Kumbe Yesu alikua mfuasi wa Buddha

Mimi kwa mtazamo wangu hizo unazoita dini ndogo ndogo huwa naita ni imani tu mbali mbali zenye kutegemea sababua mbalimbali,ila dini ndiyo hukusanya watu pamoja kwa imani moja kama hapo hiyo dini ya Buddha.

Na ndiyo huwa nadhani pengine waafrika hatukuwa na hicho kitu,tulikuwa tu na imani mbalimbali kutokana na aina ya watu wa eneo husika.
 
Mbona tangu amekufa na alipofufuka siku tatu hazifiki..umewahi kupiga hiyo hesabu...mkiambiwa ni nadharia za watu mnabisha...tena bible ya kingereza three days and three nights.!

Kwa mujibu bible alikufa saa sita mchana,ijumaa jioni knla sabato haijaanza akaingizwa kwenye kaburi bible haijasema landa aliondoka usiku ule ule au jumamosi ila jumapili asubuhi walikuta kaburi jeupe
Sasa piga hesabu alikaa kaburin ijumaa usiku jumamoss mchana na usiku(ambayo ni siku moja kamili) jumapili kaburi tupu kuna siki tatu hapo????
 
Sasa tuamini dini ipi??? mwongozo please
 
Ni kweli kabisa.
Ili imani fulani kukua na kuenea kwenye eneo kubwa ni lazima kuwe na mtu mwenye ushawishi, kipaji na ujuzi mujarabu utaomuwezesha kuikuza na kuipigania dini hiyo.

Mara nyingi dini hutumiwa kama nyenzo ya kuunganisha watu wa makundi mbalimbali kuwa kitu kimoja. Hivyo ili hilo liweze kufanikiwa ni lazima kuwepo na mkakati endelevu wa kuieneza dini/imani hiyo kwa makundi mengine yenye viimani vyao ili waviache na kufuata imini lengwa.

Ukiangalia dini zote zilizoenea kwenye maeneo makubwa na kujipatia wafuasi wengi zilikua kwenye mpangilio mzuri (well organized) pamoja na kuwa na machapisho mbalimbali yaliyopangwa vizuri well documented)

Ukiangalia kwa makini utaona dini kubwa karibu zote zimeanzia maeneo ya Mashariki ya Mbali (Confucianism, Taoism, Buddhism e.c.t) pamoja na Mashariki ya Kati (Islam, Christianity and Judaism). Kuna sababu kadhaa zinazotajwa kama msingi wa jambo hilo. Kwanza kabisa ni eneo hilo ndimo kulimogunduliwa maandishi ya kale kabisa kwa kupitia visukuku kama vile Rosetta stone manuscript yenye maandishi ya lugha mbalimbali za kale, vilevile ni katika maeneo ya Mesopotamia Iraqi ya sasa ndimo herufi za awali (Cuneiform) zilipoanzia katika jamii Ya Wasumeriani .

Mwisho niseme, kwa kukosa mfumo thabiti na teknologia iliyoendelezwa sana pamoja na ubinafsi Waafrika walishindwa kuunganisha jamii zao kupitia dini moja kubwa. Na kwa sababu hiyo ilikuwa ni raisi kwa kwa dini zao ndogo ndogo zilizoenea katika maeneo madogo kushindwa vibaya katika kukabiliana na zile za wageni ambazo zilikua kwenye mpangilio bora zaidi.
 
Pamoja na kwamba siiamini hi historia au niseme hivi, siiuamini hu ugunduzi mpya wa Yesu; nijuavyo ni hivi, ni ngumu sana kwa shetani kuanzisha DINI yeyote hapa duniani na ikubaliwe na wanadamu bila kumtaja YESU; YESU ndio mambo yote katika Mungu, remember BUDDHA ni miongoni mwa dini kongwe hapa duniani kuliko UKRISTO na uislamu but still Yesu lazima ahusishwe. Uislamu ulikuja almost miaka zaidi ya 620 tokea Yesu apae zake mbinguni kwa baba yake but was very difficult kuusambaza UISLAM bila kumuhusisha Yesu; swali ni hili; why only YESU na sio Mohamed, Daudi, Sulemani, Ibrahim au nabii yeyote!? Is because kwa Bwana Yesu, kila goti hupigwa na kila ULIMI hukiri kwamba yeye ni BWANA.
Anacho kifanya shetani ni hiki; anajaribu kuwabadirishia njia wanadamu kumuhusu Yesu, yaani anajua huwezi mtoa YEsu kwenye IMANI yoyote duniani so the best way is, potosha njia yake, watu waende kwenye njia tofauti na ile inayotakiwa.
 
Ukiambiwa wakristo wamejimilikisha Yesu ndiyo maana hata wewe umekuwa na huo mtazamo utasemaje mkuu?

Na ndiyo maana kuna wakristo wengine wanasema Issa na Yesu ni watu toauti kabisa na si mmoja,hii yote ni kujimilikisha Yesu kuona wao ndiyo wanahusika nae.
 
Hebu cheki hiyo;
 
Ndiyo maana mie sionagi maana haya malalamiko ya waafika kwamba wazungu na waarabu wameharibu dini zetu na kutuletea dini zao au sijui waafrika tumeacha imani zetu asili na kufuata imani za kigeni,halafu wanatolea mifano ya wachina huko na wahindi kwamba hadi leo bado wana imani zao.
 
Ukakasi ni kunitajia habari za mfalme nebkadreza..huyu jamaa alipatikana miaka ile kipindi cha daniel(kwa mujibu wa biblia) na kipindi hicho israel walikuwa utumwani..ni mbali mno kumuhusisha na yesu ambaye baada ya miaka mingi ndio anakuja kuzaliwa..sasa nebkadreza huyu ni yupi..ni uongo ambao haukuvaa ch***p *
 
Ni kweli Yesu hakuishi kipindi cha Nebukadrineza. Kwani Nebukadrineza alikua mtawala wa Babeli (Babylon) katika kipindi cha (605-562 BC) miaka karibu 500 kabla ya Yesu kuja duniani.

Alikua ni mtawala katili ayewatawala na kuwapeleka Wayahudi uhamishoni katika maeneo ya utawala wake. Hivyo kutokana na tukio hilo kulitokea makundi mengi ya Wayahudi kuwa na kuishi nje ya ardhi yao ya awali.

Hivyo mwandishi kwenye makala anapomtaja Nebukadrineza anakumbushia tukio la kihistoria la mtawala aliepelekea baadhi ya Wayahudi kuishi katika maeneo tajwa na Yesu kuweza kuwatembelea kwani hao walikua ndugu zake.
 
Mimi ni mmoja wao nisie amini kwamba Yesu na Issa ni mtu mmoja; Niambie hilo jila la Issa ni la lugha gani? Maanake Biblia za Kingereza Yesu zinamuita Jesus, ya Kiarabu Yesu inamuita YASU, Issa ni lugha gani!?
 
uhusiano ni mkubwa kwa kweli;
 
the jesus narrated in the bible never existed...period
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…