Ninayoyasoma sasa ndiyo nimekuwa najiuliza kila nikitembelea Monastery na temples za ki Buddha. Mafundisho, matendo ya monks ni sawa na watawa wa kikatoliki wale wa mwanzo. Kujinyima, kukaa kimya, kufunga, kutoa mali zao na wenyewe kubaki bila kitu, kujenga temples na mambo mengi.
Ukifika sehemu kama Nepal, Burma, Thailand ukaingia kwenye monastery ukaongea na watawa utashangaa. Kuhusu Bwana Yesu kuja far East, imesemwa na inaonekana kwenye maandiko ya zamani ambayo yapo kama miaka 1800 iliyopita. Meaning hawa watu wanamtaja myahudi aliyewajoin kule India about 200 AD. Ningeruhusiwa kupiga picha na kucopy maandishi ningeweka ila hawaruhusu sababu ni maandishi ya kale wanaogopa mionzi itayaharibu.
Tofauti ya wakatoliki (nataja hilo dhehebu sababu ndilo nalifahamu na limenilea) na wabudha ni kuwa Sisi tunaamini ukifa bila dhambi unakwenda Mbinguni, ukiwa na dhambi ndogo kidogo unakwenda toharani na kama mdhambi kabisa ni jehanam.
Budism tofauti. Ukifariki umekamilika, unakuwa Enlighten yaani wewe huwezi rudi tena soul yako inatulia. Ukiwa bado hujatenda mema ya kuridhisha, soul yako inaweza rudi ikiwa katika aina nyingine kama mnyama, mdudu, mti, whatever.
Christians tunaamini kuna Mungu mmoja, wenyewe hawaamini kuna Mungu ila kuna Enlightenment . Cha kushangaza wanasoma rosary kama sisi, wanachant kama watawa wetu wanavyofanya na mambo mengi. Inabidi mtu aone mwenyewe.
Samahani labda nimeongea nje ya mada ila na mimi nimekuwa nakuna kichwa kila nikiona hivi vitu.