KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

Namkumbuka Marehemu kuna Warsha/Semina au maonyesho ya watu ambao hawatumii nyama yalifanyika Diamond Jubilee miaka hiyo na nikiwa kijana mdogo nami nilienda hapo , pia kukiwa na mapishi mbalimbali ya Vegans & Vegetarians

Nikapata wasaa wa kuongea na Munga na bahati mbaya kwangu ni mimi ndo alinipa nafasi ya kunisikiliza zaidi kuliko yeye kujieleza ( anyway nafikiri ni ujana wangu na ujuaji na kuwa na taarifa nyingi bila mpangilio [emoji23]) japokuwa nilipaswa mimi kumsikiliza zaidi sababu nilikuja kugundua baadae nilikuwa naongea na Nguli wa Elimu ya utambuzi

Nafikiri alitaka sana kujua kutoka kwangu ilikuwaje nikawa nina shauku ya kutaka kujua mambo ambayo kwa mtizamo wa kawaida na wa kijamii sikuwa naonekana kama nita kuwa nina ufahamu wa hiyo Dunia, kwanza nilikuwa naonekana bwana mdogo mdogo sana kwa umri afu pia na kwa mtizamo wa nje nilikuwa nina ule muonekano wa wale vijana wa mjini mjini hivi

Nikamuambia mambo ya Mantra, meditation ya pumzi nayo fanya pia moja ya vitabu vilivyonipa hamasa kuanza kuutafuta ukweli kutoka ndani yangu, na kimoja ya hivyo vitabu ni kitabu nilichonunua tu randomly kwenye zile β€˜corridors’ za posta mpya wanao panga panga chini vitabu ambavyo vingi vimechakaa chakaa cha mwana dada wa kimarekani kama sikosei na jina lake Shirley MacLaine/ Maclain (Kama sijakosea jina) na jina la kitabu ni β€˜ Going Within’

Kipindi hicho tunaongea bado nilikuwa sijaanza rasmi kujitafuta zaidi ya kusoma vitabu mbalimbali vya utambuzi na meditation ya pumzi na ya maneno ( Mantra)


Baadae sana ndo nikaanza kufuatilia Magazeti ya Jitambue yalivyo anza kutoka na nikaanza kuujua ukubwa wa Nguli Tehenan

Ni mmoja wa watu/wana habari ambao walikuja ki tofauti zaidi na alijitahidi kuleta uelewa mkubwa kumuhusu binaadam na nguvu alizonazo za kuweza kuumba na kuharibu ( ambazo kila mtu anazo ni namna ya kuzijua na ku tap hiyo energy iliyo ndani ya kila mmoja wetu) na kujua kwamba ni binaadam anaweza umba/ tengeneza hatima na majaliwa yake

Pia nilisikia pia nae alikuwa influenced na mtu mmoja anaitwa Rashid Mbughuni ( sina uhakika na jina na hiyo tetesi) maana sikuwa karibu sana na Munga zaidi ya siku hiyo na sijakutana nae tena mpaka niliposikia amefariki na niliomboleza kimya kimya kuondokewa na mtu mkubwa ktk ngazi ya ufahamu

RIP Munga Tehenani

Asante sana Mshana Jr kutuletea kumbukizi tena ya huyu mwamba na tusherehekee Maisha yake na jitihada zake za kutaka tuujue ukubwa wetu, Barikiwa sana
 
Hakika ipo miamba ambayo ilifanikiwa kutimiza malengo yao katika makasha waliyopewa na sasa wameenda kutumika katika Ulimwengu mwingine...

Mbele yetu nyuma yako Mzee Munga
 
Habarini wapendwa poleni na msiba mkubwa wa kitaifa na misiba mingine ya ndugu jamaa na marafiki, ... Hongereni pia kwa sikukuu ya pasaka
Bado nakumbuka ahadi yangu kwenu ya kupata kazi za Munga na kuzirudufu kwa manufaa ya wengi.. Nitaendelea kuwapa updates hapa hapa kwenye hii mada yetu

SIJAWASAHAU....[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Gazeti la JITAMBUE hakika lilikuwa na thamani kubwa kuliko almasi. Lala salama MUNGA TEHENAN. Hakika kizuri hadumu!
 
Dah So sad Kupotea kwa Haya Magazeti.... Kiukweli ya kale Ni dhahabu
 
Mkuu tushirikishe Kidogo Makala hiyo....
 
Wakushi twamuenzi
 
Mkuu tushirikishe Kidogo Makala hiyo....
Nakala zangu zote za jitambue ziliharibiwa pindi nilipoondoka nyumbani. Ila ile mada ilihusu kujiwekea akiba kwa vikundi halafu mnajikopesha kulingana na uwezo wenu. Ila inahitaji nidhamu ya hali ya juu kufikia hili lengo.
Kwa ufupi tu ni hivyo mkuu.
 
Ndo Maana Nakukubali Sana... Wewe Ni Mmoja wa Member Muhimu Sana Mlionifanya nipende JF. Upo Wewe Bujibuji, Mkeo Faiza Fox, Preta na Mamndenyi.... Big up Sana Kaka kwa Mchango wako humu jamvini....
Mkeo Faiza Fox, [emoji16][emoji16][emoji16][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1548][emoji1752]
 
Mkeo Faiza Fox, [emoji16][emoji16][emoji16][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1548][emoji1752]
Mkuu mi niliyakuta humuhumu. Sasa Mimi Ni Nani nipingane na wahenga??? Ili Hali nilikuwa Mgeni?? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu mi niliyakuta humuhumu. Sasa Mimi Ni Nani nipingane na wahenga??? Ili Hali nilikuwa Mgeni?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3]sawa mkuu bi mkubwa yuko bukheri wa afya japo tumetengana kwa muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…