali langu kwa nini asiwaambie kitabu hicho mkitumiacho kimepungua. kweli mwakasege ameshindwa kugundua yalio fichwa hali yakua ni mwalimu mbobezi kwenye Biblia. au kanisa la kisabato lililo na utaalamu wa maandiko ya Biblia.

lakini iwe iwavyo uwepoi Kristo haupingiki na marejea yake hayazuiliki, yaliofichwa yatawekwa wazi kama umuhimu wake utakuwepo, ilaa hilo l,a kuwa ni mfuasi wa budha ni ngano\hadithi\tungo\ simulizi zilizo na mashaka makubwa sana juu ya ukweli wake.
nawatakieni kila jema..
 
πŸ˜€πŸ˜€ Yaani vitu vingine sijisumbuagi kusoma muda mwingine kwakweli
Kuna msemo wa zamani wa Kikorea usemao "Upanga hauwezi kuwa imara kama haujapita kwenye moto mkubwa na Kugongwa nyundo nyingi" kwa hiyo mtu hawezi sema yeye ni imara katika jambo kama hajaweza kuvikabili na kushinda vikwazo katika jambo tajwa.

Mimi huwa nasoma kila kitu pindi ninapopata nafasi na muda na nikiona Mashaka ndani yake hutafakari majibu na malengo ya jambo husika na nikikosa majibu huwashirikisha makundi mengine kama mjadala.

Huwa nafuata mawazo ya moja kati wa manabii wawili walioweka msingi wa sayansi Descartes (1596-1650) kupitia andiko lake la kitalaamu Discourse on Method, (1937) ambamo alielezea mfumo wa kisayansi wa kushuku na kuhoji kwa kusema tilia Mashaka kila jambo isipokua tu ule uwepo wako. Alisema asichoweza kutilia Mashaka yeye ni uwepo wake tu kwa kusema (cogito egro sum, "I think therefore I exist") Kwa msingi wake yeye husema huwezi kulihukumu jambo kwa hekima kama hujalitengenezea taharuki na kulichambua katika engo zote.

Tujifunze kuwa wavumilivu ndipo tutafanikiwa.
 
Ninayoyasoma sasa ndiyo nimekuwa najiuliza kila nikitembelea Monastery na temples za ki Buddha. Mafundisho, matendo ya monks ni sawa na watawa wa kikatoliki wale wa mwanzo. Kujinyima, kukaa kimya, kufunga, kutoa mali zao na wenyewe kubaki bila kitu, kujenga temples na mambo mengi.

Ukifika sehemu kama Nepal, Burma, Thailand ukaingia kwenye monastery ukaongea na watawa utashangaa. Kuhusu Bwana Yesu kuja far East, imesemwa na inaonekana kwenye maandiko ya zamani ambayo yapo kama miaka 1800 iliyopita. Meaning hawa watu wanamtaja myahudi aliyewajoin kule India about 200 AD. Ningeruhusiwa kupiga picha na kucopy maandishi ningeweka ila hawaruhusu sababu ni maandishi ya kale wanaogopa mionzi itayaharibu.

Tofauti ya wakatoliki (nataja hilo dhehebu sababu ndilo nalifahamu na limenilea) na wabudha ni kuwa Sisi tunaamini ukifa bila dhambi unakwenda Mbinguni, ukiwa na dhambi ndogo kidogo unakwenda toharani na kama mdhambi kabisa ni jehanam.

Budism tofauti. Ukifariki umekamilika, unakuwa Enlighten yaani wewe huwezi rudi tena soul yako inatulia. Ukiwa bado hujatenda mema ya kuridhisha, soul yako inaweza rudi ikiwa katika aina nyingine kama mnyama, mdudu, mti, whatever.

Christians tunaamini kuna Mungu mmoja, wenyewe hawaamini kuna Mungu ila kuna Enlightenment . Cha kushangaza wanasoma rosary kama sisi, wanachant kama watawa wetu wanavyofanya na mambo mengi. Inabidi mtu aone mwenyewe.
Samahani labda nimeongea nje ya mada ila na mimi nimekuwa nakuna kichwa kila nikiona hivi vitu.
 
Walikuwa na imani gani hao watu kabla ya ujio wa dini ya Buddha?
 
K
Walikuwa na imani gani hao watu kabla ya ujio wa dini ya Buddha?
Maeneo yote duniani yalikua na dini ndogo ndogo za kale ambazo hazikuwa zimeendelezwa sana. Dini hizo zilikua na matambiko mbalimbali ambayo yalifanywa ili kuleta ustawi wa jamii husika.

Subira kuna uzi utakuja na vile vile zipo nyuzi nyingine nyingi humu ndani zinazoelezea hizo dini za kale kwa kiwango fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…