Hapa umegonga nyundo pahali pake.Watapita kimya kimya
Two wrongs don't make a right.... Huwezi justify JPM sio dikteta simply sababu ameua sawa tu na Mkapa!! That's madness!!
Kipindi Cha JPM ndio zimeletwa sheria kali za kubana uhuru wa maoni.
1. Sheria ya huduma ya habari.
2. Regulations za TCRA kwenye leseni za online Tv. Ilitakiwa upeleke ratiba ya vipindi Ina advance, ulipie million 1 kupata leseni n.k yote haya ku discourage watu kusikiliza bloggers wanaomkosoa JPM.
3. Sheria ya takwimu Ili mtu binafsi asichapishe utafiti huru au takwimu mpaka apate "vibali" yote hizi kupunguza tafiti mfano za Twaweza.
4. Sheria ya vyama vya siasa iliyompa mamlaka Msajili kuingilia internal procedure za chama.
5. Kufungia mikutano ya kisiasa ambayo ni haki kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.
6. Kwa mara ya kwanza 90% ya wagombea wa upinzani walienguliwa kwenye uchaguzi wa TAMISEMI.
7. Kwa mara ya kwanza ripoti ya bunge ilikabidhiwa kwa Rais yaani walikua hawawezi kupitisha maazimio juu ya wizi wa Tanzanite. More so alitoa order kwa Spika kuwatimua wapinzani Ili aje awashughulikie huku nje.
8. Hili ndio kubwa zaidi... Alituondoa kwenye open governance initiative Ili serikali isiwajibike kwa bunge au wananchi. Yaani Kulikua na usiri mkubwa sana wa mambo.
9. Alianzisha parallel bar Ili kuwaengua mawakili wa serikali TLS yote haya kuepuka "uanaharakati" wa TLS. yaani hofu ya kukosolewa akaona aunde parallel body!!
10. Alipunguza bajeti ya CAG kwa nusu Ili isiweze kuwa na capacity ya kukagua serikali. Ukisoma performance audit ya CAG wanasema licha ya bajeti ya NAO kupangwa na kamati ya bunge ila serikali ilitoa nusu pekee ya pesa yote Ili tu kuvuruga ukaguzi.
11. JPM alizuia utekelezaji wa sheria ya TEITI iliyotaka mikataba yote ipelekwe bungeni. Ieleweke ilipitishwa 2016 yeye akiwa Rais ila alipinga mikataba kuwekwa wazi kwa kuhofia wapinzan kupata pointi bungeni.
Mifano ni mingi ila udikteta wa JPM unapimwa kwa mengi tu aliyowazidi JK na Mkapa na sio vifo pekee.
Cc
Carlos The Jackal Nyamizi Msanii
Naomba mjibu hizi hoja one by one na mtueleze why asiwe dikteta.