KUMBUKIZI (2019): Magufuli alipompokonya Ardhi ya Ekari 1,000 Mohamed Kiluwa hadharani kwa udanganyifu

KUMBUKIZI (2019): Magufuli alipompokonya Ardhi ya Ekari 1,000 Mohamed Kiluwa hadharani kwa udanganyifu

Ozon

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
2,910
Reaction score
4,711
Tarehe 7 Juni 2019 aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayatui Magufuli alikutana na wafanyabiashara kutoka Kila Mkoa Ikulu ya jijini Dar es Salaam.

Ref: Ikulu, Dar: Rais Magufuli akutana na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka kila Wilaya nchini. Ataja changamoto za biashara kwa Serikali na Wafanyabiashara then hii - Serikali ya Tanzania yaishtukia Kiluwa Group, yaifutia hati ya ekari 1,000

Miongoni mwa wafanyabiashara waliofika Ikulu ni Mohammed Kiluwa wa Kiluwa Steel Group ambaye alinyang’anywa Ardhi Ekari 1,000 kwa udanganyifu.

Lukuvi alimkaanga ipasavyo, ana siri ya utapeli wa bwana huyu

=====
Story nzima hii:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali ilifuta hati ya umiliki wa eneo la ekari 1,000 iliyokuwa ikidaiwa kununuliwa na Kiluwa Group kwa sababu iliuzwa kinyume cha sheria.

Mbali na kuuzwa kinyume cha sheria, pia imethibitishwa kuwapo kwa udanganyifu mwingi katika kampuni hiyo ikiwemo kutomiliki viwanda bali kufanya kazi kama Kituo cha uwekezaji (TIC) kwa kuchukua ardhi na kukodisha kwa wengine.

Ameyasema hayo leo Ijumaa 7, 2019 wakati akijibu ombi la Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohammed Kiluwa aliyeomba aruhusiwe kufanya uendelezaji wa kujenga viwanda katika eneo hilo lililopo Mkoa wa Pwani, huku akiahidi kama atashindwa yuko tayari kufukuzwa nchini.

Lukuvi amesema katika eneo la Kibaha, gharama ya kununua ekari moja ya ardhi waliyopewa ni Sh5.8 milioni lakini suala hilo halikufanikiwa kutokana na kutetewa na Mkoa.

“Tuliambiwa msipowapa kwa Sh1 milioni, Mheshimiwa Rais anaweza kuwapa bure kama alivyowapa watu wa Bagamoyo kwa hiyo wakawauzia kinyume cha matarajio lakini kabla kazi hiyo haijafanyika, sijui kwa huruma ya namna gani Mkurugenzi, Mwenyekiti wa Halmashauri, Sekretari wa Mkuu wa Mkoa na mtu mwingine wa uwekezaji walipelekwa China kwanza.

“Waliporudi mambo yalibadilika na mambo mengine walirudi nayo mi nafikiri mtu wa Takukuru atajua baadaye na walikuja kuuza eneo kinyume cha bei ya matarajio ya Sh1 milioni kwa ekari na bado wakalazimishwa wapewe.”

Lukuvi amesema shamba lolote linapofutwa kwa amri ya Rais, Wizara ya Ardhi ndiyo inasimamia upangaji wa ardhi katika eneo hilo.

“Lakini baada ya halmashauri ya wilaya hiyo kuona hawawezi kumpa eneo hilo, wakampa viwanja vya mbele ekari 1,000 kwa bei ambayo hata wakazi wa eneo hilo walikuwa tayari kununua kwa bei hiyo.”

Mbali na hilo, pia Lukuvi amesema Kampuni ya Kiluwa kwa mujibu wa taarifa za Brela za leo, inamilikiwa na watu tofauti kama Kampuni ya Kamata kutoka Urusi yenye hisa 6,500, Mohammed Kiluwa, hisa 1,500, huku Kiluwa Steel Group wana hisa 2,500 katika eneo wanalotaka kulichukua.

“Huyu Mrusi aliwahi kuja ofisini kwangu anadai Sh4 bilioni ya fedha ambazo alimpatia Mohammed Kiluwa ili anunue eneo, lakini yeye alinunua kinyume na bei iliyokuwa imepangwa na kutumia Sh1 bilioni.

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Lukuvi hatakiwi kulaumiwa katika suala hilo kwa sababu uamuzi wa kufuta hati aliyatoa yeye huku akibainisha kuwa Kiluwa hata aende sehemu gani hawezi kulipata eneo hilo.

“Mimi nilimshangaa huyu Kiluwa, nilikuwa simjui nilipoona ameanza kuzungumza hilo suala, nikajiuliza huyu shetani amempandia wapi, yaani uchukue eneo kutoka kwa wananchi wengi umpe mtu mmoja,” alisema Rais Magufuli.

Amesema suala la Kiluwa kutokuwa mmiliki wa kiwanda hicho aliliona alipoenda kuzindua kiwanda chao katika eneo la Kibaha kwa sababu Wachina ndiyo walikuwa wanakitolea maelezo.

“Lakini nikasema ngoja ninyamaze kwa sababu mtu ameshakula asilimia zake na mimi ninachotaka ni viwanda bila kujali wewe ni mweupe au mweusi na tunatengeneza ajira na Serikali inakusanya kodi,” amesema Rais.

=====

VIDEO HII HAPA chini

=====

Waweza soma pia: Mohamed Kiluwa kashindwa kuendana na zama hizi
 
Thread 'Mkataba wa Kiluwa wa Trilioni 17 wa kujenga viwanda Pwani ni zaidi ya Utajiri wa Mo Dewji (Tajiri Namba Moja Afrika Mashariki)' Mkataba wa Kiluwa wa Trilioni 17 wa kujenga viwanda Pwani ni zaidi ya Utajiri wa Mo Dewji (Tajiri Namba Moja Afrika Mashariki)
1000326554.jpg
 
Mwamba ambaye inasemekana ndiye mmiliki wa KILUWA GROUP yuko Belarus anasaini mikataba ya billions of money kuja kuwekeza hapa bongo.

Kiluwa amewaambia Waandishi wa Habari kuwa uwekezaji huo utahusisha ujenzi wa Viwanda mbalimbali ikiwemo Viwanda vya kuunda trekta na mashine za kilimo, Viwanda vya kuunda Mabasi, Malori, Viwanda vya mashine na teknolojia za kilimo cha kisasa, dawa za binadamu na visa tiba pamoja na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za Viwandani kutoka Belarus bidhaa ambazo zitalihudumia soko la Tanzania na Nchi nyingine za Afrika. ​

Hizi kufuru hata Mo, Bakhresa na Manji hawajawahi kuzifanya. Nani yuko nyuma yake?

Ngoja tuone maana hizi mbanga hata Mzee wetu Reginald Mengi siku za mwisho mwisho za uhai wake naye alikuwa nazo plan kubwa sana za kuleta wawekezaji kujenga viwanda vya magari na vifaa vya elektroniki.
 
Huyu mwamba alivuma wakati fulani kwa kesi za ardhi. Hasa maeneo ya Pwani Kibaha Kama sikosei.

Alimiliki maeneo makubwa sana. Kuna kesi moja alipishana na wachina ambao waliingia mkataba nae.

Disclaimer: Inawezekana siyo huyu bali majina tu yanafanana.
 
Back
Top Bottom