Kumbukizi: G.Lema alimuonya Sabaya,yeye akatia kiburi

Kumbukizi: G.Lema alimuonya Sabaya,yeye akatia kiburi




Mkishauriwa kutenda haki muwe na masikio. Sabaya alionywa na Lema hakusikia.Leo yamemfika. Kwa mnaokumbuka vizuri Shujaa naye pia alionywa na huyu huyu Lema atende haki,hakusikia!
Na siku Mbowe akila mvua uje ushangilie hivyohivyo
 
Kuna watu Mungu huwatumia kupeleka ujumbe wakati mwengine,bahati mbaya wahusika mara nyingi hupuuza. Sasa Lema ya kwake haya hapa yanatimia. Na ya Magufuli yalitimia. Lumumba roho juu hawajui nani anayefuata kupewa ujumbe na Lema,huenda akawa Kingai.
 
Jamaa alikuwa na kiburi, dharau, na jeuri haswa, kumbe matumaini yake aliyaweka kwa mwanadamu asijue mwanadamu ni mavumbi na iko siku mavumbini atarejea.

Hii hukumu aliyopewa leo inatufundisha kumtumaini na kumtegemea Mungu.

Naye naamini kwa hukumu hii sasa amejua nani anastahili kutegemewa ndio maana leo baada ya hukumu yake kusomwa amesikika akisema "Mungu wake yuko kazini kumpigania".
 
Hivi lema Ana Nini kila akiongeacho kinatokea
Umewahi kusoma au kusimuliwa kile kisa cha hekaya za Abunuasi? Kuna jamaa alikuwa anakata tawi la mti huku amekaa upande anaokata na alipoambiwa likianguka utaanguka nalo lakini akabisha? Na lilipoanguka akaanguka nalo kama alivyoambiwa lakini yeye akabaki kushangaa kuwa yule aliyemuonya alijuaje? Basi na nakuhakikisha wala mtu hahitaji kisomo cha darasa la saba kujua kuwa aliyokuwa anatenda Sabaya yangekuwa na mwisho na tena mbaya. Pia Magufuli alivyokuwa anadharau suala la korona wakati alikuwa na tatizo la moyo, kuna watu wengi wengi tu walishaona kuna uwezekano mkubwa wa matokeo mabaya. Ninachotaka kusema ni kuwa hayo yaliyotokea siyo kwa sababu Lema aliyasema bali alitoa tahadhari pale alipoona mtu anakata tawi la mti alilolikalia.
 
Adhabu ya miaka 30 na kuchapwa viboko aliyopewa Ole Sabaya yafafanuliwa kwa kina, Na inapeleka gonzo dani kwa waliopo madarakani


  • Kupewa unifomu za gerezan
  • Kupangiwa genge na mnyapara
  • Mfungwa hupakwa dawa ya vidonda ya spirit kisha kutandikwa viboko
  • Magereza sasa yanajitegemea na hayati mwendazake Rais Magufuli aliagiza kila gereza lijitegemee hivyo Kazi za Kupasua mawe, kilimo, ujenzi n.k hufanywa
  • Hukumu hii ni funzo kwa vijana wenzetu wa CCM waliokuwa wakimuiga Ole Sabaya na kukubali kutumika vibaya na wakubwa
  • Waliopo madarakani watambue cheo ni dhamana hivyo watende haki na kutunga sheria za haki

Source : Mubashara Studio
 
Back
Top Bottom