Kauli aliyoitoa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa ametoa nia kugombea ubunge Arusha mjini,
Kauli hii ni ukweli uliojificha kwa maana wengi huwa wanalaumu mitandaoni kwanini watu hawa hujionesha wanaipenda CCM, mfano katika tukio la juzi la harambee katika kuchangia 100Billions ni mfano mzuri kwani wafanya biashara na makampuni madhara yamejitokeza kuchangia mfano Afro oil, GSM, watu wa madini, young Africans SC, na watu binafsi.
Hizi zimezua hisia tofauti mfano wanayanga wenzangu tukio la yanga kuchangia 100M limezua hisia tofauti kwani club ina wanachama tofauti ambao wengine sio wana CCM itakuwaje na wao wakisema tunataka vyama vyetu vichangingiwe tofauti na CCM.
Ukweli ni huo aliousema Makonda taasisi ambazo ni NGO, kampuni na wafanyabishara kiuhalisia wanajilinda hapo kwamba ukialikwa alafu usitoe kuna namna unaweza ukawa mwenye kuwekewa vikwazo kama alivyosema Makonda, saa nyingine wanasiasa hujisahau wanaongea ukweli uliojificha ambao baadae hujiona waliongea si sehemu sahihi.
Ndio huwa kuna muda wanajisahau wanasema ukweli walioumeza mfano Nape akiwa waziri wa mawasiliano alisema uchaguzi na ushindi sio lazima uzingatie sanduku la kura nalo huzingatia nani anatangaza na akitangaza unamuomba Mungu amsamehe pale alipokosea.
Kuna muda nashindwa kuwalaumu ni kwasababu mifumo imeshaundwa iko hivyo ni ngumu kuikwepa ,ukikwepa unakuwa kama mtu haramu.
Marekebisho ya Katiba inayozingatia Ukomo wa madaraka katika mihimili mitatu yaani bunge,raisi na mahakama ni muhimu sana kwetu. Yaani namaanisha hiyo mihimili mitatu isiingiliane kila mmoja ufanye kazi yake basi tutakuwa na angalau uwajibikaji.